Baada ya kutumia Mfumo wa Awamu Mbili (TRS) katika Himaya ya Ujerumani, na matumizi ya mfumo wa uwakilishi wenye usawa katika Jamhuri ya Weima, tazama, mfumo mpya wa uchaguzi ulibuniwa na Baraza la bunge katika mwaka wa 1949. Mfumo huo ulijengwa na Sheria ya Kimsingi ya Jamhuri ya Muungano ya Ujerumani – Katiba ya Ujerumani Magharibi. Hivyo basi ulikuwa zao la majadiliano kati ya vyama kati ya vikosi vya demokrasia Ujerumani Magharibi. Kama Sheria ya Kimsingi, awali ilichukuliwa kuwa ya muda, lakini haijabadilishwa tangu mwaka wa 1949.
Mfumo wa uchaguzi nchini Ujerumani hugawika kama mfumo sawazishi wa kibinafsi au, hujulikana nchini Nyuzilandi kama Mfumo Sawazishi wa Wanachama Mseto (MMP). Ubora wake ni njia ambamo hujumuisha kura ya mtu binafsi katika maeneo ya mwanachama mmoja na kanuni ya uwakilishi wenye usawa.
Hivi sasa, bunge la Ujerumani (Bundestag) lina viti 622, bila kujumuisha viti vingine vya ziada (tazama hapo chini). Kila mpigakura huwa na kura mbili. Kura ya kwanza ni ya mtu binafsi, ambayo hupigiwa mgombea fulani (au chama) katika maeneo bunge 299 ya mjumbe mmoja. Kura ya pili ni ya chama, ambayo hupewa orodha ya chama katika kiwango cha serikali ya muungano. Wagombea huruhusiwa kushindana katika maeneo ya mwanachama mmoja na vilevile sawa na orodha ya chama. Wagombea hupata wingi wa kura katika maeneo ya mjumbe mmoja huchaguliwa. Hata hivyo, kura ya pili huamua idadi ya wawakilishi watakaotumwa kutoka kwenye kila chama hadi kwenye Bundestag.
Kwenye kiwango cha kitaifa, kura zote za pili (Zweitstimmen) kwa vyama hujumlishwa. ni vyama vinavyopata zaidi ya asilimia tano tu ya kura katika kiwango cha taifa au, pengine, vilivyo na wanachama waliochaguliwa moja kwa moja katika maeneo bunge yenye uwakilishi wa mjumbe mmoja, huzingatiwa katika ugawaji viti wa kitaifa kwa kutumia orodha ya PR. Idadi ya wawakilishi kutoka kwenye kila chama kilichoafiki masharti ya kisheria hupigwa kulingana na fomula ya Hare. Viti hivyo basi hupeanwa katika majimbo 16 ya muungano (Länder).
Idadi ya viti vilivyoshindwa moja kwa moja na chama katika maeneo ya uwakilishi wa mojumbe mmoja wa jimbo fulani la muungano hutolewa kutoka idadi ya jumla ya viti vilivyopeanwa kwa orodha ya chama hicho. Viti vinavyosalia hupeanwa kwa orodha funge. Ikiwa chama kitashinda viti vingi vya Direktmandate katika jimbo fulani la muungano kushinda idadi ya viti vinavyopeanwa kwake na kura za pili, viti hivi vya ziada (Überhangmandate) huwekwa na chama hicho. Katika hali hiyo, idadi ya jumla ya viti katika Bundestag huongezeka kwa muda.
Mfumo wa Ujerumani si, unavyopaswa kuwa wakati mwingine, mfumo mseto, bali mfumo wa PR. Unatofautiana na uwakilishi wenye usawa hivi kwamba asilimia tano ya idadi inayohitajika katika kiwango cha kitaifa haijumuishi vyama vidogo vidogo kutoka kwenye uwakilishi bungeni, na kutokana na uwakilishi wenye usawa idadi kubwa ya vikosi vya kijamii na kisiasa huwakilishwa Bungeni. Isitoshe, mfumo wa uchaguzi kwa kiwango fulani, uko wazi kufanyiwa mabadiliko ya kijamii na ya kisiasa. Licha ya masharti haya, vyama vipya vya kisiasa vikiungwa mkono na sehemu fulani ya wapigakura huweza kufika Bungeni. Kando na Muungano wa Kidemokrasia wa Wakristo/ Muungano wa Kijamii wa Wakristo (CDU/CSU), Chama cha Kidemokrasia cha Kijamii (SDP) na Chama cha Demokrasia Huru (FDP), ambavyo vimekuwa katika Bundestag tangu 1949, chama kipya cha Green Party (GRÜNE) vilipata viti katika miaka ya 1983 na 1987. Baada ya kukosa kuafiki masharti katika mwaka wa 1990, wanaGreen, kwa ushirikiano na Alliance’90, waliweza kurudi Bungeni katika mwaka 1994. Baada ya kuungana kwa Ujerumani, hata vyama vidogo vya Ujerumani Mashariki vilipata viti bungeni. Katika chaguzi za wajerumani wote za mwaka 1990, Muungano wa Ujerumani Mashariki ‘90/wanaGreen na Chama cha Demokrasia ya Usoshalisti (PDS) kilipata asilimia tano iliyohitajika ya masharti, kivyake katika eneo la iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki na iliyokuwa Ujerumani Magharibi, kwa uchaguzi huo mmoja. Miaka minne baadaye, PDS kilivamia nafasi iliyokuwepo kwa kushinda vinne katika vitatu vinavyohitajika vya Direktmandate.
Kura binafsi kwa mgombea katika maeneo bunge ya mwakilishi mmoja hulenga kuhakikisha kwamba kunakuwa uhusiano wa karibu kati ya wapigakura na wawakilishi wao. Kwa kawaida hata hivyo, ubora wa maeneo haya haupaswi kupewa thamani kubwa. Nchini Ujerumani, chaguzi za maeneo ya mwakilishi mmoja huegemea kwenye mapendeleo ya chama bali sio kwenye sifa za wagombea. Matumaini ya kwanza kwamba mfumo wa MMP unahakikisha kwamba uhusiano wa karibu kati ya mpigakura na mwakilishi wake unakuwepo, licha ya juhudi za wawakilishi kujenga mbinu za kushirikiana na maeneo bunge yao. Isitoshe, kipengele hiki cha maeneo bunge katika mfumo wa PR husaidia angalau kwa kiwango fulani kuziba pengo kati ya wapigakura na wawakilishi pengo ambalo aghalabu huzidishwa na mifumo ya PR yenye orodha funge.
Aidha, mifumo yote miwili huwawezesha wapigakura kugawa kura zao vilivyo kati yao washirika waliopo wa miungano. Kwa hakika, ugawaji kura ni hai ya kawaida miongoni mwa wafuasi wa vyama vidogo. Kwa kuwa wagombea wa vyama vidogo wana nafasi ndogo ya kushinda eneo la mwakilishi mmoja, wafuasi wavyo mara nyingi humpa kura yao kwanza mgombea wa eneo bunge kutoka kwenye chama cha muungano mkubwa. Vivyo hivyo, wafuasi wa vyama vikubwa wanaweza ‘kukopa’ kura yao ya pili kwa chama kidogo katika muungano huo, ili kuhakikisha kwamba kinaafiki mahitaji ya kisheria. Hivyo basi, ugawaji kura hutumiwa kwa njia fulani na wapigakura kuunga mkono mshirika katika muungano wa chama chao au angalau kuonyesha mapendeleo ya muungano huo.
Kwa kutoa matokeo yenye viwango vya juu vya usawa, mfumo wa uchaguzi hufanya idadi ya wapigakura, ambapo chama kimoja hushinda wingi wa viti bungeni kutokana na uchache wa kura. Kwa hakika, kwa miongo mitano iliyopita nchini Ujerumani, uundaji wa kura nyingi haujafanyika. Serikali nyingi zimekuwa za miungano, na mabadiliko yoyote ya serikali yametokana na mabadiliko katika ujenzi wa muungano. Serikali za miungano nchini Ujerumani mara nyingi huwa dhabiti na huchukuliwa kama halali na wapigakura, na kwa sababu ya hatua za kushirikiana katika ujenzi wa miungano, Wajerumani wengi hupendelea serikali ya muungano badala ya serikali ya chama kimoja. Jukumu la uchunguzi hutimizwa na upinzani, ambao pia huwakilishwa vilivyo. Ni muhimu kutambua kuwa uhusiano kati ya serikali na upinzani katika siasa za Ujerumani ni muhimu na shirikishi badala ya kuwa wa mizozo. Hili hata hivyo, ni matokeo ya historia na siasa badala ya mfumo wa uchaguzi wenyewe.
Hivi leo, mfumo wa MMP haujaonyesha matatizo yoyote nchini Ujerumani. Umedumu kwa muda wa kutosha kuwa na kiwango cha juu uhalali; kanuni za kimsingi za maeneo ya mwakilishi mmoja na uwakilishi katika orodha ya PR hazijabadilishwa tangu mwa 1949. Hata hivyo, mabadiliko mengine madogo ya mfumo wa uchaguzi yamefanyika. Kubwa katika mabadiliko hayo lilikuwa kuingia katika kura mbili tofauti katika mwaka wa 1953, kabla ya hapo mpigakura alikuwa na kura moja ya kutumia kwa upeanaji wa viti katika wilaya na mfumo wa PR wa kitaifa.
Hata hivyo, majaribio mengi ya kubadilisha mfumo wa uchaguzi yamefanywa kuanzia mwaka 1949, na hasa katika miaka ya 1960, ambapo wapinzani wa mfumo wa PR walitaka kuanzishwa kwa mfumo wa FPTP. Kwa kiwango fulani hili lilikuwa kwa sababu ya ushawishi wa kisiasa kuimarisha nafasi ya vyama vikuu, na kwa upande fulani kutokana na mtazamo wa kinadharia uliopendelea mfumo wa Uingereza; lakini majaribio yote hayakufaulu. Katika siku za hivi karibuni, mfumo wa uchaguzi umekashifiwa kwa kutoa viti vingi vya ziada bila kuviridhia vyama vilivyokosa nafasi ya kutosha Bungeni.