ACE
Encyclopaedia   Mada   Mifumo ya Uchaguzi   Uchunguzi wa Mifumo ya Uchaguzi  
Bolivia: Mabadiliko ya Uchaguzi katika Marekani Kusini

 

 

Tajriba ya demokrasia nchini Bolivia imeonyeshwa na utafutaji wa njia za kusuluhisha tatizo la kimsingi la tawala za marais wa Marekani Kusini, ambazo mara nyingi zimeishia katika kukwama kati ya tawi endeshaji la serikali na wabunge wakiongozwa na wale kutoka kwenye vyama vidogo bungeni. Mifumo mingi ya urais katika Marekani Kusini hutokeza tatizo kubwa kwa kuwa katika mifumo ya siasa za vyama vingi na uwakilishi sawa; hili limeelezwa kama “tatizo la urais”, na limekuwa chanzo cha kudumu cha mizozo ya kisiasa hali ambayo imetatiza uwezo wa kudumisha demokrasia.

Nchini Bolivia, tatizo limetatuliwa kwa kiwango fulani kupitia kwa mabadiliko mepesi ya kiasasi kutoka kwa “mfumo rais” huku serikali ndogo hadi kwa “mfumo rais unaotokana na bunge” katika serikali kubwa. Mfumo huu tofauti wa serikali ni “mtoto za kimestizo”, ulio na sifa zote mbili za mfumo bunge na mfumo rais. Ni mfumo rais kwa sababu rais huwa mamlakani kwa kipindi fulani maalumu na, japo amateuliwa na bunge la Kongresi, hategemei imani ya bunge hilo kwake. Hata hivyo ni mfumo bunge kwa sababu rais huchaguliwa na bunge kwa misingi ya kushiriki katika siasa za awali, hivyo basi kuhakikisha uungwaji mkono pakubwa na kuingiliana vizuri na mamlaka ya ubunge. Nguzo kuu ya mfumo huo ni hali ya kawaida katika tawala za mfumo bunge: siasa za miungano.

Kama vyama vingine kokote kule, vyama vya Bolivia hung’ang’ana kuongeza migao yake ya kura, lakini havitarajii upigaji kura kama hatua ya mwisho ya utatuzi. Badala yake, huegemea kwenye miafaka ya baada ya uchaguzi, na ni hili litakaloongoza katika kutambua anayeishia kuwa katika bunge la Kongresi na mamlaka ya juu. Ruwaza inayojulikana imekuwa ile ya miungano ya kongresi na serikali, hali ambayo imeimarisha udhabiti wa mamlaka kuu na kuingiliana vizuri kwa mamlaka za tawi tendaji la serikali na bunge. 

Kwa kuwa muhtasari wa kura “huru na za haki” katika mwaka wa 1979, mfumo wa vyama vya Bolivia, ambao ulibadilika kutoka kwenye mfumo uliosambaratika hadi kwenye ule mfumo wa vyama vingi kwa vyama sita vikuu, umedhihirika kushindwa kutoa chama maarufu, au hata uungwaji mkono unaobadilika. Hivyo, Kifungu cha 90 cha Katiba, kanuni kuu ya kuongoza mfumo wa uchaguzi, kimeeleza mbinu ya kawaida ya kuchagua rais. Haitoi nafasi yoyote ya miungano ya kisiasa, lakini ni hitaji lake kuwa marais wachaguliwe na Kongresi pale ambapo mgombea mmoja anapata kura nyingi ambazo zinapanua mtazamo wa kutetea na kujenga miungano miongoni mwa vyama vya kisiasa. 

Sehemu moja kuu ya Bolivia “mfumo bunge na mfumo rais” ni mfumo wa uchaguzi wa Orodha ya PR. Hasa, katika miaka yote ya 1980 na mapema miaka ya 1990 mfumo wa uchaguzi ulisaidia kusisitiza mipangilio ya ushindani na ujenzi wa miungano ndani ya vyama, japo mfumo pia ulikuwa na udhaifu mwingi na ulielekea kuharibiwa. Moja katika masuala makuu ya udhabiti wa demokrasia na uhalali limekuwa ujenzi wa sheria unganifu kwenye mchezo huo. Mabadiliko ya uchaguzi nchini Bolivia katika miaka ya 1986, 1991, na 1994 yalionyeshwa na hesabu za muda mfupi na hatua za dharura kutokana na shinikizo la kisiasa, bali sio kwa uchunguzi au ujenzi wa kisiasa. Isitoshe, viongozi wa vyama walikosa tajriba na walishindwa kujenga mikakati ya mabadiliko unganifu. Matokeo yalikuwa kwamba uchaguzi wa miaka ya 1985, 1989, na 1993 zilifanywa chini ya fomula tofauti tofauti za PR. Fomula ya D'Hondt iliyoanzishwa mwaka wa 1956, ilibadilishwa na ile ya mwaka wa 1986 ya pende mbili za ushiriki na ugawaji viti, ambayo ilitatiza vyama vidogo kufika kwenye Kongresi. Katika mwaka wa 1989 badiliko jingine lilijenga fomula ya Sainte-Lagu kwa manufaa ya chaguzi za urais na ubunge za mwaka wa 1993, ambayo ilihimiza uwakilishwaji wa vyama vidogo kabisa.    

Hata hivyo, wimbi la kwanza la mabadiliko muhimu lilichangia kidogo sana katika mabadiliko ya mfumo uliokuwepo wa PR kinyume na hali iliyopaswa kuwa Mahakama maalumu ya Uchaguzi, kuchukuliwa kwa uthibitishaji wa moja kwa moja wa kura kwenye vituo vya upigaji kura, na kutupilia mbali kwa mikakati iliyoziwezesha mahakama za uchaguzi za maeneo kuharibu kuharibu matokeo. Hata hivyo, mabadiliko ya katiba ya Agosti mwaka wa 1994 yalitanguliza wimbi la pili la mabadiliko, na kusababisha mabadiliko makubwa katika mfumo wa PR pakubwa kwa kuanzisha, na mabadiliko fulani, mfumo wa uchaguzi wa MMP wa Ujerumani na Nyuzilandi. Mwanzoni, marekebisho haya yaliishia katika kuchukuliwa kwa mfumo sambamba wa FPTP na mifumo ya PR – kimsingi, mfumo mseto wa PR katika masuala ya upigaji kura japo si katika masuala ya matokeo.     

Kwa hivyo katika mwezi wa Agosti mwaka wa 1996, bunge la Kongresi lililazimika kupitisha sheria mpya kuhusu utekelezaji wa Kifungu 60 cha Katiba kuondoa makosa fulani. Ilibuni upya fomula ya D'Hondt ya PR na kujenga nafasi ya viwango vitatu vya viti Bunge la Manaibu. Hivyo basi, manaibu 68 dhidi ya idadi inayokubalika kikatiba ya watu 130 watachaguliwa na mfumo wa upigaji kura wa FPTP katika maeneo ya mpigakura mmoja, huku walioasalia watachaguliwa kwa upigaji kura wa njia ya orodha ya vyama kulingana na usawa katika uwakilishwaji, katika maeneo tisa ya wapigakura wengi. Tofauti na ilivyokuwa nchini Ujerumani na Venezuela, hakuna kipengele cha kutetea uwepo wa viti zaidi. Viti hupeanwa moja kwa moja kwa wagombea wanaoshinda katika wilaya za mpigakura mmoja, hata kama chama kinashinda katika eneo moja na kupata viti vya PR. Ilivyo Ujerumani, viti kwa jumla hata hivyo, vitaamliwa kwa kuitekeleza fomula ya PR katika mtindo wa kufidia, na asilimia tatu ya idadi ya uwakilishi katika kiwango cha taifa. Chama kikishinda viti 10 kupitia kwa njia ya upigaji kura kwa kutumia Orodha ya PR, na viti vitano maeneo ya upigaji kura kwa mtu mmoja, hivyo ina uwezo wa kupewa viti kumi.     

Jambo linaloshtusha kabisa katika tajriba ya Bolivia kuhusu mabadiliko ya uchaguzi limekuwa matumizi ya hatua na mbinu za kidemokrasia. Mabadiliko yalijadiliwa katika tume za vyama vingi na kufikia mwafaka wa vyama vingi lilikuwa jambo la lazima kuidhinishwa na bunge la Kongresi. Kura za maamuzi hazikuitishwa kwa kuwa Katiba ya Bolivia hairuhusu mbinu hii ya kuhalalisha. Kutoka mwaka wa 1989 hadi mwaka wa 1992, jadala wa kati ya vyama ulizungukia mapendekezo mawili makuu, ambayo yalikataliwa hatimaye. Acción Democrática Nacionalista na Movimiento de Izquierda Revolucionaria walipendekeza wingi wa kura katika uchaguzi wa rais, hivi kwamba bunge la Kongresi lingethibitisha tu mgombea aliyepata kura nyingi; hata hivyo MNR ilipendekeza mtindo wa Ufaransa wa Awamu Mbili (TRS). Mapendekezo yote mawili yalianzia kwenye msingi kuwa hali ya rais kuchaguliwa na bunge la kongresi kutokana na nafasi ya chama hayakutilia maanani ari ya watu, na maamuzi yalichukuliwa kisiri; watu walipiga kura, lakini hawakuteua rais.

Mwafaka ulifikiwa mwisho kutokana na pendekezo la MNR kutumia mfumo wa MMP kwa kura za ubunge na zaidi kupunguza idadi ya wagombea wa urais waliokuwa na uwezo wa kupata kura nyingi katika uchaguzi wa bunge kutoka watatu hadi wawili, na kuweka mamlaka ya miaka mitano kwa rais, makamu wa rais, na wabunge. Badiliko la kuingia katika mfumo wa MMP lilitokana na kuibiwa kwa kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1989, japo sababu mahususi za mabadiliko zilikuwa tatu: wahka kuhusu mchakato wa kutohalalisha uwakilishaji wa vyama kwa sababu ya orodha funge za vyama hutatiza uhusiano kati ya wabunge na wapigakura; kuchanganya fikira wa raia wasiowajibika kisiasa kwenye vyama vinavyoongoza; na mwisho haja ya kupunguza ongezeko la utengano kati ya vyama na jamii kwa kupendelea uwakilishaji wa bungeni. 

Katika chaguzi za ubunge na urais za Juni mwaka wa 1967, mabadiliko haya ya uchaguzi hayakuwa na athari iliyotarajiwa, kwa kuwa mfumo wa vyama ulisambaratika na kukingamiza kuliko uliochaguliwa katika mwaka wa 1993. Kwa mfano, katika mwaka wa 1993 chama kikubwa kabisa kilishinda asilimia 35.6 ya kura; katika mwaka wa 1997, chama kikubwa – tofauti- kilishinda asilimia 22.3. Ni vyama saba pekee vilivyoshinda viti katika mwaka wa 1997, ikilinganishwa na tisa katika mwaka wa 1993, japo wafuasi walitoshana katika idadi, hivyo kusababisha bunge lililotawanyika la kongresi. Kulikuwa na sababu tatu kwa matokeo haya yasiyoktarajiwa.  Kwanza, Vuguvugu la Kitaifa la Mabadiliko (MNR) la rais aliyekuwa mamlakani wakati huo Gonzalo Sanchez de Lozada lilipoteza takribani nusu ya idadi yake ya kura, hivyo kuukatizia nafasi ya kujulikana kwake pakubwa kutokana dhidi ya wapinzani wake. Pili, katika mwaka wa 1993 wapinzani wakuu wa MNR, AND na MIR, waliunganishwa katika muungano ulioitwa Patriotic Accord; kabla ya mwaka wa 1997 muungano huu ulivunjika na ADN na MIR kuweka wagombea tofauti wa urais na kuwasilisha orodha tofauti za kongresi. Inashawishi kueleza kuwa kungekuwa na vyama vichache haya yasingetendeka; hata hivyo, mfumo wa uchaguzi wa MMP ulionekana kuharibu zaidi kusambaratika huko. Kutokana na hali ya vyama kuwa na ufuasi mkubwa katika sehemu mbalimbali maalumu, vyama zaidi (saba) vilishinda viti katika maeneo ya mpigakura mmoja kuliko maeneo ya wapigakura wengi (vyama vitano). Kwa jumla, vyama vipya vilikuwa na ubinfasi kushinda awali, japo ni vigumu kuhusisha matokeo haya na mfumo mseto wa uchaguzi, kwa kuwa idadi kubwa ya viongozi binafsi walichaguliwa kwa mfumo wa PR.