Bunge la chini la Ayalandi, Dáil Éireann, huchaguliwa na mfumo wa STV – uwakilishi sawa unamaanisha kwamba kuna Kura Moja Inayoweza Kuhamishwa. Mfumo huu usio wa kawaida unatokana na hali kupatikana kwa uhuru katika Jamhuri ya Ayalandi katika mwaka wa 1992. Viongozi wwaliokuwa wakiondoka, Waingereza, walitaka umbo fulani la PR ili kulinda Wapinzani waliokuwa wachache, ilhali wasomi wachache katika siasa za nchi hiyo walipendelea mfumo wa PR kikanuni.
Dáil ina umuhimu mkuu katika mfumo wa siasa za Ayalandi. Huchagua serkali, inayopaswa kudumisha umaarufu na uungwaji mkono wake katika Dáil ili iweze kuendelea kuwepo. Katika kiwango cha chini kabisa ni urais, ingawa, hali isiyo kawaida kwa mfumo wa bunge, rais huchaguliwa moja kwa moja. Uchaguzi wa rais hufanyika chini ya mfumo wa Kura Mbadala (AV).
Wajumbe 166 wa Dáil huchaguliwa ‘kutoka kwenye maeneo bunge 40, kila mojawapo watatu, wanne au watano. Upigaji kura ni wa wazi: wapigakura huashiria tu mgombea wao mpendelewa (kwa kuandika ‘1’ kando ya jina la mgombea huyo kwenye karatasi ya kura), na wanaweza kuendelea kwa kuonyesha teuo lao la pili, tatu na kadhalika. Wapigakura wanaweza kuwapanga wagombea sio tu ndani ya vyama bali pia katika vyama vyote. Ingawa wengi hupiga kura kwa misingi ya vyama, si muhimu kufanya hivyo, na wengine hupiga kwa misingi ya maeneo ya kijiografia, yaani, hupendelea pakubwa, bila ya kujali chama, wagombea wanaotoka katika maeneo yao. Mchakato wa kuhesabu, hasa kusambazwa kwa kura za ziada, huonekana kuwa mgumu kwa kundi ambalo halikuanzisha, lakini ni muhimu kusisitiza kwamba si lazima wapigakura wafahamu maelezo yote; wanahitaji tu kujua jinsiya kupiga kura zao na kuridhika kwamba shughuli ya kuhesabu ilikuwa huru na wazi.
Mfumo hwa uchaguzi umeingizwa katika katiba na hivyo basi hauwezi kubadilishwa bila kura ya maamuzi. Mara mbili hivi (1959 na 1968) chama kikubwa, Fianna Fáil, kilichochea kufanyika kwa kura ya maamuzi kubadilisha mfumo wa STV na ule Uingereza wa FPTP, kwa kutumia mtazamo kila mara kwamba aina yoyote ya PR ingezua tatizo la serikali ya muungano kukosa udhabiti. Mabadiliko yaliyokuwa yamependekezwa yalikataliwa na wapigakura kila mara, kwa tofauti kati ya asilimia 52 dhidi ya 48 katika mwaka wa 1959, na 61 dhidi ya 39 katika mwaka 1968.
Kwa misingi ya mbinu ya kuwa serikali imara, yeyote anayetathmini rekodi ya STV katika Jamhuri ya Ayalandi hataweza, kwa hakika, kuona utendakazi wake kama shida. Kuanzia miaka ya 1940, serikali (za miungano na chama kimoja) zimedumu kwa miaka mitatu, minne au mitano, tofauti ikiwa kipindi kifupi cha kukosa usalama mapema miaka ya 1980. Wapigakura, kupitia kwa upangaji wa wagombea wa vyama mbalimbali katika nambari, huweza kuonyesha mapendekezo yao kuhusu washirika wanaoweza kuunda muungano kwa manufaa ya chama wanachopendelea.
Mfumo wa STV kwa jumla umetoa matokeo yenye viwango vya juu vya usawa, huku Fianna Fáil, kikipokea bonsai (takribani asilimia 48 ya viti kwa asilimia 45 ya kura katika uchaguzi katika kipindi cha kati ya 1945 -92). Hata hivyo, idadi ndogo ya wilaya za uchaguzi (viti vinne kwa kila eneo bunge kwa jumla) hujenga uwezekano wa chama kikubwa kuvuna ikiwa kinaweza kuvutia kura za mapendeleo ya pili na tatu kutoka kwa wafuasi wa vyama vingine. Katika matokeo yaliyowahi kuonyesha kukosekana kwa usawa katika mwaka 2002, Fianna Fáil kilishinda asilimia 41 ya kura na asilimia 49 ya viti.
Mfumo huo unaendelea kuruhusu uwakilishi kwenye vyama vidogo na wagombea huru, ambao 13 katika hawa walichaguliwa mwaka 2002. Ingawa mifumo ningi a PR huviwezesha vyama vidogo kushinda viti Bungeni, mfumo wa STV unaonekana kuwapa wagombea huru nafasi ya kipekee kufanya hivyo kutokana na hali yaka ya kuegemea wagombea binafsi kuliko chama.
Sifa na kashifa nyingi za mfumo wa STV katika Jamhuri ya Ayalandi hutokana na kipengele hicho kimoja, ambacho ni mamlaka ambayo hutoa kwa wapigakura kuchagua miongoni mwa wagombea wa chama kimoja. Hili hujenga ushindani katika vyama, hasa miongoni mwa wagombea wa Fianna Fáil, ambacho huteua kati ya wagombea wawili na wane katika kila eneo bunge. Takwimu zinaonyesha kwamba Wabunge wengi waliopo wa chama cha Fianna Fáil hupteza viti kwa wale wanaowafuata kuliko wanavyofanya kwa mgombea wa chama kingine.
Wahakiki wanashikilia kwamba, kwa sababu hiyo, wagombea waliopo huchangamka katika kiwango cha eneo bunge ili kupendelewa na wapigakura na hawatumii muda wa kutosha kwenye siasa za kiwango cha taifa, kwa mfano, kuhusu kuchunguza serikali au kujadili sheria katika kamati. Wao hushikilia kwamba hili lina athari kwenye hadhi ya wabunge wa Ayalandi (hivi kwamba watu ambao wangechangia katika kiwango cha taifa wanatatizwa na mzigo ambao wanapaswa kushughulikia wakichaguliwa) na kwamba huishia katika mihula mifupi na ueneo katika fikra zao. Wao hupendekeza kwamba ushindani katika chama ili kupata unaweza kusababisha kugawanyika, kutodhabitika kwa vyama vya kisiasa.
Watetezi wa mfumo huo, kwa upande mwingine, huona nafasi ya wapigakura kuchagua miongoni mwa wagombea wa chama chao kama inayostahili. Wao hutetea kwamba inawaruhusu kubadilisha viongozi waliopo na wengine walio na uwezo mkubwa na wanaowajibika na kwamba, wakati wa kupunguza ari katika siasa za miungano, hili huwapa wabunge shughuli nzito ya kuwa na mawasiliano ya karibu na wapigakura na hivyo kutimiza wajibu wa kuwaunganisha wapigakura na mfumo wa uchaguzi. Wao hushikilia kuwa hakuna ushahidi kwamba wabunge wa Ayalandi ni wa hadhi ya chini kuliko wale walio katika maeneo mengine na kwamba rekodi za hivi majuzi za makuzi lya kiuchumi ya Jamhuri ya Ayalandi yanaonyesha kwamba hakuwezi kuwa na makosa mengi katika mwenendo wa serikali. Wao pia hutaja kuwa vyama vya kisiasa vya Ayalandi vimeungana na vina nidhamu katika mwenendo wake Bungeni, bila mirengo au makundi maalumu.
Katika mwaka 2002 kamati ya vyama vyote iliangazia hoja za watu za kuunga na zile za kupinga mabadiliko ya mfumo huo. Ilihitimisha kwamba umma ulikuwa umependa kabisa mfumo wa STV, na kwamba mabadiliko ya kuingia katika mfumo wowote ule yangepunguza mamlaka ya mpigakura binafsi, na kwamba udhaifu mwingine uliokuwa umetajwa wa mfumo huo wa uchaguzi ambao wahakiki walilaumu mfumo wa STV ulisababishwa na vipengele kadha wa kadha. Kama hitimisho hilo linavyoashiria, hakuna maoni maalumu ya kuunga mabadiliko au kubadilisha mfumo uliopo.
Tathmini yoyote ya mfumo wa STV katika Jamhuri ya Ayalandi inahitaji kuzingatia sifa za nchi hiyo. Ni nchi ndogo kwa misingi ya upana wa eneo na idadi ya watu, na idadi ya wabunge ikilinganishwa na idadi ya watu (takribani 1: 20,000) ni kubwa katika viwango vyote vya kimataifa. Hili linaweza kusababisha uhusiano wa karobu kati ya wabunge na wawakilishwa wao, mighairi ya mfumo wa uchaguzi, kuliko inavyowezekana katika nchi kubwa. Isitoshe, Jamhuri ya Aayalandi ina matokeo mazuri, ni jamii yenye wasomi wengi ambapo mfumo wa uchaguzi kwa jumla umejengwa vikamilifu na unachukuliwa kwa jumla kama halali. Jamii ya Ayalandi haina tofauti zozote (kwa mfano, kikabila, kilugha au kidini).
Kwa sababu hizi tunahitaji kuwa waangalifu kuhusu kuweka mahitimisho kuhusu jinsi mfumo wa STV utakavyoendeshwa katika mazingira mengine. Tunaweza hata hivyo, kusema kwamba hakuna dalili yoyote kwamba wapigakura katika Jamhuri ya Ayalandi wangependelea kuubadilisha mfumo huu na mwingine wowote.