ACE
Encyclopaedia   Mada   Mifumo ya Uchaguzi   Uchunguzi wa Mifumo ya Uchaguzi  
Demokrasia ya Moja kwa Moja ya Uswizi

Mtazamo wa kina kuhusu mifumo mingi ya demokrasia za moja kwa moja inayotumiwa nchini Uswizi

Demokrasia ya moja kwa moja ilianzishwa katika kiwango cha jimbo nchini Uswizi katika mwaka 1848, ingawa katika majimbo mengine ya Uswizi mifumo ya demokrasia ya moja kwa moja imekuwa ikitumika kuanzia karne ya kumi na nne. Mifumo mbalimbali ya demokrasia ya moja kwa moja huwasilishwa katika viwango jimbo na muungano, huku wapigakura wa Uswizi wakipewa nafasi ya kupiga kura katika kura za muungano mara nne kwa mwaka.

 Kuhusiana na demokrasia ya moja kwa moja, Uswizi hutazamwa kama nchi iliyo karibu sana na serikali inayotumia mfumo wa demokrasia ya moja kwa moja. Ijapokuwa Uswizi hudumisha sifa za demokrasia ya uwakilishi (k.m. ina Bunge lililochaguliwa), mifumo mbalimbali ya demokrasia ya moja kwa moja hutumiwa mara kwa mara katika kiwango cha kitaifa, jimbo na eneo la kijumuiya. Uchunguzi huu unalenga mifumo na matumizi ya demokrasia ya moja kwa moja nchini Uswizi.

Historia na Usuli

Demokrasia ya moja kwa moja ina usuli mrefu katika baadhi ya majimbo ya Uswizi, kuanzia karne ya kumi na nne. Uswizi ilipokuwa serikali ya muungano katika mwaka wa 1848, vyombo vya demokrasia ya moja kwa moja vilianzishwa katika kiwango cha taifa vilevile. Katiba ya muungano ilianzisha kanuni ya kufanya kura za maamuzi za lazima ili kubadilisha katiba, na vilevile kama hatua ya jumla ya kurekebisha katiba yote. Haki nyingine za kufanya kura za maamuzi zilianzishwa katika mwaka wa 1848, na hatua ya jumla ya kurekebisha sehemu ya katiba katika mwaka wa 1891. Kati ya 1848 na Februari 2004, kura 517 za maamuzi zilifanyik, huku kati ya 1892 na Mei 2004, hatua za marekebisho 244 zikipendekezwa.  

Maumbo ya demokrasia ya moja kwa moja – kiwango cha majimbo

Mifumo mingi ya demokrasia ya moja kwa moja inaweza kutumiwa katika kiwango cha jimbo nchini Uswizi. Mifumo hiyo huwa katika makundi mawili: kura za maamuzi na mapendekezo – hakuna sheria kuhusu kuwabandua viongozi mamlakani nchini Uswizi. Kila mfumo unaweza kutumiwa kuafikia matokeo tofauti, na una sifa tofauti kiumbo.

Kura za Maamuzi

Tofauti na ilivyo katika nchi nyingine, nchini Uswizi si serikali inayoamua ikiwa kura ya maamuzi ifanyike kuhusiana na suala; hali ambamo kura hizo za maamuzi hutumiwa ni wazi katika katiba ya nchi.

Aina ya kwanza ya mfumo wa demokrasia ya moja kwa moja ni kura ya maamuzi ya lazima, k.v.  kura ya maamuzi ambayo serikali inapaswa kuitisha kuhisiana na masuala fulani yenye umuhimu kisiasa: 

  • Marekebisho ya sehemu ya katiba au katiba nzima ya muungano;
  • Kujiunga na shirika fulani ila kuweka uthabiti katika ulinzi wa pamoja au shirika la ngazi za juu;
  • Kuweka sheria ya dharuara ambayo ufaafu wake unachukua mwaka mmoja, bila misingi inayohitajika kikatiba (sheria kama hiyo inapaswa kuwasilishwa kwenye kura katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuidhinishwa na Bunge);
  • Hatua za jumla kuhusu marekebisho ya katika nzima;
  • Hatua za maamuzi kuhusu marekebisho ya sehemu fulani ya katiba katika umbo la pendekezo la jumla zilizokataliwa na Bunge;
  • Suala la ikiwa marekebisho ya katiba nzima yanapaswa kufanyika ikiwa vitengo vyote viwili vya Bunge vinakosa kuafikiana.

Aina za kwanza tatu za kura za maamuzi huhitaji kupitishwa na uwili idadi; yaani, zipate idadi kubwa ya wapigakura (kura nyingi zilizopigwa kwenye kura ya maoni) huku kwa wakati huo kupata kura nyingi katika mengi ya majimbo. Za mwisho tatu, ambazo hufanyika kama sehemu ya mchakato, huhitaji wingi wa kura tu.

Kura za maamuzi za hiari zinaweza kufanyika kuhusiana na sheria mpya au zilizorekebishwa na/ au miafaka ya kimataifa. Kura ya maoni ya kutunga sheria hufanywa kuhusiana na sheria zote zilizopo za muungano na sheria za dharura za muungano ambazo zinahitajika kuwa halali kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kura ya maamuzi ya hiari kuhusu miafaka ya kimataifa hufanywa kuhusiana na makubaliano ya kimataifa ambayo ni ya muda mrefu na ambazo huenda zikakosa kuvunjwa, na miafaka ya kimataifa ambayo hutoa nafasi kwa mashirika wanachama kimataifa au huwa na vipengele vya kisheria ambavyo vinapaswa kutekelezwa kwa kubuni sheria za muungano. Kura za maamuzi zisizo za lazima huitishwa ikiwa saini 50,000 zinakusanywa ili kuunga mkono kura hiyo katika siku 100, au ikiwa majimbo manane yanaomba kufanywa kwa kura hiyo ya maamuzi, na kupita kwa idadi kubwa ya kura. Kufikia mwaka 2004, kura ya maamuzi isiyo ya lazima haijawahi kufaulu kuagizwa na kundi la majimbo; na kura ya kwanza ya maamuzi iliyoanzishwa na majimbo ilifanyika tarehe 16 Mei mwaka 2004.     

Hatua

Mikakati inaweza kutumiwa kupendekeza mabadiliko kwenye katiba ya muungano. Isitoshe, katika mwaka 2003, Uswizi iliidhinisha mfumo mpya wa mikakati, uliopaswa kutumiwa kuhusiana na vipengele vingi vya kisheria. Pindi mkakati unaposajiliwa, idadi fulani ya saini halali (k.v. saini za wapigakura waliosajiliwa) huhitajika ili kushinikiza Baraza la Kusimamia Muungano na Bunge kuzingatia mkakati huo na kufanya kura ya maamuzi kuhusiana na pendekezo hilo loa mikakati.

Marekebisho ya katiba yanaweza kupendekezwa kwa kutumia mifumo mbalimbali ya mikakati. Hatua inayofahamika ya kurekebisha sehemu tu ya katiba huwapa wapigakura fursa ya kupendekeza marekebisho kwenye sehemu fulani ya katiba ya muungano. Wapigakura 100,000 wanapaswa kutia saini zao kwenye shughuli hiyo ili kura ya maamuzi iweze kufanyika kutokana na pendekezo lao. Hatua ya kurekebisha katiba nzima pia huhitaji wapigakura 100,000 kuiunga mkono. Katika visa vyote viwili, saini zinapaswa kukusanywa katika muda wa miezi 18 ya kusajiliwa kwa pendekezo hilo.

Kuanzia mwaka 2006, hatua ya ufuasi wa jumla imekuwepo kwa wapigakura wa Uswizi. Mfumo huu unaweza kutumika kushinikiza kufanyika kwa kura ya maamuzi kuhusu kuidhinishwa kwa kijumla kwa pendekezo litakalojumuishwa katika kiwango cha kikatiba/ au kisheria, hivyo kuagiza kwamba sahihi 100,000 zikusanywe kuunga mkono hatua hiyo.

Kufikia mwaka 2006, mikakati nchini Uswizi iliwasilishwa kama pendekezo la jumla au katika maelezo ambayo yangeudhinishwa ikiwa hatua za kukinga mikakati hiyo zinafaulu. Hata hivyo, baada ya kutekelezwa kwa hatua ya jumla, hatua ya kurekebisha sehemu fulani ya katiba itakubaliwa tu katika hali ya maandishi (mapendekezo ya jumla kuhusiana na katiba yanapaswa kufanywa kwa kutumia hatua ya jumla). Katika kukabiliana na hali hiyo inayoafiki masharti ya saini, Bunge la Uswizi hushauri watu kuhusu ama kukubali au kukataa pendekezo hilo. Isitoshe, serikali pia huweza kuunda pendekezo jingine la kujibiza hili la watu ambalo huwekwa kwenye kura. Suala la kura mbili huwaruhusu wapigakura kuidhinisha hatua zote mbili, ile asilia na jibu la serikali, na kuonyesha katika hatua hizo mbili ni ipi wanayopendelea. Hatua inayopata uungwaji mkono kwa wingi ndiyo hupitishwa.  

Maumbo ya demokrasia ya moja kwa moja – kiwango cha mikoa

Matumizi ya demokrasia ya moja kwa moja yameenea sana katika majimbo 26 ya Uswizi (k.v. halmashauri za serikali). Hata hivyo, matumizi ya demokrasia ya moja kwa moja hutofautiana kati ya majimbo; kati ya 1970-2003 Zurich ilifanya 457, huku Ticino ikifanya 53 pekee (Jimbo la Jura lilifanya kura za maamuzi 45, japo lilibuniwa tu rasmi na kura ya maamuzi katika mwa 1979).

Pamoja na kura ya maamuzi na mifumo ya mikakati iliyotumiwa katika kiwango cha muungano, mikakati ifuatayo hutumiwa pia katika baadhi au majimbo yote ya Uswizi.

Tofauti na kiwango cha muungano, hatua ya kisheria kwa muda fulani imewapa wapigakura katika majimbo yote fursa ya kupendekeza nyongeza kwenye sheria. Katika majimbo mengine, hatua ya usimamizi katika kuzindua jimbo inaweza kutumiwa kushurutisha kwamba kazi fulani ifanywe katika usimamizi wa umma (k.m., kujenga shule mpya au barabara mpya). Aidha, majimbo mengine hutoa fursa ya kushinikiza jimbo fulani kuweka muswada kwenye Bunge la Muungano.

Majimbo yote ya Uswizi hutoa nafasi ya kura za maamuzi za kutunga sheria kuhusu sheria iliyopitishwa na bunge la jimbo; hata hivyo, katika majimbo tofauti, haya yanaweza kuwa ya lazima au ya hiari. Kura za maamuzi kuhusu usimamizi zinaweza kufanywa kuhusu miradi mikubwa itakayochangia matumizi ya raslimali za umma (na yanaweza kusababisha ongezeko la ushuru); wakati mwingine kura hizi huitwa kura za maamuzi. Mwisho, kura za maamuzi kuhusu usimamizi zinaweza kufanyika kuhusiana na masuala yasiyo ya kifedha na yanayohusiana na umma ambayo yematajwa hapo juu. 

Sifa za matumizi ya demokrasia ya moja kwa moja nchini Uswizi

Waliojitokeza

Wapigakura wa Uswizi hupewa fursa ya kupiga kura katika kura za maamuzi za miungano mara nne hivi kwa mwaka. Kwa mfano, wapigakura pia watapiga kura kuhusiana na masuala fulani yanayohusu jimbo au maeneo yao siku ya uchaguzi wa miungano. Katika sehemu ya pili ya karne ya ishirini na moja, kujitokeza kwa wapigakura kwenye kura za miungano hutoka katika takribani 50-70% hadi 40%; hili liliashiria kupungua kwa aina hiyo katika kujitokeza kwa watu katika chaguzi za miungano kutoka 80% hadi takribani 45%. Pendekezo moja ni kwamba kupungua huku kwa idadi ya wanaojitokeza kupiga kura ni kutokana na idadi ya juu ya kura ambazo Waswizi wanaweza kupiga; hata hivyo, inasemekana kuwa idadi kubwa ya watu ni changamfu kisiasa kushinda inavyodhihirika katika idadi ya 40%, kwa kuwa si hali ya kawaida kwamba kuna 40-45% ya wapigakura wanaopiga kura kila mara. 

Maswala

Kutokana na nafasi nyingi za kutumia demokrasia ya moja kwa moja nchini Uswizi, haistaajabishi kwamba masuala mbalimbali yanayosababisha kufanyika kwa kura za maamuzi ni kubwa. Kuanzia mwaka wa 1990, kura za maamuzi zimefanywa kuhusiana na masuala mbalimbali kama vile:

  • Kupiga marufuku ujenzi wa vituo vya nyuklia;
  • Kujenga reli mpya za Alpini;
  • Katiba mpya ya Muungano;
  • Kudhibiti Uhamiaji;
  • Kufutilia mbali jeshi;
  • Kujiunga na Umoja wa Mataifa;
  • Kupunguza saa za kufanya kazi;
  • Kufungua masoko ya umeme.

Athari za demokrasia ya moja kwa moja

Bila shaka, demokrasia ya moja kwa moja imechangia katika kulainisha mfumo wa kisasa wa siasa za Uswizi. Hata hivyo ni muhimu kuuliza athari kamili ya demokrasia ya moja kwa moja kwenye masuala ya kisheria, katika nchi nyingine, ni jukumu la wawakilishi waliochaguliwa.

Kwa upande mmoja, inaweza kuelezeka kuwa athari yake imekuwa finyu: katika karne ya kwanza ya matumizi ya hatua (1891-2004), ni kanuni 14 tu zilizopitishwa nchini Uswizi. Kwa kuzingatia takwimu hii pekee zinapuuza kwa kiwango fulani, athari fiche ya demokrasia ya moja kwa moja. Ingawa mikakati mingi haikufaulu, ukweli kwamba kumekuwa na hatua, na hivyo basi kampeni, kunakuza kujulikana kwa suala hilo katika na ufahamu wa umma kulihusu suala hilo. Hili pia linaweza kuongeza shinikizo kwenye serikali kuweka mikakati ya kukabiliana na suala hilo, hata kama haihitajiki kufanya hivyo kutokana na kufaulu kwa kura ya maamuzi. Shughuli kama hiyo inaweza hivyo basi kufaulu zaidi katika kuafikia baadhi ya malengo yake, hata kama haikufaulu katika njia ya kupita. Mwelekeo huu unaeleza sababu za shughuli nyingi hubuniwa lakini ziondolewe tena; kwa sababu wakati mwingine serikali huamua kuchukua hatua kabla kufikia kiwango cha kura ya maamuzi.   

Athari nyingine ya mikakati ya demokrasia ya moja kwa moja nchini Uswizi ni kwamba serikali hulazimika kutafuta mwafaka mpana kuhusu hatua za kisheria ambazo inakusudia kuweka kuliko ilivyo hali katika mfumo wa uwakilishi. Katika mfumo wakilishi, chama cha serikali kinaweza, hata wanapokosekana wapigakura wengi, wanapaswa kujenga mwafaka kuhusiana na suala hilo ili kuhakikisha kwamba hatua hiyo inaidhinishwa. Katika mfumo wa Uswizi, uwezekano wa kufanyika kwa kura ya maamuzi isiyo ya lazima hilazimisha serikali kuhakikisha mwafaka na makundi yaliyo nje ya Bunge ili kuzuia uwezekano wa makundi kama hayo kubadilisha sheria.  

Kwa upande mwingine, athari ya demokrasia ya moja kwa moja katika mfumo wa Uswizi hudokezwa mara nyingi kama sababu ya udhaifu katika vyama vya kisiasa vya Uswizi na umuhimu mdogo unaohusishwa na chaguzi za kawaida. hivi ni kwa sababu, kutokana na umaarufu wa demokrasia ya moja kwa moja, vyama vya kisiasa ndivyo pekee vilivyo na jukumu la kudhibiti ajenda ya muungano. Isitoshe, demokrsia ya moja kwa moja mara nyingi huzua masuala muhimu yanayoweza kuleta tofauti kati ya wanachama wa vyama vya kisiasa.