Ujenzi wa asasi za kisiasa zilizo na uwezo wa kuhakikisha uwepo serikali dhabiti na inayofaa limekuwa kero na changamoto kubwa nchini Indonesia, nchi iliyo na makabila mengi na visiwa takribani 20,000 ambavyo umoja wake uliegemea tu ushirikiano wao dhidi ya mkoloni. Utambulikaji wa kisiasa nchini Indonesia ni suala changamano, awali likihusishwa na mirengo mbalimbali ya Uislamu, hadi katika taifa huru, au katika maeneo mengine Ukristo-ambapo tathimini ya ubora wa uongozi na athari za ufisadi sasa, katika mwaka 2004, vinaonekana kuongezwa. Kubuni mifumo ya uchaguzi jumuishi na mwafaka katika mazingira ya umpja wa serikali ya Indonesia hakujawa rahisi.
Uchaguzi mkuu wa kwanza nchini Indonesia baada ya kujinyakulia uhuru mwaka 1945 ulifanyika mwaka wa 1955. Mfumo wa PR katika maeneo 15 ulitumika bila kupingwa. Viti viligawika kwa misingi ya usawa wa idadi, huku mgao mdogo wa ziada ukipewa maeneo ya Kisiwa cha Outer. Mbinu ya Kikubwa kuchukua Vilivyobaki iliyotumia Idadi ya Hare ilichukuliwa. Vyama au mashirika yangeteua orodha, na wagombea wenyewe pia wangeteuliwa. Wapigakura wangepigia kura ama orodha au kwa kuandika katika jina la mgombea mmoja.
Bunge lililopatikana lilijumuisha vyama 27 na orodha, pamoja na mwanachama mmoja. Vyama vikubwa vinne vyote vilipata asilimia 16 na 23 ya kura. Chama kimoja hakikuweza kupata uungwaji mkono wa kutosha bungeni; wala hata vyama viwili havikuweza. Ilikuwa vigumu kuunda serikali, na uwezo wao wa kudumisha imani katika bunge ulikuwa mdogo. Bunge la Wajumbe, lilichaguliwa muda mfupi baadaye ili kutengeneza katiba ya kudumu, lilikuwa na usawa kama huo kisiasa na lilishindwa kufikia makubaliano.
Kupoteza kwa imani kabisa katika asasi za kisiasa za nchi na upinzani dhidi ya serikali ya muungano yalimwishia Rais Soekarno kuingiza mfumo wa imla katika mwaka 1959. Mfumo huu ulikwepo hadi ulipobadilishwa na Hali Mpya ya Rais Soeharto katikati ya miaka 1960, mfumo mpya ulioweka mamlaka mengi katika matawi tendaji, bunge na mahakama. Chaguzi zilifanyika, lakini kampeni zilidhibitiwa kabisa, wagombea wengi kufutiliwa mbali, na kanuni zilitumiwa katika njia kandamizi dhidi ya wapinzani wa serikali. Azma ya kukamilisha udhibiti wa kitengo kikuu dhidi ya uteuzi wa wagombea ilichangia katika uteuzi wa mfumo wa PR wenye orodha funge. Soeharto alitaka kuondoa wasiwasi katika umaarufu wa kisiasa wa Wajava, na Java kilipokea tu nusu ya viti vilivyochaguliwa, japo kilishinda zaidi ya asilimia 70 ya kura zilizosajiliwa katika mwaka wa 1955. Ingawa idadi hii imepungua, ilikuwa asilimia 61 katika mwaka wa 2004.
Kuingia katika Demokrasia: Chaguzi za mwaka 1999
Baada ya utawala wa Soeharto kuanguka katika mwaka wa 1998, sheria mpya za uchaguzi zilikamilishwa baadaye Januari mwaka 1999. Mfumo wa uchaguzi- ulioelezwa kama ‘mfumo sawa uliokuwa na sifa za kiwilaya’-ulikuwa wa kipekee. Ulikuwa zao la wazi majadiliano ya kisiasa kuweka nyongeza dhidi ya makataa ya wakati. Makubaliano haya yaliafikiwa bungeni na vyama vya enzi ya utawala wa Soeharto, ambavyo vilikuwa chini ya shinikizo kutoka kwa vyama vipya na vingine vilivyokuwa nje ya majadiliano hayo, pamoja na kutetea misimamo yao na kutokana na shinikizo walilopata kutoka katika maeneo yenye ufuasi wao mkubwa. Kutokana na shinikizo hizi, haiwezekani kuona kwamba matokeo ya mwisho ya majadiliano hayo yangekuwa tofauti.
Katika uchaguzi wa Juni 1999, kila mpigakura alipiga kura moja kwa chama cha siasa. Mikoa yote 27 ilidumishwa kama wilaya za uchaguzi, huku zikiwa na viti kuanzia vinne hadi 82. Idadi ya viti vilivyoshindwa na kila chama katika kila mkoa ilitambuliwa kutokana na kanuni za PR, na kila mgombea kwenye orodha ya aliunganishwa na chama kwenye moja katika wilaya hizi zenye uwili (kota, mabaraza ya mji, na kabupetan, mabaraza yaliyokuwa nje ya maeneo ya mji) katika mkoa huo. Kutokana na suala la kudumisha amani katika nchi hiyo, kulikuwa na sheria zilizozuia usajili hasa chama cha kieneo. Sheria kuhusu vyama vya kisiasa ilihitaji kwamba vyama vyote vya kisiasa vilivyowania nyadhifa katika chaguzi vipatikane katika angalau mikoa tisa.
Sheria hiyo haikuwa wazi kuhusu maelezo ya muhimu. Mbinu ya kubadilisha kura zilizopigwa katika viti vilivyopatikana haikujumuishwa. Wala hakukuwa na kanuni za kutambua wagombea kutoka kwenye orodha ya chama ambaye angechukua viti vilivyoshindwa na chama hicho. Masuala haya yalitatuliwa tu baadaye.
Kanuni za kupeana kiti cha mwisho zilishikilia Mbinu ya Kukubwa kuchukua Mabaki kwa kutumia Idadi ya Hare. Kupeana viti vilivyoshindwa kwa wagombea kulikuwa changamano hata zaidi. Kwa kawaida, uongozi mchache wa vyama vikuu pia ulikubaliana na kanuni hizo, na uongozi huo ulichukua mamlaka ya kueleza Tume ya Uchaguzi wagombea waliokuwa wamechaguliwa kuchukua viti ambavyo chama chaoi kilikuwa kimeshinda.
Chaguzi za 1999 hata hivyo zilitazamwa kama zilizokuwa za kwanza tangu mwaka 1955 kukubalika kwa jumla, japo kulikuwa na maswali maalumu au ya kieneo. Vyama vitano vilipata zaidi ya asilimia 2 ya kura: nguvu zavyo nyingi zikitofautiana pakubwa katika sehemu tofauti tofauti za Indonesia. Vyama vingine kumi na sita vilipata uwakilishi.
Kumbukumbu ya uchaguzi wa mwaka 1999 ilipitwa haraka kutokana na marekebisho kamili ya katiba ya 1945. Kukamilika kwa marekebisho haya katika mwaka 2002 kuliishia katika mabadiliko muhimu, yakiwa ni pamoja na kuingizwa kwa migao ya mamlaka, kanuni ya kuhakikisha usawa, uchaguzi wa moja kwa moja wa rais na makamu wake, na ujenzi wa bunge la pili la wajumbe walioteuliwa katika maeneo likiwa na mamlaka machache sana. Marekebisho manne muhimu yalipitishwa kwenye katiba, hivyo basi kubadilisha kabisa njia ambamo asasi hizi zingefanya kazi baadaye, na sheria tano mpya – kuhusu uchaguzi, uchaguzi wa rais, vyama vya kisiasa, muundo wa mashirika yaliyochaguliwa, na ujenzi wa Mahakama ya Kikatiba-yalipitishwa. Indonesia hivi sasa inapatikana katika familia kuu ya marais wenye demokrasia.
Kura za Ungi wapigakura Zinakosa Kuungwa Mkono kwa Uchaguzi wa Bunge
Baada ya 1999, kulikuwa na kampeni kubwa ya kuidhinishwa kwa mfumo wa SMD miongoni mwa vyombo vya habari na hasa katika anga za kielimu, kwa kuwa kuhusika kwa wajumbe waliochaguliwa kulichukuliwa pakubwa kama kulikokosekana katika bunge lilichaguliwa mwaka wa 1999. Hata kama mfumo wa uchaguzi huchukuliwa tu kama usio mwafaka wa kisiasa bali kama jaribio muhimu la kuunganisha kanuno za mfumo wa PR na kuwajibika kwa wajumbe waliochaguliwa kwenye eneo la uchaguzi, hakuna hatua ya mjumbe kuungana na eneo bunge lake iliyojengwa.
Hata hivyo, visingizio vilivyotolewa baada ya chaguzi za mwaka wa 1999 kwamba mfumo wa wingi wa SMD ungetoa matokeo yasiyo na usawa nchini Indonesia kushinda ilivyokuwa katika sehemu nyingine duniani. Mahusiano yaliyoendelea kuharibika kabisa kati ya bunge lililochaguliwa mwaka 1999 na wadau wengi katika anga za usomi, vyombo vya habari na mashirika ya kutetea jamii pia yalieleza kuwa uungwaji mkono wa mifumo ya SMD na makundi haya haukuwezekana. Ilikuja kuwa wazi kwamba mfumo wa wingi bila shaka ungefeli kuonysha tofauti za raia wa Indonesia, na kwamba kuanzisha mchakato wa kutumia wilaya zinazokubalika kwa uchaguzi wa mwaka 2004 kungechukua muda na kusumbua kwa kiwango fulani, na kwamba mifumo ya wingi haikuelekea kuwapendelea wanawake.
Mfumo wa Uchaguzi wa mwaka 2004
Mahitaji mapya ya katiba yaliyokubaliwa katika mwaka 2002 yanasema kwamba washiriki katika uchaguzi kwenye bunge la chini (Bunge la Taifa) ni vyama vya kisiasa, hivyo basi kupunguza nafasi za mfumo wa uchaguzi katika sheria mpya ya uchaguzi. Muswada wa serikali wa sheria ya uchaguzi ulipendekeza mfumo wa PR kwa kutumia maeneo ya wapigakura wengi, hivyo kujibu shinikizo la uwajibikaji kwa kupendekeza orodha wazi na kugawa mikoa mikubwa. Umbo hili la kimsingi hatimaye lilichukuliwa, huku likiwa na maeneo ya wapigakura wengi, kati ya viti vitatu na 12 vilivyowekwa na Tume ya Uchaguzi. Mjadala uliofuata uliishia katika wilaya zenye kwapigakura wengi ambazo uwezo wake uliegemea pakubwa tofauti hii. Mfumo funge wa orodha wazi ulioidhinishwa hatimaye unawahitaji wapigakura kupigia kura chama kimoja na, wakipenda, mgombea mmoja kutoka kwenye chama hicho. Hata hivyo, hili litaishia tu katika uchaguzi wa mgombea fulani kutoka kwenye orodha iliyopo ambamo majina yanapatikana kwenye orodha ya chama ikiwa mgombea huyo anapata zaidi ya nusu ya idadi ya kura katika mfumo wa Hare – hali iliyofanya athari yake kuwa ndogo, inavyodhihirishwa na uchaguzi wa bunge wa mwaka 2004.
Kutokana na ujenzi wa bunge la kieneo, vyama vingine vilitaka kuwe na mfumo wa ‘mpigakura mmoja, kura moja, thamani moja’ (OPOVOV) kwa bunge, na idadi hiyo hiyo kwa kila kiti, huku wengine wakiunga mkono kudumishwa kwa mapendeleo ya uwakilishi katika Visiwa vya Outer. Mwafaka wa mwisho ni fomula changamano kutokana na idadi ya viti vya kila mkoa kwa idadi ya chii kabisa watu 325,000 kwa kila kiti katika mikoa midogo na idadi ya juu kabisa ya watu 425,000 kwa kila kiti katika ile mikubwa, huku kukiwa na idadi ya chini kabisa ya viti vitatu kwa kila mkoa.
Uongozi wa chama kikuu ulionyesha mapendeleo kidogo ili kulegeza msimamo wake kwenye vyama. Vyama vikubwa vilikaza mahitaji ya vyama kushiriki katika chaguzi za 2004 na nyingine andamizi.
Kukataliwa kwa vyama vya kieneo kumedhabitishwa. Maswala ya uwazi na ufunge wa orodha, OPOVOV, usawa kati Java na Visiwa vya Outer, na kushiriki kwa vyama yalijadiliwa yote kati ya vyama mwafaka wa mwisho ulipoafikiwa. Kampeni kubwa, hata hivyo, uliishia katika kuchukuliwa kwa ‘mfumo idadi’ kwa uwakilishi wa jinsia: vyama huhitajika kuzingatia haja ya kujumuisha angalau asilimia 30 ya wagombea wa kike kwenye orodha zao. Japo hakuna kanuni ya kuhakikisha kwamba hilo litekelezwa, hili lilidhihirika kuwa ala muhimu ya kuhimiza wagombea wengi wa kike, na asilimia 12 ya wabunge wa bunge la 2004 ni wanawake – nyongeza nzuri kutoka kwa ile ya 1999.
Matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2004 yalidhihirisha mabadiliko na maendeleo hayo yote. Vyama vivyo hivyo vitano vilivyoshinda zaidi ya asilimia 3 katika mwaka wa 1999 vilifanya hivyo tena, na viungana na vingine viwili zaidi. Kwa jumla vyama kumi na saba viliwakilishwa.
Kuchaguliwa kujiunga na Bunge la Eneo: SNTV Inashtusha
Katiba inaeleza kuwa wagombea wa bunge jipya la maeneo (Baraza la Wawakilishi wa Maeneo) wanapaswa kuwa watu, si vyama. Wajumbe wane wanapaswa kuchaguliwa katika kila mkoa. Muswada wa sheria ulipendekeza mfumo wa Upigaji Kura wa Bloku, ulioratibiwa kuvifaa vyama vilivyo na uungwaji mkono nje ya Java ambako mikoa ni midogo. SNTV ilipendekezwa kama njia mbadala ya chama kilichokuwa na nguvu nyingi katika Java, na ulikubaliwa kama sehemu ya mwafaka wa mwisho.
Uchaguzi wa kwanza kwenye bunge la kieneo ulifanyika katika mwaka 2004 na ulidhihirisha udhaifu fulani wa SNTV: huku jumla ya wagombea 30 waliowania viti vinne katika kila mkoa, wengi wao walichaguliwa na chini ya asilimia 10 ya kura. Hata hivyo, kampeni nzito za wagombea wa kike ziliashiria kwamba asilimia 21 isiyotarajiwa ya wajumbe wa bunge jipya ilikuwa wanawake – kiwango ambacho hakikutarajiwa katika shirika huru lililochaguliwa nchini Indonesia.
Chaguzi za Moja kwa Moja za Urais
Rais na makamu wake hivi sasa huchaguliwa moja kwa moja, huku wagombea wakiungana kutafuta tikiti hiyo. Mfumo wa awamu mbili za wapigakura wengi hutumiwa, na lengo la kuhakikisha kwamba wagombea wanaofaulu wanapata uungwaji mkono wa kutosha katika nchi nzima. Ili jozi hiyo (rais na makamu wake) ichaguliwe kwenye awamu ya kwanza, haipaswi kupigiwa kura tu na idadi kubwa ya kura zilizopigwa bali pia iafiki hitaji la kuenea kwa asilimia 20 ya kura katika angalau nusu ya mikoa. Japo mshindi wa kura nyingi anaweza kupata hili bila shaka, hitaji hilo huzuia jozi ambayo uungwaji wake mkono umejikita katika maeneo ya Java tu na kuwa mdogo katika sehemu nyingine kutokana na kushinda kura katika awamu ya kwanza. Katika uchaguzi wa kwanza wa mwaka 2004, jozi tano ziliwania nyadhifa katika awamu ya kwanza mwezi Julai, huku kukikosekana yoyote iliyopata zaidi ya asilimia 35; katika awamu ya pili mwezi wa Septemba, Susilo Bambang Yudhoyono alishinda kwa wingi wa kura kwa kupata asilimia 61 ya kura hizo.
Ukweli wa Kisiasa: Kuafikia kuhusu Migao
Makualiano kuhusu mfumo wa uchaguzi wa mwaka 1999 yalipaswa kukubaliwa na vyama vyote vya Mfumo Mpya, ambao ndio ulioshikilia mamlaka, na vyama vipya nje ya mtaa huo. Marekebisho ya katiba yaliyofuatia uchaguzi wa mwaka 1999 pia yalihitaji makubalinao katika anga zote za kisiasa. Sheria ya uchaguzi ya mwaka 2004 ndiyo mwafaka mwingine, iliyoshabihiana kabisa kikanuni na ile ya mwaka 1999, japo ikiwa na tofauti muhimu kuhusu maelezo. Kila wakati, kulikuwa na masuluhisho machache kutokana na mazoea na historia ya kisiasa ya wadau. Hata hivyo, kuna ishara chanya za demokrasia katika mfumo mpya wa kiasasi wa Indonesia: ni bahati nzuri kwamba maono mengine ya muda mrefu yalikuwepo pampja na mitazamo muhimu ya ubora mdogo wa kisiasa miongoni mwa vyama na watu walioleta mabadiliko hayo.