ACE
Encyclopaedia   Mada   Mifumo ya Uchaguzi   Uchunguzi wa Mifumo ya Uchaguzi  
Ikweda: Kutafuta Uongozi wa Kidemokrasia

Kwa kufahamu udhaifu wa kikatiba na mimtindo za kanuni iliyopita ya uchaguzi, Kongresi iliindhinisha mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi katika mwezi Machi mwaka 2000 ili kuanzisha “Ujumuishaji wa kura”. Katika umbo hili lililoimarishwa, kila chama huweka pamoja kura zilizoshindwa na wagombea binafsi na jumla ya kura zilizoshindwa itatumiwa kugawa vit kulingana na fomula ya D'Hondt wa usawa katika uwakilishi. Viongozi wa chama badala yake hugawa viti vilivyopatikana kwa wagombea waliopigiwa kura nyingi katika kila chama. Nakala iliyorekebishwa ya fomula ya uchaguzi itatumiwa kwanza katika kiwango cha taifa katika chaguzi za mwaka 2002. Mwisho, uchaguzi wa wabunge wa Kitaifa pia uliondolewa kwa uchaguzi wa mwaka 2002, hivyo kuacha bunge la Kongresi likiwa na uwakilishi wa mikoa pekee.  

Licha ya majaribio ya kina nay a mara kwa mara na mfumo wake wa uchaguzi, Ikweda haijaweza kukuza muungano wa wanasiasa wawakilishi na serikali mwafaka. Baada ya muda, kumekuwa na jukumu la kudumu la serikali katika kuufanya mfumo wa uchaguzi kupunguza kugawika mfumo wa uchaguzi na kuhimiza ujenzi wa miungano ya uchaguzi ambayo hatimaye inaweza kuunga mkono mikakati inayoongozwa na serikali bungeni. Kuchukuliwa kwa mfumo wa awamu ya pili ya uchaguzi wa rais na viwango vyake vilivyoimarishwa au kupitisha viwango vya kawaida vya uwakilishi wa vyama vikubwa vya siasa kupitia fomula ya PR vilipaswa kutoa uhalali na vilevile kupata uungwaji mkono wa chama mwafaka  kwa wagombea wa urais wakati wa kuchukua ofisi. Kinyume na kauli ya “ujenzi wa wingi”, makundi tofauti tofauti ya kijamii na kikabila, na vilevile siasa bunifu zilidai kuwa mfumo wa uchaguzi ulipendelea nia za vyama kuhusu mahitaji ya serikali na kuazimia kulegeza masharti yanayoongoza uchaguzi hadi kwa ushiriki wa kisiasa na kukuza wagombea “Huru” wa kisiasa. Kwa sababu hiyo, ueneaji wa wagombea huru katika miaka ya tisini ulifanya ujenzi wa muungano katika Kongresi kutokadirika.     

Malumbano ya kikatiba kuhusu mahitaji ya kudumisha sajili ya vyama yanaeleza vizuri mzozo kati ya uongozi na uwakilishi. Sheria ya Vyama vya Kisiasa wa mwaka 1949 ilitaka kuwa vyama ambavyo havikufikisha 5% ya kura halali katika chaguzi mbili mtawalio zingepoteza nafasi yake katika sajili ya uchaguzi. Udhibiti huu ulitangazwa kukosa kuzingatia katiba katika mwaka wa 1983, kurudishwa tena katika mwaka 1994 kama 4%, kuondolewa tena katika mwaka 1996 na kurudishwa tena mwaka 1998 kama 5%. Huku watetezi wa uongozi wakitetea kwamba vyama vidogo vilichangia katika misambaratiko ya bunge na ujenzi usiokadirika wa miungano katika Kongresi, watetezi wa mfumo wa uwakilishi walitetea kwamba watu wachache katika Ikweda walistahili kuwakilishwa na vyama hivyo. Hivyo basi, vyama vidogo na hasa vya kibinafsi viliweza kudumisha kuwepo wake kwa miaka mingi.

Ikweda haijapata fomula ya kugawana mamlaka kudumisha uongozi wa kidemokrasia. Suala moja la wazi la kujadiliwa ni kukubaliwa kwa mfumo wa wanachama mseto kwa bunge. Kikanuni, hili lingeweza kuunganisha haja ya uwakilishi wa moja kwa moja wa mikoa wa watu anuwai wa Ikweda na uchaguzi wa wanasiasa wa kitaifa. Suala jingine ni kuanzishwa kwa sifa nyingine za ubunge kama vile kugawana baraza la mawaziri kungefanya vyama katika muungano kuwajibika zaidi kwa wapigakura wake na serikali. Katika hali hiyo, mfumo wa bora wa uchaguzi ungehitaji kuimarika kwa muda (bila kuhusishwa na mabadiliko ya dharura) na yangezingatia asasi nyingine za kisiasa na mazoea ya nchi.