ACE
Encyclopaedia   Mada   Mifumo ya Uchaguzi   Uchunguzi wa Mifumo ya Uchaguzi  
Ufini: Uteuzi wa Mgombea na Usawa wa Vyama

 

 

Mfumo wa uchaguzi wa Ufini uilianzishwa katika mwaka 1906. Chaguzi zilifanywa mwaka uliofuata, ambazo ndizo zilizokuwa chaguzi za kwanza huru zenye usawa kwa wanaume na wanawake. Katika mwaka 1917 Ufini ilipata uhuru kutoka Urusi, na Katiba yao ya uhuru ya Jamhuri mpya iliwekwa katika matumizi mwaka 1919; baadaye mfumo tofauti na wa ubunge ambao uliitwa nusu –urais ulijengwa. Tangu mwaka 1906, wanawake na wanaume wote wamekuwa wakishiriki kupiga kura na kuteuliwa katika chaguzi. Umri stahifu kwa upigaji kura umekuwa ukipunguzwa kutoka miaka 24 katika mwaka 1906 hadi kwa 21 katika mwaka 1944, hadi 20 katika mwaka 1969 na hatimaye 18 katika mwaka 1972. Sifa moja bainifu ya chaguzi za Ufini ni idadi kubwa ya kura zilizopigwa kwa njia ya kura. Kwenye uchaguzi wa mwaka 1995, asilimia 43.4 ya kura halali zilipigwa.

Bunge la Ufini lina jumla ya wabunge 200 waliochaguliwa kutoka maeneo 15. Katika wilaya zote, ila Visiwa vya Aland vinavyozungumza lugha ya Kiswidi, utoaji wa viti kwa vyama (ikiwa ni pamoja na miungano ya uchaguzi) ni sawa kwenye kura zinazofuata za mfumo wa d'Hondt wa orodha ya chama mfumo wa Uwakilishi wenye Usawa, tazama Mfumo Mseto wa Usawa wa Wagombea. Kabla ya mwaka 1954, wapigakura walipaswa kuteua kati ya orodha za wagombea (orodha ilijumuisha wagombea wawili na mmoja mbadala); mabadiliko ya baadaye kwenye mfumo inamaanisha kuwa sasa hivi inawezekana kuchagua mgombea mmoja pekee. Mabadiliko haya yalibadilisha mfumo wa uchaguzi wa Ufini katika mfumo usio wa kawaida wa orodha, ambao unawalazimu wapigakura kupigia kura wagombea binafsi. 

Uchaguzi wa wagombea kutoka kwenye orodha ya chama hauamuliwi mapema, japo hutegemea idadi ya jumla ya kura zinazopigiwa kila mgombea. Mpigakura huteua idadi iliyowekwa ya mgombea wake (orodha ya wagombea, kila mmoja akiwa na nambari ya kumtambulisha, huwa mbele ya mpigakura) na huaindika kwenye karatasi ya kura. Kwa sababu hiyo, uchaguzi si ushindani tu kati ya vyama; bali pia ni ushindani kati ya wagombea kwenye orodha ya chama. Aidha, wapigakura hakuna mpigakura anayepewa nafasi ya kupigia kura chama; bali wagombea walioteuliwa, lakini ambao hawakuorodheshwa na chama au orodha isiyo ya chama.

Huku wilaya za Visiwa vya Aland zikichagua huchagua mjumbe mmoja, maeneo mengine 14 ni ya ungiwanachama. Uzito wa wilaya huamuliwa na idadi ya watu, ambayo hupendelea maeneo bunge katika sehemu za mashambani kaskazini na mashariki. Usawa bado ni wa kiwango cha juu katika matokeo yote ya uchaguzi, ingawa tofauti kati ya maeneo bunge katika hali hii ni kubwa. Kwa jumla, maeneo bunge ya sehemu za mijini yana usawa, na maeneo mengi ya sehemu za mashambani hutoa matokeo mengi yasiyo na usawa.

Kwa kuwa fomula ya d'Hondt ya kugawa viti hupendelea vyama vikubwa, nchini Ufini vyama vidogo aghalabu huchukua nafasi ya kujiunga na miungano ya uchaguzi pamoja na chama kimoja au zaidi. Miungano ya uchaguzi hubuniwa katika kiwango cha wilaya, kumaanisha kwamba chama kimoja kinaweza kujiunga na miungano tofauti katika wilaya 14; miungano hii hivyo basi ina viwango tofauti vya kufaulu. Isitoshe, kulingana na sheria ya uchaguzi ya mwaka 1969, mgombea anaweza tu kuteuliwa katika eneo bunge moja. Kabla ya hilo, mgombea angeweza kuteuliwa katika wilaya zote, mkakati maalumu wa kupata kiongozi mstahifu wa chama kidogo. Vyama vingi vidogo hujiunga na miungano, na bila nafasi hii ya usawa kati ya kura na viti, kwa kiwango fulani, kudhoofishwa.