Mfumo wa uchaguzi nchini Uhispania una historia ndefu. Ulianza mapema katika karne ya 19, katika hali isiyo ya kawaida kutokana na nchi hiyo kuvamiwa na jeshi la Napoleon. Pengo la utawala lililoachwa lilifungua njia ya kubuni bunge la kitaifa (las Cortes) na Baraza Kuu (Junta)- viongozi wa upinzani – katika bandari ya Cadiz katika mji wa Andulasia. Manaibu, waliotoka katika maeneo yote ya Uhispania Moja na ughaibuni, walichaguliwa na wingi wa kura (kulingana na “Maagizo ya uchaguzi wa manaibu” ya 1810, yaliyoambatishwa kwenye arifa ya mikutano na ilikuwa chanzo cha kuchipuka kwa sheria ya uchaguzi). Bunge hili, katika mkutano wake wa kwanza, liljitangaza kuwa huru na jumlishi na hivyo likawa bunge la kwanza la kisasa katika historia ya Uhispania. Liliisha kwa kubuniwa kwa Katiba katika mwaka 1812. Matini ya Katiba yalitokana na fikira za mabadiliko (kauli ‘mabadiliko ya usawa’, likitumiwa katika siasa, usuli wake kitaifa ni jina lilipeanwa kwenye kundi la manaibu katika Bunge la Cadiz) na Wahispania limekuwa ishara ya uhuru wa kisiasa. Uandishi wa Katiba ya kwanza katika Kihispania, iliyojumuisha mawazo mengi kutoka kwa mapinduzi ya Ufaransa na mifumo fulani ya Katiba ya Marekani, pia ilitokana na mazoea ya demokrasia kongwe ya manispaa za Uhispania. Katika matini ya Katiba ya mwaka 1812, manispaa zilirudisha hadhi zao za awali za asasi za kuchaguliwa (manispaa katika historia na historia ya kisiasa ya Uhispania zimekuwa na wajibu muhimu katika kulinda uhuru).
Bunge la Cadiz limechukuliwa kama msingi wa mawazo wa kidemokrasia na haki ya kupiga kura, sio tu katika Uhispania bali pia katika ulimwengu mpana wa Kihispania. Hili lilikuwa kwa sababu, pamoja na manaibu kutoka Uhispania Moja, wale wengine kutoka mikoa ya Uhispania huko Marekani (moja katika makundi matatu ya wawakilishi waliokutana Cadiz lilijiita chama cha “Wamarekani”), walishiriki katika kuandika matini hizo. Wengine katika hawa baadaye walikuja kuwa viongozi wa mavuguvugu ya kupigania uhuru katika Marekani Kusini. Katiba ya Cadiz hivyo basi haikuvutia tu katiba andamizi za Uhispania, bali pia ingekuwa kama msingi wa katiba za kwanza za nchi huru za Marekani Kusini. (Tunaweza kusema kwa muhtasari kuwa katika takribani nchi zote za Marekani Kusini, mchakato wa kupigania uhuru ulianza katika mapambano ya kuweka demokrasia ya mamlaka katika mabaraza ya miji). Inafurahisha hata hivyo, kwa sababu hii, sheria nyingi za kwanza za uchaguzi katika karne ya 19 katika nchi zilizozungumza Kihispania katika pande zote za Atlantic zingetazamwa kurejelea matini hiyo ya kikatiba.
Kutokana na mwanzo huu muhimu, sheria za uchaguzi zilizopaswa kuongoza haki ya kupiga kura zilianza rasmi nchini Uhispania kutoka mwaka 1837, na upigaji kura ukianzishwa katika mwaka 1869, na zilifungamanishwa na sheria ya mwaka 1907. Hata hivyo, historia yenye joto ya Uhispania katika karne nzima ya 19 na sehemu ya karne ya 20 iliashiria migoto na maendeleo katika mchakato wa kutekeleza uhuru wa kidemokrasia na hivyo katika utendakazi wa mfumo wa uchaguzi.
Jamhuri ya pili, iliyopatikana katika mwaka 1931 baada ya matokeo ya chaguzi za manispaa yaliyolazimisha mfalme kung’atuka, pia yalianzisha upigaji kura wa wanawake. Wanawake wa Kihispania, waliopiga kura katika Chaguzi Kuu za mwaka 1931 na baadaye, walifanya hivyo kabla ya hili kufanyika katika nchi nyingine za Ulaya Magharibi (kabla Ufaransa kwa mfano). Ushindi wa Popular Front katika uchaguzi wa 1936, matokeo ambayo hayakushukiwa na yeyote, katika miezi michache yalizalisha jibizo lisilo la kidemokrasia na kuzuka kwa vita vya kikabila kuanzia mwaka 1936-39. Uliishia katika ushindi wa Jenerali Franco kutokana na mizozo ya vikosi vya ripablika na uungwaji mkono mkubwa kutoka tawala za kifasisti.
Ni wazi kwamba uanzishaji wa udikteta uliowekwa kwa takribani miaka 40 kama kizingiti dhidi ya utekelezaji wa haki za kidemokrasia. Hata hivyo, miongo hii minne haikutosha, kwa kuwa mabadiliko ya kisiasa ya Uhispania hatimaye yalikuja kudhihirika, kuondoa hali za awali au kujaza tajriba ya karne ya sheria za uchaguzi, kutoka kwa kumbukumbu za kihistoria: kati ya 1810 na 1936 sheria kumi na mbili za uchaguzi zilikuwa zimepitishwa pamoja na kanuni nyingi zinazoongoza kufanyika kwa chaguzi 55 za bunge katika Uhispania kwa muda huu mrefu.
Ukweli ulikuwa kwamba, hata kabla ya kifo cha Franco na katika Uhispania, kwamba katika mazingira ya usomi na miongoni mwa wanachama wa vyama pinzani vya kidemokrasia vilianza kujitokeza kama maficho ya kisiasa, suala la mfumo mwafaka wa uchaguzi kwa nchi hiyo lilikuwa likijadiliwa na kuchunguzwa. Punde baaya ya kifo cha Franco katika mwezi Novemba 1975, suala hili lilivuka na kuingia katika vyombo vya habari na mjadala mpana kuanza kuhusu ubora na ubaya wa mifumo yote miwili iliyotumiwa katika Jamhuri ya Pili na kuhusu mifumo tofauti tofauti iliyotumiwa katika nchi nyingine.
Maendeleo Katika Mabadiliko ya Kisiasa
Kufuatia kifo cha dikteta huyo mzee, mwafaka wa jumla uliafikiwa kuhusu umuhimu wa kujenga muungano kati ya mirengo ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na mrengo wa wanamapinduzi wa mfumo mkongwe. Mapinduzi ya amani yalifanywa kwa njia ya chaguzi za haki, wazi na za kuaminika kupitia kwa mfumo wa uchaguzi ambao ungetoa nafasi mwafaka kwa maszingira pana ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na vyama vya kitaifa, kushindania uwakilishi katika bunge la baadaye.
Mwaka mmopja baada ya kifo cha Franco, Disemba mwaka 1976, Wahispania walihitajika kuidhinisha kwa kutumia kura ya maamuzi sheria ya Mapinduzi ya Kisiasa ya nchi. Kwa kuepuka kutofautiana kivyovyote na asasi za kale, hili liliashiria kutambulika mwanzoni kwa kanuni ya uhuru, hivyo kuwezesha raia kujitangaza wazi na kuchagua ama mfumo wa uchaguzi unaoegemea demokrasia, au kuendelea kwa udikteta. Katika hali ya kwanza, kwa kupiga kura ya “Ndiyo”, mamlaka halali na huru yatapeanwa na kura kwa kubuni bunge la kiemokrasia, ambalo litachaguliwa miezi sita baadaye. Utatokana na mfumo wa uchaguzi ambao uatapaswa kuidhinishwa ikiwa matokeo ya kura ya maamuzi yatakuwa “Ndiyo” kwa demokrasia. Matokeo yalikuwa kwamba kura ya “Ndiyo” ilishinda pakubwa, kwa kuwa ni asilimia mbili tu ya wapigakura wa Uhispania waliopiga kura ya “La” kukataa demokrasia.
Kwa kuidhinishwa na kura ya maamuzi, mabadiliko ya kisiasa yalibuni mabunge mawili, yaliyojumuisha Kongresi la wajumbe 350 (kwa misingi ya mjumbe 1 kwa wakazi 100,000) na Seneti la maseneta 297 (idadi hii ikawa imebadilika). Mjadala kuhusu ujenzi wa mfumo wa uchaguzi ili kujenga mabunge haya mawili ulizungukia vipengele viwili vikuu ambavyo ni muhimu katika msingi wa mifumo yote ya uchaguzi: kuhusu mipaka ya utendakazi wake ikiwa maeneo bunge yanapaswa kubuniwa; na fomula ipi ya uchaguzi iliyokuwa mwafaka kuchukuliwa katika muktadha wa historia/ siasa za nchi?
Athari nzito ya historia kuhusu maeneo mbalimbali ya Uhispania iliashiria kwamba mfumo wa uchaguzi ulioidhinishwa kuanzia mwaka 1977 ulipaswa kuwasazisha kipengele cha idadi ya watu (k.v. ulipaswa kulipa kila eneo idadi ya wajumbe wa kuchaguliwa kulingana na idadi ya wakazi waliokuwa na haki ya kupiga kura) na fomula ambayo ingeruhusu idadi hiyo ya watu katika kila eneo kuwa na uwakilishi wa kiwango fulani kulingana na ukubwa wa eneo husika. Tutaeleza wazi hapa kuwa Uhispania ni nchi iliyo na sifa ya kukosa usawa wa kuenea kwa idadi ya watu kwa ardhi yake. Hivyo basi, mfumo wa uchaguzi uliochukuliwa kulingana na ugawaji wa viti kwa kila eneo bunge ulitegemea mfumo wa uwiliu wa uwakilishi wenye usawa, kujumuisha chaguzi katika kiwango cha kitaifa na orodha za kitaifa za vyama.
Ugawaji wa mipaka ya kila eneo bunge ulihusishwa na kugawika kwa Uhispania katika mikoa (kuna mikoa 50), ambayo iliongezwa maeneo bunge mawili yaliyowakilisha miji ya Uhispania iliyokuwa nje ya Peninsula. Usambazaji wa viti 350 vya Kongresi ulifanywa katika njia ambapo kila eneo bunge lingekuwa na viti viwili vya kudumu vilivyotolewa kwake kwa misingi ya mipaka, huku vingine vikigawika na kutolewa kwa kila eneo bunge kulingana na idadi ya watu. Hiki ndicho kigezo kinachowezesha visa vingine, kutoka uchaguzi mmoja hadi mwingine, kupata idadi ya wajumbe ambao kila eneo bunge lingechagua kutofautiana kwa kiwango fulani, Katiba hatimaye ilitambua idadi ya viti vilivyopaswa kuchukuliwa katika Kongresi ya Manaibu kuwa kati ya 300 na 400. Hata hivyo kwa kawaida, viti asilia 350 vya bunge vimedumishwa hadi hivi sasa, vikigawika katika maeneo bunge 52 kulingana na mfumo ulioelezwa.
Ili kufidia athari za kugawa viti kwa maeneo bunge kwa misingi ya mfumo huu “upana/idadi ya wakazi” (ambao ulipendelea ugombea mwingine kuliko inavyofanyika kwingine), mfumo wa uchaguzi ulitafuta kipengele cha kuerekebisha katika fomula ya kubadilisha kura kuwa viti. Mifumo ya washindi wa kura nyingi kama vile FPTP au TRS, ambayo ingeishia katika athari zisizolingana za mfumo mseto wa uwili, zilitupiliwa mbali, na mfumo wa PR wa orodha funge za vyama kuteuliwa, na kutumia fomula ya d'Hondt kugawa viti. Karatasi nyingi za kura zilizokuwa na orodha funge na Sheria ya Hondt kuhusu usawa viliwekwa ili kuamua idadi ya viti kwa kila mkoa, ambapo kati hali hii unapendelea ugombea mwingine. Kwa wakati huo huo, kipengele cha vizuizi dhidi ya ugombea kuingia katika usambazaji wa viti kuliwekwa katika kiwango cha asilimia tatu ya kura katika kila eneo bunge.
Mfumo wa Seneti, ambacho ni kitengo cha uwakilishaji wa kimaeneo, sasa hivi kilicho na maseneta 264 (hii inaweza kuwa na tofauti ya ama mmoja zaidi au chini), huwa na mpangilio tofauti, kwa kuwa ni viti 208 vinavyochaguliwa na uchaguzi wa moja kwa moja. Hivi huonyeshwa na uenezaji wa viti vinne kwenye kila eneo la mkoa, huru dhidi ya idadi yake, mpigakura akiwa na uwezo wa kuwapigia kura wagombea watatu wanaopatikana kwenye karatasi moja ya kura (ambako kila kundi la kisiasa huwasilisha wagombea watatu kuchaguliwa na huwa na nafasi tatu). Chini ya mfumo huu wa orodha wazi ya PR kwa mfano, inawezekana kuchagua kupigia kura mgombea mmoja au wagombea watatu wa vyama tofauti. Wanaosalia katika maseneta (56 katika bunge la sasa) huchaguliwa na kura ya moja kwa moja na mabunge ya maeneo huru 17 (“Wakomunisti”).
Kwa kurejelea haki za kupiga kura (kuwa na uwezo wa kuchagua) na haki za kupiga kura (kuwa na uwezo), mfumo wa uchaguzi wa Uhispania uliwapa raia wote bila masharti ya umri kamili (miaka 18), isipokuwa wale waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha mwisho cha mahakama au, katika hali ya wagombea wanaopaswa kupigiwa kura, wale wanaoshiriki kikamilifu shughuli fulani za umma (majaji, jeshi, viongozi wa ngazi za juu katika usimamizi, nk). Aidha, wagombea hawangelazimishwa kuweka pesa zozote ili kushindana katika uchaguzi. Ilipendelewa kuwa ili kuondoa mapendeleo yoyote dhidi ya wagombea wengine katika kuwasilisha ugombea wao katika hatari ya kuwahujumu, ingawa wangewasilishwa na chama kilichosajiliwa kisheria (kusajili chama cha kisiasa ni rahisi sana) au na kundi la wapigakura. Mwisho, kuhusiana na ushiriki wao katika uchaguzi, mpigakura aliachwa huru kabisa kuamua ikiwa angetekeleza haki hiyo yake ya kupiga kura au la – uwekaji wa masharti ya lazima katika kupiga kura katika mazingira hayo ya mabadiliko kutoka katika mfumo wa udikteta hadi kwenye demokrasia ungekuwa mkinzano wa kimawazo.
Kulingana na makataa yaliyowekwa ya wakati, miezi mitatu baada ya kura ya maamuzi ya kikatiba, kanuni za kwanza za uchaguzi (kama ilivyoelezwa hapo juu) ziliidhinishwa kwa kiwango fulani, na miezi mitatu baadaye uchaguzi mkuu ulifanyika kuchagua bunge rasmi. Uwezo wa kuunganisha wa mfumo wa uchaguzi ulifafanuliwa – muhimu kwa mabadiliko ya kisiasa ili kukubalika – licha ya kukosa ukamilifu kama inavyokuwa katika mfumo wowote wa uchaguzi, ulidhihirishwa na uweli kwamba wanataifa wa mrengo wa kushoto, kati, wasosholisti, wakomunisti, na Basque na waCatalan walipata uwakilishi katika bunge kulingana na matarajio yao. Wingi huu bungeni, uliopatika bila migawanyiko mingi na uliashiria hali ya mawazo katika nchi hiyo, ulikuwa muhimu katika kupatikana kwa mwafaka kuhusiana na matini ya Katiba. Utayarishaji wake changamano ulihitaji zaidi ya mwaka mmoja na hakukuwa na pingamizi kwamba kuanzia kwenye msimamo wa sheria linganishi, unaweza kutazamwa kutokana na vipengele vingi vilivyo dhabiti ulimwenguni.
Katika vifungu vya Katiba (Kifungu cha 8), pengine moja katika masuala muhimu ni kulipa Bunge mamlaka ya kipekee kuunda kanuni za uchaguzi, na pia lile la kuhakikisha kwamba sheria ya uchaguzi inakuwa na hadhi sawa na sheria ya kikatiba. Marekebisho yoyote, hata yangawa madogo kiasi gani, yanapaswa kuwasilishwa ili yachunguzwe na Tume ya Bunge kuhusu Katiba na kufuata hatua ziliwekwa kwa sheria za kikatiba.
Baada ya kuidhinishwa na kura ya maamuzi ya mwaka 1978 ya Katiba mpya ya Uhispania, Bunge rasmi, lililokuwa kimetimiza jumuku lake la kuunda sheria ya kimsingi ya Nchi, lilivunjwa hivyo punde. Chaguzi Mpya Kuu ziliitishwa ambazo zingetoa nafasi bunge la kwanza la kawaida, na pia chaguzi za kwanza za manispaa za kidemokrasia, hivyo kumaliza awamu ya kwanza ya mabadiliko ya kisiasa nchini Uhispania.
Lengo Amilifu na la Kisheria la Mfumo wa Uchaguzi
Mfumo wa uchaguzi nchini Uhispania, kama chombo muhimu cha kuhakikisha kura yenye usawa nay a kidemokrasia na kuzitazama kura katika mwelekeo wa uwakilishi wa kisiasa, umekuwa mfumo mwafaka, pakubwa hivi kwamba umeendelea kuwa imara na usio na mabadiliko yoyote kwa miaka ishirini baada ya nguzo zake kuu kuidhinishwa kwa pamoja katika awamu ya kwanza ya mabadiliko. (Umewezesha kuwepo kwa serikali inayoungwa mkono na watu wengi na iliyo dhabiti, na vilevile mabadiliko ya mwaka 1982 na katika mwaka wa 1996). Sheria ya kwanza Uchaguzi Kikatiba iliyopitishwa katika mwaka wa 1985 illidhinisha misingi ya mfumo uliobuniwa mwaka 1977 na kupanua maendeleo ya kanuni zilizotumiwa katika kipindi cha mabadiliko ya kisiasa.
Ni kweli kwamba mjadala fulani umeanzishwa kuhusiana na nafasi ya kuanzisha mabadiliko machache katika mfumo wa uchaguzi na kuidhinisha mfumo hup wa orodha wazi badala ya orodha funge, na mapendekezo ya woga yakisikika ujenzi wa maeneo bunge ya mwakilishi mmoja na ugombea vilevile. Hata hivyo, inaonekana kwamba hapana uwezekano kwamba katika mazingira haya changamano ya uchaguzi/ siasa za Uhispania, ubora wa mifumo mingine utafidia ugumu unaoweza kuchipuka, hasa kuhusiana na maeneo bunge ya mwakilishi mmoja, ambayo makundi yote ya kisiasa yanafahamu.
Katika hili, uhalali wa mfumo wa uchaguzi wa Uhispania unapatikana katika uamilifu wake kisiasa (katika mfumo wa jamii ya Kihispania) na uhalali ambao mfumo huu umepata taratibu kupitia kwa michakato mbalimbali ya uchaguzi iliyofanywa katika muda wa miaka thelathini ya mfumo huo. Hakuna kikosi chochote cha kisiasa ambacho kimewahi kuleta malalamishi ya ulimwengu kuhusu ulaghai katika uchaguzi, na malalamishi yanayotolewa kuhusu makosa ambayo yamewahi kutolewa ni finyu. Wagombea wote hukubali matokeo ya muda ya uchaguzi yaliyotangazwa na Ofisi ya Mambo yaKuu usiku wa uchaguzi kama ya kuaminika, na vyombo vya habari na wapigakura.
Sababu ya hili ilikuwa imani kubwa iliyoshikiliwa na walioandika sheria ya uchaguzi ya Uhispania, ambayo mfumo wowote ule wa uchaguzi, ambao kinadharia ungeweza kuzingatiwa kama bora kabisa ulimwenguni, ungekuwa ovyo katika matumizi. Ikiwa hatua za utekelezaji wake zingeacha mwanya wowote wa kuhujumiwa katika sehemu muhimu kama vile ujenzi wa orodha za uchaguzi, usajili wa wagombea, hesabu ya kura na nyingine nyingi, za kiufundi na kiusimamizi, ambazo moja kwa moja huathiri uhalali wa demokrasia kwa mchakato wa uchaguzi.
Ili kuepuka hatari za aina hii, Katiba na Sheria ya kwanza ya Uchaguzi (L.O.R.E.G.), Sheria ya Uchaguzi ilizingatiwa kuwa tawi la Sheria ya Kikatiba. Mwelekeo wa kisheria ulijengwa, hivyo kuweka nafasi za juu na kuzuia tafsiri mbaya iliyochochewa na kimya au utata katika kanuni na kuzuia mamlaka ya juu dhidi ya kulazimisha kanuni za ‘dharura’ ambazo zinaweza kuishia kuharibiwa katika awamu yoyote ya mchakato wa kubuni haki ya kupiga kura.
Nchini Uhispania hivyo basi, kwa misingi ya filosofia yake, Serikali au usimamizi katika upana wake haina mamlaka kisheria kudhibiti au kuanzisha vifungu vya kisheria vinavyoathiri udhibiti wa uchaguzi. Mamlaka ya ngazi za juu ina uwezo tu wa kuidhinisha kanuni ya kuitisha uchaguzi au kanuni za kiufundi za kutekelezwa kwenye sheria. Tangu Katiba iandikwe, mamlaka ya ngazi ya juu na usimamizi zimetekeleza wajibu wa kuchochea tu, na ni waandalizi tu wa mchakato wa uchaguzi. Kauli hii sasa hivi katika utamaduni wa uchaguzi wa Uhispania, na ingawa mfumo wa uchaguzi haujabadilika vile, kipengele kwamba unaimarika katika mijadala ya bunge ni ule wa utendakazi kamili wa kanuni za uchaguzi kuhusiana na uratibu wa mchakato wa uchaguzi, udhibiti wake, na usasa wake kiufundi.
Inatambulika pia kuwa dhana ya Sheria ya Uchaguzi nchini Uhispania, tangu kuidhinsihwa kwake kama sheria ya kikatiba, ni sehemu moja na, inavyoelezwa katika usuli wake, hujibu “haja ya kuvichukulia katika njia ya umoja na kilimwengu” vipengele vyote vya mchakato wa uchaguzi. Hakuna kukosekana kwa mifano katika Ulaya magharibi ya mifumo ya ‘kifumbo’ ya aina ya sheria, ambapo Sheria ya Uchaguzi ni mfumo jumla wa kudhibiti unaopaswa kufuatiwa au kukamilishwa na ama sheria nyingine moja au fungu la sheria kadhaa, au pengine na kanuni, ilani, n.k. zinazotoka kwa mamlaka ya ngazi za juu. (Badala ya kuchochea uwazi hivi huishia katika mchanganyiko wa kisheria). Hata hivyo, bunge la Uhispania kwa wakati liliondoa matumizi ya mfumo wowote mzee wa sheria zilizogawanyika kama marejeleo na kuamua kujumuisha vifungu vyote katika matini hiyo moja, hivi kwamba ingeweza kuwa amilifu nay a kuunganisha, na kuandika katika njia fupi na ya wazi. Katika hali hii, Sheria ya Uchaguzi inajumuisha mwongozo maalumu wa hatua, unaorejelea katika mtindo fulani sio tu kanuni za kikatiba zinazoongoza mfumo wa uchaguzi, bali pia vifungu vya moja kwa moja na makataa ya utekelezwaji wake ambavyo lazima vidhibiti, kufadhili, kutunza, na kusimamia mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia tofauti za makundi hayo (chaguzi za ubunge, kieneo nk).
Maelezo ya Vipengele Amilifu vya MfumoOperesheni za Usimamizi na Udhibiti wa Mchakato wa Uchaguzi:
Shirika linalowajibikia majukumu haya limebuniwa na jina Baraza la Uchaguzi, ambalo katika nchi nyingine za Marekani Kusini huitwa “Mamlaka ya Uchaguzi.” Baraza la Uchaguzi lina mpangilio wa vyeo vyake na hutokana na maeneo: Baraza Kuu la Uchaguzi; Mabaraza ya Mikoa na Kieneo; na Mabaraza ya Uchaguzi ya Jumuiya Maalumu (nchini Uhispania kuna mfumo wa ugatuzi wa miungano, na maeneo 17 huru). Shirika hili linajumuisha wanachama mseto huku sehemu fulani ya wanachama wake ikiteuliwa na Baraza la Mamlaka ya Mahakama na nyingine kuteuliwa na Bunge.
Baraza Kuu la Uchaguzi ni la kudumu; lina wanachama 13 ambapo wanane ni majaji wa Mahakama ya Ngazi za Juu waliochaguliwa na wengi na wengine watano walioteuliwa na Bunge, hushikilia Nyadhifa kuu Vyuoni katika Nyanja za Sheria, Sayansi ya Kisiasa, au Sosholojia. Rais huchaguliwa kutoka miongoni mwa majaji na Katibu (bila kura) ndiye Katibu Mkuu wa Kongresi ya Manaibu. Baraza Kuu la Uchaguzi hurekebishwa siku 90 baada ya katiba ya Bunge jipya baada ya uchaguzi. Ofisi yake inapatikana katika majengo ya Bunge. Mabaraza ya Uchaguzi, katika nafasi zake za uwakilishi, yana mamlaka ya kutosha kuhusu masuala yanayohusiana na uratibu wa mchakato, ingawa kwa sababu ya ufaafu hayafanyi majukumu maalumu ya kuratibu chaguzi, bali hutekeleza huduma zake zote katika kurasmisha operesheni zake na udhibiti na usimamizi wa uhalali wake.
Shughuli za uandalizi na usahihishaji wa Sensa ya Uchaguzi: Raia wa Uhispania huhitaji uwezo wa kupiga kura na ustahifu wao kufanya hivyo kwa kufikisha umri wa miaka 18, na hujumuishwa moja kwa moja kwenye orodha za uchaguzi. Wahispania kwa kawaida wanaoishi ng’ambo pia hujumuishwa kwenye orodha maalumu za uchaguzi. Raia wa kigeni wa Muungano wa Ulaya na Norwei, kwa kawaida wanaoishi nchini Uhispania, pia huingizwa kwenye orodha za uchaguzi, wanaweza pia kupiga kura na wanaweza pia kushiriki katika chaguzi za manispaa. Wale waliofikisha umri wa miaka 17 hujumuishwa kwenye orodha iliyopatikana, ili waweze kupiga kura wakifikisha umri wa miaka 18 kwenye siku ya uchaguzi. Hakuna kadi ya mpigakura inayotolewa kwa kuwa kitmabulisho chake huchunguzwa kwenye meza za uchaguzi; hivi ni kwa kutumia kitambulisho au pasipoti. Wapigakura (kwa hivi sasa milioni 30) hupokea kadi kwa anwani zaKuu kwao, japo huonyesha kwamba wamesajiliwa kwenye Sensa, na meza ya uchaguzi wanakopaswa kupatikana.
Utunzaji wa Sensa ya Uchaguzi ni jukumu la Ofisi ya Sensa ya Uchaguzi, shirika lililo chini ya uangalizi wa moja kwa moja wa Mabaraza ya Uchaguzi na kifedha hutegemea Baraza la Takwimu za Kitaifa (lililo pamoja na Wizara ya Fedha). Habari za kimsingi za kusaidia kwa manufaa ya Sensa hutolewa na Mabaraza ya Miji (kuna zaidi ya manispaa 8,000 ambazo ni lazima kuongezeka na kupungua kwa idadi ya watu, mabadiliko katika anwani, na mabadiliko katika ramani), na Balozi na Rejista za Raia katika visa vya vifo.
Hatua muhimu katika kusasaisha utunzaji wa Sensa ya Uchaguzi imechukuliwa hivi karibuni na mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1995; badala ya usasaishaji wa awali wa kila mwaka wa orodha za uchaguzi, usasaishaji wa kila mwezi umewekwa. Uwekezaji wa kiasi fulani umefanyika katika matumizi ya tarakilishi uliowekewa mamlaka ya ngazi za juu na mabadiliko rasmi ya Sheria, unaashiria kwamba kadiri muhula unavyokuwa mfupi ndivyo uwezekano wa kasoro unavyopungua. Hivi sasa, kila uchaguzi huchukulia sensa ya kila mwezi ya uchaguzi kama msingi wake kabla uitishwe, na orodha hizo za kila mwezi wa uchaguzi huonyeshwa kwa umma katika vituo vya kupigia kura wiki moja baada ya kuitishwa. Wapigakura wanaweza kupinga hivyo punde ikiwa kuna kosa au hawakusajiliwa.
Shughuli za mashirika yanayohusiana na mchakato wa uchaguzi: Ofisi ya Mambo yaKuu inawajibikia masuala muhimu na utunzaji wa gharama ya kifedha iliyiopatikana katika uandalizi wa uchaguzi. Ni lazima pia, bila shaka, kushughulikia masuala ya usalama ili kuhakikisha kampeni za amani wakati wa uchaguzi na hali ya kudhihirisha haki yao huru ya kupiga kura. Polisi mbalimbali na vikosi vingine vya Ulinzi wa Raia hupokea mafunzo katika taasisi zao kuhusu masuala haya na kwenye siku ya uchaguzi hubeba kadi ya mfukoni inayowakumbusha kuhusu vifungu muhimu vya Katiba na Sheria ya Uchaguzi. Kuhusiana na uandalizi na utumizi fedha, Naibu wa`Meneja huwa na jukumu la kupanga chaguzi na kupanga wakati na ratiba ya uchaguzi kulingana na vifungu mbalimbali vya Sheria ya Uchaguzi ambayo, ilivyosemwa, huwa wazi na hutambua vipindi vyote muhimu, ikiwa ni pamoja na saa za kufunga na kufungua vituo vya uchaguzi.
Katika sehemu za usimamizi wa uchaguzi katika utekelezaji wake, Ofisi Kuu ina uhusiano fulani na Baraza Kuu la Uchaguzi, na mara nyingi hujadiliana na Baraza kuhusu tatizo au swali lolote linaloweza kuzuka katika awamu mbalimbali za mchakato wa uchaguzi. Maagizo ya Baraza la Uchaguzi – hata kama wakati mwingine wafanyakazi wa kiufundi katika uchaguzi wana maoni tofauti wakati utekelezaji wake unapoelekea kuwa na matatizo – husikizwa bila tatizo.
Katika kiwango cha maeneo, kuhusiana na maagizo ya Ofisi Kuu, huduma za usimamizi za Serikali katika kila mkoa hushughulikia majukumu maalumu ya kuhifadhi na kusambaza nyenzo za uchaguzi, na vilevile kuchapisha karatasi na bahasha za uchaguzi. Ofisi Kuu pia huingia katika mikataba na mawakala wa kuenezaji sifa kuhusu kampeni za kutumia sauti na picha ambazo hutangazwa katika mchakato wa kuwaarifu au kuwakumbusha wapigakura kuhusu masuala fulani (kuonyesha orodha, hatua za kupiga kura kwa kutumia cheo, karatasi za utambulisho zinazohitajika kupiga kura, nk).
Jukumu muhimu la Ofisi Kuu ni hilo la kuupa umma matokeo ya muda ya kura zilizohesabiwa, ambayo watu wengi hutaka kusikia. Punde hesabu ya kura ikishafanywa, maelfu ya maajenti wa uchaguzi wanaowakisha usimamizi huchukua nakala ya matokeo katika kila mojawapo wa hizo meza takribani 50,000 za uchaguzi zilizosambazwa kotekote nchini, na kuyatuma kwa njia ya simu hadi kwenye vituo vilivyowekwa tarakilishi, ambavyo huwa na habari na huzituma kenye tarakilishi kuu. Nchini Uhispania kasi ya kuwasilishwa kwa matokeo ya muda ya uchaguzi husaidiwa pakubwa na ukweli kwamba maeneo yote ya uchaguzi yana simu kwenye jingo hilo au karibu. Pesa kiasi cha haka pia huwekwa katika shughuli hii (kiasi cha dola 5,000,000 za Marekani zinaweza kuonyeshwa).
Matokeo yajuhudi hii kubwa mkesho wa kuamkia uchaguzi yamekuwa kufupisha muda unaochukuliwa kuiarifu nchi kwa kina kuhusu matokeo ya uchaguzi, ili saa baada ya kufungwa kwa shughuli za upigaji kura katika meza zote 50,000 za uchaguzi, hesabu ya kina inawekwa kwenye tarakilishi na kuwasilishwa kwa watu katika asilimia mia moja ya uhakika. Makundi pinzani ya kisiasa na vyombo vya mawasiliano huwa na njia za moja kwa moja kuwaunganisha hadi kwenye tarakilishi kuu katika Ofisi Kuu, hivyo kuvipa uwezo wa kuafikia katika wakati na kutoka mwanzoni, katika ujenzi wa hesabu ya kura. Tangu mwaka 1996 mchakato wa kuhedsabu umetambulishwa kwa wavuti ulimwenguni kote. Hivi sasa, uwezekano wa kuanzisha upigaji kura wa kielektroniki unachunguzwa, ingawa haijakuwa wazi ikiwa uwekezaji katika teknolojia hii mpya – majaribio mengine yamefanyika – unafaa, kwa kuwa unaweza kupunguza kwa saa tatu pekee kasi ambayo Uhispania imewahi kutumia kupiga kura na mfumo uliopo wa kuhesabu kura. Kipengele kingine kisicho na habari za kutosha ni kile utunzaji na uangalizi wa maelefu ya vifaa vya upigaji kura wa kielektroniki ambavyo huenda ikalazimu vichunguzwe kabla ya kila uchaguzi mpya. Kura kwenye ‘tovuti’ pia inachunguzwa.
Operesheni za udhibiti wa wapigakura na wagombea katika mchakato wa uchaguzi:
Nchini Uhispania uwepo wa waangalizi wa kimataifa haukupendekezwa rasmi na chama chochote cha kisiasa katika chaguzi za kwanza za mabadiliko miaka thelathini iliyopita. Hivi ilikuwa kwa sababu, kwa upande mmoja, vyama vikuu vya kisiasa vilivyoidhinishwa kisheria vilikuwa na muundo msingi na usimamizi uliovitosha, pamoja na wanajeshi na wafuasi wengine, uwekaji wa kampeni. Aidha, vingehakikisha maadili mwafaka ya kura kwa kuwapo kwa wafuasi wake halali katika takribani vituo vyote vya uchaguzi katika maeneo bunge husika. Kwa upande mwingine, mfumo wa uchaguzi wa Uhispania ulianzisha kuanzia mwanzo kanuni kwamba uhuru wa watu ulipaswa kuashiria udhibiti wa moja kwa moja wa sheria ya uhuru katika kupiga kura na wapigakura wenyewe, wao wakiwa ndio wenye uwezo wa kusimamia na kuongoza mchakato wa upigaji kura na hesabu ya kura. Sheria ya Uchaguzi, kama ilivyojengwa baadaye, imeendelea kufafanua vipengele hivi viwili kwa kina.
Kuhusiana na uwezo wa kudhibiti wagombea katika mchakato wa uchaguzi, sheria za Uhispania hazina chochote kipya. Ugombea huwasilishwa kwa Mabaraza ya Uchaguzi katika kila eneobunge, ambayo hutumia kigezo cha malengo katika kutathmini ufaafu wake; ni lazima pia kwa kila makundi pinzani ya kisiasa katika chaguzi kuteua Mwakilishi kwenye Baraza Kuu la Uchaguzi katika muda usiozidi siku tisa baada kuitishwa kwa uchaguzi, ili kuwa kama msemaji wa ugombea huo. Hili hata hivyo halimaanishi kwamba Wawakilishi hawa wanashiriki katika mipangilio ya usimamizi huo.
Kuhusiana na udhibiti wa kura na wapigakura wenyewe, inaweza kuwa hali mpya kabisa kwa baadhi ya watu kwamba ni lazima kwa wanachama watatu wa meza ya uchaguzi (Rais mmoja na Wajumbe wawili) kuwa wapigakura waliosajiliwa kwenye orodha ya wapigakura iliyo mezani. Utaratibu wa uteuzi wao huelekea kuepuka kuingiliwa kivyovyote, kama sehemu ya umma kugawa hufanyika katika mkutano wa pamoja katika kila Ukumbi wa Mji kati ya siku 25 na 29 baada ya kuitishwa kwa chaguzi. Katika mkutano huu wanachama kwa majina tu huteuliwa na wengine sita mbadala, ambao ni lazima wawepo mezani kwenye siku ya uchaguzi ikiwa wanachama wale wa majina wakikosekana. Marais ni wale walio na kiwango cha juu cha elimu. Wapigakura walioteuliwa na kundi wana wajibu wa kisheria kutekeleza majukumu haya na teuzi hizo huwasilishwa kwao kwa barua rasmi kutoka kwa Baraza la Uchaguzi, na kuwasilishwa kwenye makazi yao. Pamoja na arifa hizi, wao hupokea Mwongozo wa Maagizo inayosimamiwa na Baraza Kuu la Uchaguzi. Miongozo hii, kama makala nyingine za uchaguzi, huchapishwa na Ofisi Kuu katika matoleo yao ungi lugha ya maeneo bunge hayo, ambayo yana KiCatalan, KiBasque, au KiWagalicia kama lugha zao rasmi, na vilevile kama ilivyo katika KiCastilia, ambacho ndicho lugha rasmi kwa Nchi nzima. Nchini Uhispania, lugha ya Kihispania haimo rasmi katika Katiba, ambayo hurejelea tu kwenye lugha inayojulikana tu kihistoria kama KiCastilia; hujulikana kwa upana kama lugha rasmi ya Uhispania, kwa kuwa katika Kifungu cha Tatu cha Katiba, lugha nyingine zinazotajwa kuchukuliwa tu kama lugha za Uhispania.
Uteuzi wa wanachama wa meza kimakundi kutoka miongoni mwa wapigakura na hakikisho zinazotolewa kwao kutumia mamlaka yao katika njia huru, ambayo mara nyingi hufanywa na uangalifu mkubwa, pia zimekuwa muhimu katika kuhakikisha kwamba ulaghai unakuwa mgumu katiki kiwango cha upigaji kura, hatua ya kuhesabu kura, (hesabu hufanyiwa machoni pa umma katika eneo moja na la upigaji kura), na matoleo yanayofuatia na Rais na mwanachama mwingine kwenye meza, ya nakala asilia iliyowekwa kwenye bahasha na kufungiwa na Jaji aliye karibu. Wawakilishi wa wagombea (ambao kila mmoja huwa na nakala ya orodha ya uchaguzi ya meza na ni lazima atie sahihi kwenye Kumbukumbu za maendeleo, ambayo wao hupata nakala) pia hushiriki. Kwa kuonyesha mbele ya umma katika kituo cha upigaji kura ni arifa iliyo na matokeo, ilhali nakala katika bahasha iliyofungiwa hupeanwa mwanachama wa tatu anayesubiri wa meza ya Tarishi ambaye huichukua kutoka kila kituo cha kupigia kura ili kuiwasilisha kwa Baraza la Uchaguzi la Mkoa au Eneo ambalo hufanya hesabu ya mwisho.
Katika mtazamo wa jukumu muhimu la meza ya uchaguzi, Sheria ya Uchaguzi imeanzisha mahitaji maalumu kuhusiana na idadi ya wapigakura kwenye meza, na imeweka sehemu au maeneo fulani yanayojumuisha kati ya wapigakura 500 na 2,000 ambao hugawika katika meza mbalimbali (kwa kawaida idadi ya juu kabisa ya wapigakura kwa kila meza huwa 1,000). Aidha, kigezo cha upana wa maeneo huwekwa, hivi kwamba katika kila manispaa, hata kama ni wapigakura wachache ambao manispaa hiyo inaweza kuwa nao, angalau kila meza huwekwa japo wapigakura wanaweza kuwa wachache chini ya 500. Orodha ya uchaguzi ya kila meza hupangwa kialfabeti kwa kuzingatia majina ya ukoo. Sheria ya Uchaguzi pia inatambua kuwa muda wa kupiga kura ni saa 11 (muda wa kutosha kadiri taratibu za uchaguzi zinapoendelea kufanywa haraka) na vituo vya upigaji kura huenda visifungwe kati ya saa tatu asubuhi na saa mbili usiku, hata kama wapigakura wote kwenye orodha wamepiga kura.
Shughuli za usimamizi wa kifedha wa mchakato wa uchaguzi: hii ni sehemu muhimu ya usimamizi katika awamu zote za mchakato wa uchaguzi. Kulingana na Sheria ya Uchaguzi ya Uhispania, Serikali inapaswa kupunguza si gharama zinazotumiwa katika utekelezaji na usimamizi wa uchaguzi wowote ule bali pia, kulingana na Sheria ya Kikatiba kwenye Ufadhili wa Vyama vya Kisiasa, inapaswa pia kupunguza gharama za uchaguzi za makundi ya kisiasa yanayoshindana katika chaguzi za kuingia katika Mabunge Makuu, ya Kieneo, au ya Ulaya. Gharama za uchaguzi wa kuingia katika mabunge huru zinapaswa kuchukuliwa na Jumuiya Huru katika kanuni zizo hizi. Idara ya Ofisi Kuu inayoshughulikia uenedeshaji wa uchaguzi ina jukumu la kuandaa bajeti na usimamizi wa fedha za umma za kutumika katika uchaguzi kulingana na vifungu vya Sheria ya Uchaguzi. Kwa hakika, Ofisi Kuu hufanya kazi kama shirika simamizi lililo na uwezo wa kutoa kandarasi ya kuletwa kwa nyenzo kutoka nje na huduma zinazohitajika kuratibu chaguzi; aidha hufanya kazi kama kiunganishi kati ya Hazina na washiriki wanaoshindana katika chaguzi.
Sheria ya Uchaguzi inaeleza – katika makadirio yaliyoidhinishwa na Bunge – kwamba baada ya siku ishirini na tisa za kuchapishwa kwa kanuni ya kuitisha uchaguzi, vyama au makundi ya kisiasa ambayo awali yamekuwa yakiwakilishwa, yanaweza kuwa masurufu yaliyopunguzwa takribani asilimia 30 ambayo vilipata katika uchaguzi uliopita. Punguzo lote watakalopata mwishoni mwa mchakato mpya wa uchaguzi, alimuradi vinapata uwakilishi, litategemea idadi ya kura. Pesa hizo hulipwa na Serikali baada ya kukamilika kwa kipindi kilichotengewa madai muhimu na baada ya kuwasilisha (siku 100 baada ya kura) makala ya kina kuhusu mapato yote na fedha zote za matumizi ya uchaguzi kwenye hazina kwa sababu hii ya ugombea, ambayo inaweza kukaguliwa katika mchakato mzima wa uchaguzi na Baraza la Uchaguzi na Ofisi ya Ukaguzi ya Kitaifa. Sheria ya Uchaguzi inazuia michango ya makampuni au watu binafsi kwenye kampeni za uchaguzi za chama cha kisiasa au kundi la wapigakura kuliko ilivyo katika kiasi kidogo (takribani US $7,000). Wakikosa kupata uwakilishi au kupata kura chache kuliko zile zilizotumika kwa hesabu ya kwanza, wagombea wanapaswa kurudisha matoleo yaliyotolewa kama sehemu au kwa ukamilifu.
Pesa za matumizi zilizopunguzwa na Serikali huhusishwa na shughuli ya uchaguzi ya wagombea ni za jumla: karatasi za kura na bahasha; pesa za matumizi ya utangazaji na kueneza habari ili kupata kura; kukodi majengo na ofisi za kampeni; fidia za kifedha zinazolipwa kwa wafanyakazi wasio wa kudumu wa vyama, wanaoajiriwa wakati wa kampeni; fedha za matumizi ya usafiri na uchaguzi wa wagombea, viongozi na wafanyalzi wa kusaidia wa kampeni; na gharama ya mawasiliano au kutuma barua. Isitoshe, ridhaa ya benki kwenye mikopo ya kifedha iliyotolewa kisheria kwa kundi linalosimamia kampeni hadi kwenye tarehe ambapo Serikali inalipa nyongeza kuhusiana na kila mgombea kulingana na matokeo yake ya uchaguzi.
Tutaeleza kuwa kuna uwezekano wa kubadilisha sheria ya uchaguzi inayojadiliwa sasa chini ya mjadala kuhusiana na kupunguza vyama vya kisiasa na kampeni za uchaguzi, kutokana na matatizo ya ufisadi. Uhispania, kama nchi nyingine katika Magharibi ya Ulaya, imekubwa na shida hii katika miaka ya hivi majuzi. Inasababishwa na ufadhili wa kisiri na usio halali wa kampeni nyingine za uchaguzi, ambapo gharama huwa ghali sana na ambapo mipaka ya kisheria kuhusu kiwango cha juu kabisa cha gharama zilizobuniwa kwa raslimali ya umma hazizingatiwi. Mjadala unaelekea kuegemea pakubwa kwenye uwezekano wa kufadhiliwa na watu binafsi au makampuni, kwa kuimarisha kiwango cha michango kama hiyo inayokisiwa sasa hivi katika Sheria. Hata hivyo, ikiwa sheria ya uchaguzi itarekebishwa, michango ya kibinafsi ya kifedha inaweza kila mara kutokana na mwafaka wa bunge, kulazimisha uchapishaji na udhibiti wake.
Mabadiliko kutoka kwenye Serikali za Kimaeneo
Haitawezekana kuhitimisha maelezo ya mfumo wa kisiasa wa Uhispania na mfumo wake wa uchaguzi bila kutaja hata katika muhtasari kitu muhimu kihistoria kama vile mabadiliko kutoka kwenye serikali ya kiimla hadi kwenye mfumo bora wa kidemokrasia. Tunayarejelea mabadiliko mabadiliko yaliyokinzana na yale yaliyoelezwa hapo awali, kutoka kwenye Serikali kuu hadi kwenye Serikali iliyogatuliwa – mabadiliko ambayo katika kiwango cha kijamii na kisiasa yamekuwa magumu na changamano kuliko yale ya kutoka kwenye udikteta hadi kwenye mfumo wa kidemokrasia. Pengine lilikuwa tatizo kubwa ambalo Katiba ya mwaka 1978 ilipaswa kutatua.
Kwa kawaida, kwa watu wengi wa Uhispania ambao tunaweza kusema walikuwa wahafidhina kupita kiasi, sawa na ilivyo kwa wengi walio na wazo la maendeleo ya kisiasa, imekuwa na ingali, vigumu kukubali utambulisho uliotolewa kwa viongozi wa kitaifa, tofauti za kiisimu, na ujenzi wa serikali huru katika maeneo mbalimbali ya Uhispania ambayo yamekumbwa na mamlaka mapana. Isitoshe, kuingia kwa demokrasia kulichochea mlipuko wa madai ya kitaifa, ambayo tangu wakati huo yamehusishwa pakubwa katika mfumo wa uchaguzi kupitia mikakati ya uchaguzi inayokinza mchakato wa ugatuzi. Inavyodhihirika, mfumo huo unaruhusu HB, ugombea wa kisiasa unaohusishwa na kundi haramu la ETA, kugombea kisheria katika chaguzi zote (za bunge , manispaa, Basque Huru, na Ulaya). Kila mmoja amekubali matokeo hayo kila mara, ingawa kwa miaka fulani wameonyesha kudorora kwa hali ya juu katika kura ya HB.
Katika mfumo huo migongano hii yote, ruwaza ya Uhispania ya ugatuzi ilikuwa asilia, hivi kwamba ilitilia maanani uwepo wa mahitaji ya uhuru dhidi ya mamlaka kuu. Haya yalikuwa dhabiti sana katika eneo la Catalonia na katika nchi ya Basque, katikati katika sehemu nyingine, na hasa ilikuwa bure katika maeneo kadhaa, na iliweza kubuni mkakati wa kudumu kwa usawazishaji wa uwezo wa kujitawala kwa kila eneo.
Kwenye kanuni hizi tarafa ya Uhispania iliongozwa katika Jumuiya 17 Huru, kila mojawapo ikiwa na Bunge lililochaguliwa na wingi wa kura. Mabunge haya yalibuniwa katika njia halali, mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa Serikali kuanzia na chaguzi huru za nchi ya Basque na wa Catalonia uliofanyika mwanzoni mwa 1980. Mabunge ya Galicia na Andalucia yalichaguliwa kuanzia hapo, katika miaka ya 1981 na 1982 mtawalio. Maeneo haya manne ndiyo yanayoitwa “mataifa ya kihistoria”. Mabunge yanayosalia 13 huru yalibuniwa kuanzia kwenye chaguzi huru zilizofanyika wakati huo na chaguzi za kieneo za mwaka 1983.
Katika mchakato wa kugatua Serikali, moja katika sifa muhimu za usawazishaji ulikuwa kuchukuliwa kwa mfumo kama huo wa uchaguzi katika eneo zima: uchaguzi wa mabunge huru (ingawa manaibu wao hutofautiana katika idadi) huongozwa na kanuni zizo hizo kwa usambazaji wa viti kama ilivyo kwa uchaguzi wa manaibu kenye Bunge kuu (las Cortes). Kila Jumuiya Huru ina Sheria yake ya Uchaguzi, ambayo inapaswa kuoana na Sheria ya Jumla ya Uchaguzi katika hatua zake za kimsingi.
Kutokana na vikao vya mabunge huru yaliyochaguliwa na wingi wa kura, hali inayochangia katika kujengeka kwa mapendeleo ya maeneo limechipuka katika sehemu nyingi ambako ufahamu huu haupo. Hata hivyo, kuna hali ya kujumuishwa kwa utaifa katika mfumo imara na wenye mpangilio mzuri, ambao huruhusu mamlaka kuu na huru kujadiliana kwa misingi ya uhalali, ambao zote mbili hupata katika debe la kura. Ni majadiliano haya ambayo yametoa nafasi kwa migao mikubwa ya ugatuzi (kubwa kushinda ule ulio katika majimbo mengi yanayofahamika kama ‘majimbo’) ambayo sasa hivi yamekubalika na wengi.