Wakati mataifa matatu yaliyotawaliwa na Uingereza Kaskazini ya Marekani yalipoungana katika mwaka 1867 – mwaka uo huo Uingereza iliongeza idadi ya wapigakura hadi kwa asilimia 10 – muungano mpya wa Kanada kiasilia ulikubali asasi za Uingereza kwa demokrasia katika uchaguzi. Waasisi wa taifa la Kanada, kinyume na wenzao wa Australia hadi kwa vizazi vya baadaye, walishindwa kuuliza ikiwa mfumo wa Uingereza wa FPTP ulifaa kwa muungano wa Nchi kwa maeneo mapana. Ingawa majaribio mengine ya kieneo na mikoa na mifumo tofauti tofauti ya uchaguzi yalifanyika baada ya Magharibi iliingia katika muungano mapema karne hii, na haikudumu kwa muda mrefu. Leo, sio tu Wabunge 308 waliochaguliwa kupitia mfumo wa FPTP, lakini ndivyo wabunge wa maeneo kumi ya ubunge na maeneo matatu. Kwa hakika, kwa miaka mingi, mfumo wa uchaguzi wa muungano ulikaribia ule muundo wa wengi wa FPTP jinsi maeneo machache ya Uwakilishi uwili uliokuwepo umeondoka taratibu.
Kwamba mfumo wa FPTP unafaa kwa nchi ya Kanada umechukuliwa kimzaha kwa sababu ufahamu wa Kanada na tajriba ya uchaguzi nje ya mipaka yake kwa jumla inafikia Marekani na Uingereza. Hadi sasa, hili halielezi wazi jinsi Nchi inayohusika pakubwa na marekebisho ya katiba, haujajitokeza wazi kwa kubadilisha asasi za uchaguzi –hasa, kama tutakavyoona, kutokana na mabaya yaliyojitokeza. Hili halimaanishi kwamba marekebisho kwenye mfumo wa usawa hayajapendekezwa; ila tu kwamba haijalifanya hilo kuwa ajenda ya kisiasa. Jopo kuhusu Umoja wa Kanada (Tume ya Pepin-Robarts) katika Ripoti yake ya mwaka 1979 lilijumuisha mapendekezo ya zaidi ya asilimia 20 ya viti katika Bunge la Uwakilishi kupeanwa kwenye vyama kwa usawa kwa kuzingatia ufuasi wake na kutoka kwenye maeneo hayo yaliyokuwa na uwakilishwaji mdogo. Pendekezo tofauti kidogo lilitolewa na walioegemea mrengo wa Chama cha Demokrasia Mpya, chama ambacho hakikuwa na uwakishwaji mzuri chini ya mfumo wa FPTP. Hadi sasa, pale ambapo serikali ya Trudeau ilipinga ripoti ya Pepin-Robarts, marekebisho ya uchaguzi katika Bunge la Uwakilishi pia yalipunguzwa.
Ukweli kwamba suala hilo halikuwa na ajenda ya siasa ulikuwa wazi miaka kumi baadaye pale ambapo Pierre Lortie, Mwenyekiti wa Tume ya Royal kuhusu Marekebisho ya Uchaguzi na Ufadhili wa Vyama iliyobuniwa na serikali ya Mulroney katika mwaka wa 1990, liliweka wazi kuwa kubadilisha mfumo wa uchaguzi kama uliokuwa nje ya mamlaka ya Tume. Mjadala kuhusu marekebisho ya uchaguzi kwenye asasi za bunge la muungano uliegemea kwenye pendekezo lililotolewa na mikoa ya Magharibi kugeuza bunge lililokuwa limeteuliwa na bunge la juu, Seneti, hadi kwa yule aliyechaguliwa. Lakini mabadiliko ya Seneti yalikufa kutokana na kukataliwa kwa pendekezo la marekebisho ya Katiba katika kura ya maamuzi ya mwaka 1992, njia hii nzuri yqa kuingia katika mifumo ya uchaguzi badala ya FPTP ilifungwa.
Katika kinaya, athari za kutatiza za mfumo wa FPTP kwenye uwakilishi katika Bunge la Uwakilishi – pamoja na mielekeo ya raia wa Kanada kujitambulisha na maeneo fulani – pengine havijakuwa vikubwa kushinda chaguzi mbili za muungano zilizofanyika katika miaka ya 1990. Katika mwaka wa 1993, wapigakura walikataa chama kilichokuwa mamlakani cha Progressive Conservatives, japo mfumo wa uchaguzi ulikaribia kuangamiza mfumo kale wa vyama nchini Kanada. Badala ya kuchagua wajumbe 46 katika wale 295 ambao mfumo sawazishi ungevipa, Tories alimudu kuchagua wawili pekee. Kinyume cha haya, vyama viwili vya kimaeneo, the Bloc Québécois na Reform, huku asilimia 13.5 na 19 ya kura mtawalio, vilichagua wabunge 54 na 52.
Katika mwaka wa 1997, kwenye viti 301 vya Bunge, Liberals walishinda viti 155, Reform 60, Bloc Québécois 44, NDP 21 na Tories 20. Viti hivi vingegawika kulingana na ufuasi vya vyama, Wahafidhina (Conservatives) wangekuwa wa tatu na viti 58, nyuma Reform na 59, huku NDP na Bloc Québecois vikiwa chini kwa viti 33 kila kimoja, hivyo kuacha Liberals na viti 118. Thuluthi mbili ya viti vya Liberals vilitoka Ontario, huku Reform ikipata uungwaji mkubwa kutoka mikoa ya Magharibi, na Bloc Québécois Québec – “robo ya Kanada”-kama Mwanauchumi alivyoeleza, hivyo kutoa kile ambacho mabingwa wa Kanada walikiita “Bunge la Upinde.” Kiti hicho kingepeanwa kulingana na ufuasi mkubwa wa vyama, Liberals, Conservatives, na NDP vingepata viti katika mikoa au maeneo yote; Wanamapinduzi katika yote ila Québec. Hili bila shaka, linawacha nje ukweli kwamba chini ya mfumo wa PR vyama hivyo vingekuwa na hatua ya kutumia nguvu na raslimali zao kwa umbali wa zaidi ya maeneo ambako walipata matokeo mazuri: Wahafidhina wangejikaza kabisa katika maeneo ya Magharibi; NDP na Wanamapinduzi wangejitahidi sana kuungwa mkono katika eneo la Québec. Kwa hakika, kuna sababu nzuri ya kuchukulia kwamba idadi hiyo ndogo iliyojitokeza ya thuluthi mbili ya wapigakura waliosajiliwa inahusishwa na ukweli kwamba katika vinyang’anyiro vingi ni chama kimoja au viwili tu vilivyokuwa na ushindani wa kweli, huku wafuasi wa vile vingine wakiwa wamesambaratishwa kabisa.
Mageuzi katika uchaguzi ya kuingia katika mfumo wenye usawa yalipendekezwa na waandishi na wahariri kadhaa katika chaguzi mbili, na kukuzwa na viongozi wa Chama cha Maendeleo ya Uhafidhina (PCP), japo katika hali ya kusononesha. Katika mwezi wa Novemba mwaka wa 1997, muswada wa mgombea binafsi uliwasilishwa na mbunge maarufu wa NDP akipendekeza Bunge liidhinishe mfumo wa PR na kuteua kamati ya vyama vyote kujadiliana na umma kuhusu suala hilo na kuleta habari kamilifu kuhusu pendekezo hilo ambalo hatimaye lingewekwa wazi kwa raia wa Kanada kulifanyia uamuzi katika kura ya kitaifa ya maamuzi. Hadi sasa, kama ilivyo kwa miswada mingine iliyoletwa na wabunge binafsi, hili litakatizwa kwenye orodha ya miswada. Kwa upana, wanasiasa huchukulia mabadiliko ya uchaguzi hatua ya mwanzo ambayo hawana haja ya kuingiza nguvu zao nyingi za kisiasa.
Japo hili linaeleweka linasikitisha. Kwa kuwa mfumo wa FPTP umechangia katika kuibuka kwa serikali nyingi, mwenendo wa mfumo huu wa kukandamiza badala ya kukuza haujaihudumia nchi ya Kanada vizuri. Kama zoezi lililotumiwa kwa jaribio, mtu anaweza kukisia tu matokeo ikiwa juhudi kubwa ya hivi karibuni kuleta mabadiliko katika uchaguzi hadi kwenye ajenda ya siasa za mikoa ilifaulu. Hii ilifanyika huko Québec katika miaka ya 1980 ambapo tume za uchunguzi zilipendekeza kuchukuliwa kwa mfumo wa orodha ya kieneo ya PR, pendekezo lililoidhinishwa na baraza la mawaziri la Québec lakini ambalo kutokana na kukosa kuungwa mkono na upinzani, na hata katika jopo kuu la chama kilichokuwa mamlakani – halikuwasilishwa bungeni. Lingeidhinishwa, ugawanaji wa mamlaka hivi leo ungekuwa mikononi mwa vyama vinavyowakilisha asilimia 25 ya wakazi wa Québec wanaotaka mabadiliko japo wanapendelea mwafaka usio huru na unaoungwa mkono na Parti Québécois.
Mabadiliko ya kipekee ya uchaguzi yaliyofanikiwa kuingia katika ajenda ya kisiasa yalikuwa sheria zilizochukuliwa katika mikoa mingine ya Magharibi kuruhusu kubanduliwa mamlakani kwa wabunge. Kulingana na mabadiliko ya uchaguzi, hatua ya pekee inaweza kuwa Kanada kufuata mfano wa Uingereza. Ikiwa Uingereza inadhihirika kujiandaa kwa kubadilisha mfumo wa uchaguzi iliyoupokeza Kanada, raia wa Kanada wanaweza kuiga.