Katika mwaka wa 2002, Wabrazili waliingia katika uchaguzi kuchagua rais mpya, wabunge wa mabunge yote mawili ya kitaifa, magavana wa sehemu husika za muungano (majimbo 26 pamoja na Wilaya ya Jimbo ya Brazili), na wabunge wa bunge moja la kisheria la jimbo. Huu ndio uliokuwa uchaguzi wa nne wa moja kwa moja tangu kukamilika kwa utawala wa kijeshi katika mwaka wa 1985 hadi kwenye ule wa rais na nyadhifa nyingine kuu na za ubunge.
Chaguzi za urais nchini Brazili hufanyika chini ya mfumo wa awamu mbili ya kura nyingi, na wagombea wanaowania kupigiwa kura katika eneo zima la kilomita mraba 8,511,965 za Nchi. Kufuatia marekebisho ya katiba yaliyoidhinishwa Juni mwaka wa 1997, marais sasa hivi wanaruhusiwa kuwania kuchaguliwa tena mara moja. Fernando Henrique Cardoso, aliyekuwa mamlakani wakati marekebisho hayo yalipofanywa, alishinda kura muhula wa pili katika mwaka wa 1998 katika awamu ya kwanza na asilimia 53.1 ya kura. Hata hivyo, Luiz Inácio Lula da Silva alipata asilimia 46 katika awamu ya kwanza mwaka wa 2002 na alichaguliwa katika awamu ya pili.
Kanuni zinazoongoza chaguzi za ubunge hazijabadilishwa tangu zilipobuniwa katika mwaka wa 1946. Bunge la Seneti ambako maeneo ya Brazili huwakilishwa: kila mojawapo ya sehemu hizo 27 za muungani huwakilishwa na maseneta watatu wanaochaguliwa na wengi kwa awamu ya miaka minane. Uwakilishi huo husasaishwa kila baada ya miaka minne na thuluthi na thuluthi mbili, wakibadilishana: ikiwa maseneta wawili wanapaswa kuchaguliwa, wapigakura wana kura mbili chini mfumo wa Kura za Bloku (BV).
Bunge la Manaibu lina wabunge 513 wanaoshindana katika maeneo 27 ya uchaguzi wa wapigakura wengi, wanaolingana na majimbo 26 na Brasilia. Uzito wao hutambuliwa na idadi ya watu, ikiongozwa na udhibiti kwamba hakuna jimbo linaloweza kuwa na chini ya wawakilishi wanane au zaidi ya wawakilishi 70. Chaguzi hufanyika chini ya mfumo wa orodha wazi ya PR. Kila mpigakura ana kura moja ya kupiga, inayoweza kupeanwa kwa chama au kwa mtu binafsi. Kura zinazopigiwa wagombea kutoka kwa kila chama huwekwa pamoja na kuongezwa kwenye kura zilizoshindwa na chama hicho ili kupata idadi ya jumla ya kura, ambayo hutumika kutambua idadi ya viti vya kupewa kila chama. Wagombea waliopigiwa kura nyingi kwenye kila orodha ya vyama hupewa viti vilivyotengewa chama hicho. Upeanaji viti umefanywa chini ya Fomula ya D’Hondt tangu mwaka wa 1950. Vyama vinavyokosa kupata idadi ya kutosha ya kura katika wilaya moja, hata hivyo, hutengwa dhidi ya kupata kiti chochote. Kufikia mwaka wa 1998 hesabu ya maeneo ilitegemea idadi kamili ya kura halali na zisizojazwa, hivyo basi kuinua kizingiti cha uwakilishi.
Kukosekana kwa Usawa katika Ugawanyaji
Kanuni za uchaguzi wa Bunge la Manaibu pengine ndizo kipengele tatizi kabisa katika mfumo wa uchaguzi wa Brazili. Uwazi kuhusu upana wa maeneo ya uchaguzi unaashiria kwamba uwakilishwaji katika Bunge kwa misingi ya idadi ya watu hailingani katika majimbo yote. Hili linahujumu pakubwa kanuni ya ‘mtu mmoja, kura moja, thamani moja’ (OPOVOV), kwa kuwa idadi ya watu inayohitajika kuchagua mjumbe mmoja katika mji wa São Paulo, ulio na zaidi ya wapigakura milioni 25 na viti 70, ni mara kumi zaidi ya ilivyo katika mjili wa Amapá, ulio na wapigakura 290,000 na viti vinane. Hali inayopatikana ya kukosa usawa katika ugawanyaji hunufaisha majimbo yasiyojulikana, ambayo mara nyingi huonekana kuwa maskini na yanayotegemea sana kilimo, na hutatiza nafasi ya majimbo makubwa, ambayo ni tajiri na yenye viwanda vingi. Kwa sababu hii imelaumiwa kama mikakati mikuu ya kudumisha utamaduni katika siasa na hivyo basi kulegeza vyama vya kisiasa.
Hata hivyo, hili linahitaji kutetewa. Anayepoteza katika hali hii ya kukosekana kwa usawa katika ugawanyaji ni jimbo la São Paulo, ambako idadi ya wajumbe inaweza kuongezeka kwa 40 zaidi ikiwa kiasi cha maeneo ya uchaguzi kingetokana na idadi ya watu. Majimbo mengine hayajawakilishwa vilivyo, hasara ya pili kubwa ikipatikana katika Minas Gerais (takribani wajumbe wanne). Hasara kutokana na kukosekana kwa usawa katika ugawanaji hivyo basi hukitwa katika sehemu moja. Aidha, huashiria malengo ya waandishi wa katiba ya mwaka 1946, ambao walijihusisha na kupata fomula ambayo ingewezesha São Paulo (na kwa kiwango cha chini Minas Gerais) dhidi ya kutawala majimbo kama ilivyokuwa katika kipindi kilichojulikana kama Jamhuri ya Kwanza (1899-1930).
Kufikia kwenye kiwango kwamba kukosekana kwa usawa katika ugawanaji hupendelea majimbo maskini kisiasa, inaweza kusaidia kukuza ugawanaji wa raslimali ambazo hazina thamani kubwa katika Nchi kutokana na viwango hivyo vikubwa vya kukosekana kwa usawa kama ilivyo nchini Brazili.
Isitoshe, imani ya mara kwa mara kwamba majimbo yaliyowakilishwa na watu wengi yanaweza kwa njia fulani kuzuia utungaji wa sheria za kitaifa, hudhihirika. Huenda hiyo ikawa siyo hali kwamba mwelekeo wa siasa inayodhihirisha majimbo yaliyo na uwakilisho mkubwa ni tofauti na yale yenye uwakilishwaji mdogo. Mienendo ya kiufuasi ipo katika majimbo yote, na chaguzi ni tukio linaloleta kiwango cha juu cha ushindani. Ikiwa ufuasi wa uteja ndio unaodhihirisha siasa za Brazili, kukosekana kwa usawa katika ugawanaji wa Bunge la Manaibu huenda ukakosa kuwa chanzo kamili.
Ushindani Kati ya Vyama – na Katika Vyama
Moja katika sifa za mfumo wa orodha wazi ya PR kwa Bunge la Manaibu ni kwamba huruhusu ushindani ndani ya chama na baina ya vyama. Chaguzi hizi huwa na ushindani mkubwa. Kwa mfano, katika mwaka wa 2002 jumla ya wagombea 4,901 waligombea viti 513 Bungeni. Ni katika maeneo tisa tu dhidi ya maeneo 27 ya uchaguzi kulikokuwa wagombea chini ya 100; idadi ya chini kabisa ikiwa 66 kwa viti vinane vya Tocantins. Kulikuwa na wagombea 793 kwa viti 70 kutoka São Paulo, 602 kwa viti 46 kutoka Rio, na 554 kwa viti 53 kutoka Minas Gerais. Vyama hushindana baina yavyo. Wagombea, waliotaka kuchaguliwa kwa viti ambavyo vyama vyao hupata, hushindana wenyewe kwenye viti hivyo ambavyo vyama vyao vinapata. Hili husemekana kusababisha ubinafsi, ambao huchukuliwa kama mwanzo wa udhaifu katika siasa za vyama nchini Brazili, hadi kwa uhusiano wa kiuteja kati ya wapigakura na wawakilishi wao, na bunge la kitaifa ambalo linahusika na masuala ya kieneo badala ya yale ya kitaifa.
Aidha, mtazamo huo unapaswa kuthibitishwa. Kwanza, mtazamo kwamba ni ubinafsi unaoongoza maamuzi ya wapigakura katika chaguzi za ubunge nchini Brazili haujajengeka. Ingawa idadi ya kura za mapendeleo (pale ambapo mpigakura anateua mgombea maalumu, si chama) ni pana zaidi ya idadi ya kura za vyama, tarakimu hizi huonyesha nafasi ndogo sana kuhusu jinsi wapigakura wanavyofanya uamuzi. Ikiwa wapigakura wanapendelea mtu binafsi kuliko chama, wapigakura wengi wanaopigia mgombea fulani pia watapendelea kupigia kura mgombea hata kama wanaweza kubadilisha vyama. Japo hakuna uchunguzi wowote uliojaribu kueleza suala hili moja kwa moja, ushahidi uliotawanyika unaonyesha kwamba wajumbe wanaobadilisha vyama katikati ya kipindi cha bunge wana nafasi ndogo ya kuchaguliwa, jambo linaloonyesha kuwa hawawezi kubeba kura walizopata hata wakaingia bungeni mwanzoni.
Wapigakura na Wawakilishi wao
Ni machache tu yanayojulikana kuhusu kutoshana kati ya wapigakura na wawakilishi wake. Juhudi kubwa zimetumiwa kujaribu kuonyesha taswira ya mapendeleo ya mfumo uteja na na mfumo wa kieneo ambayo lazima ilikuwa msingi wa kampeni bora za uchaguzi na safari ya kutunga sheria. Wagombea wanaofaulu, ilisema, ni wale wanaoleta zawadi kwenye maeneo bunge yao. Nchini Brazili, mfumo wa maeneo ya wapigakura wengi, ingawa, mfumo wa mtu binafsi ni mmoja katika angalau wanane wanaowakilisha eneo hilo, hivi kufanya iwe vigumu kujenga uhusiano kati ya mtu huyo na muradi mpya wa matumizi. Ijapokuwa wagombea wengine wanaweza kujaribu kukata maeneo bunge yanayofahamika kwa manufaa yao wenyewe, hii siyo njia ya pekee, na huenda isiwe mwafaka, kwa kuingia katika Bunge la Manaibu. Uchunguzi mmoja kuhusu maeneo ya kijiografia kuhusu kura za wagombea waliofaulu unaonyesha kuwa katika miaka ya 1994 na 1998 ni takribani asilimia 17 pekee ya wajumbe waliotumia mbinu hii, yaani, waliweza kupata idadi kubwa ya kura katika makundi ya maeneo fulani ya kijiografia. Wengine walitumia mbinu tofauti, kama vile kugawana na wapinzani eneo fulani maalumu, kuwaamrisha raia waliokuwa wametaengana, au kupata idadi ndogo ya jumla ya kura zao katika maeneo yasiyo na watu wengi. Kutokana na kiwango cha ushindani katika chaguzi na kukosekana kwa maeneo bunge yaliyokingwa vilivyo kisheria, haiwezekani kwamba mwakilishi atahisi kuwa salama kuhusu ‘mdhamini’ wake. Kwa hakika, viwango vya kuchaguliwa tena haviko juu: makadirio huviweka kwenye takribani asilimia 60 ya wale wanaotafuta nafasi za kuchaguliwa upya. Hivyo basi, mfumo uteja haudhihirishi, japo si kwa jumla, mahusiano kati ya wawakilishi na wapigakura.
Je, Mfumo wa uchaguzi huchangia kusambaratika kwa vyama?
Kungali na mengi tunayopaswa kujua kuhusu njia ambamo mfumo wa orodha wazi ya PR iliyo na maeneo pana ya upigaji kura, kama inavyofanya kazi ile iliyoko Brazili. Tunajua hata hivyo kuwa, chaguzi zina ushindani mkubwa, na kwamba nafasi ya juu aliyo nayo mgombea anayetetea kiti chake iko chini, na kwamba mahusiano ya manaibu na maeneo ya kuchaguliwa kwao hutofautiana, hivi kwamba hakuna mbinu bora inayoweza kumsaidia mgombea kufaulu.
Hatua ambamo mfumo fulani hufaulu hushirikisha usomi na ubinafsi katika Bunge la Manaibu ni ya kuchunguzwa. Japo ni zaidi ya maelezo haya kujadili mbinu ambayo rais na viongozi wa vyama wanaweza kutumia kulengeta mienendo ya manaibu wa vyama, manaibu hao wana shinikizo jingine pamoja na mahitaji maeneo bunge yaliyopo nay ale maalumu. Shinikizo hizi ni changamaoto kwa udhabiti wa chama kwa zinaweza kuchangia katika kusambaratika.
Kusambaratika kwa vyama katika bunge la nchini Brazili kumelaumiwa kwa kuchangia maovu mbalimbali ambayo Nchi kilipitia kutoka miaka 15 iliyopita. Kiwango cha juu cha kusambaratika huko kwa mfumo wa vyama huhusishwa mara na maswala mbalimbali, amabayo ni pamoja na mfumo wa uchaguzi na mwelekeo wake wa kupendelea sehemu binafsi, sifa za mifumo ya urais, na miungano dhabiti iliyoidhinishwa na katiba katika mwaka wa 1988.
Kiwango cha kusambaratika katika Bunge la Manaibu kimebaki vilevile, katika vyama vinane tangu uchaguzi wa mwaka wa 1990. Vipengele vingine vya sheria ya uchaguzi huelekea kupendelea vyama vikubwa na kuzuia kusambaratika huko. Mifano ni pamoja na kuongeza kura zisizo na maandishi kwenye msingi ambapo kundi la uchaguzi hutambuliwa (inayofanya kundi hilo kuwa kubwa na hivyo basi ngumu kuafikia), na kuhusisha vyama vyote ambavyo havipati nafasi katika kutokana na kushinda kiti kilichosalia.
Maingiliano kati ya mifumo ya urais na ya vyama hayajaeleweka vizuri. Hili linaacha mfumo wa majimbo kama sababu ya kusambaratika kwa mfumo wa vyama. Vyama vingine vya kitaifa nchini Brazili ni miungano tu ya vyama vya kieneo. Vyama vidogo huibuka kutokana na miungano hii kwa sababu za maeneo hayo, hivyo basi kujaa kwa vyama katika kiwango cha taifa. Kama hii ndiyo sababu hasa au ya pekee ya kuzuka kwa vyama vipya, haijaeleweka wazi kama mfumo wa majimbo husababisha kusamabaratika huko au pengine ni marejelo ya nia za kimaeneo ambazo Nchi na Brazili kwa jumla zinapaswa kukubali ili kujiendesha kidemokrasia.