Orodha ya Mifumo ya Uchaguzi
Zoezi la Mifumo ya Uchaguzi
Mada hii ya Mifumo ya Uchaguzi inashughulikia mpangilio, mikakati, na athari za kuwepo kwa mifumo mbalimbali ya uchaguzi katika viwango vya kitaifa, kijamii na kimataifa.
Itatambulisha, kueleza na kuainisha mifumo 12 ya uchaguzi na kujadili mahusiano yake na miundo mikubwa ya kitaasisi pamoja na athari zake kwenye maswala ya kiutawala na pia itaangazia masuala mahususi yanayohusiana na mabadiliko ya mchakato wa mifumo ya uchaguzi.
Hali kadhalika, michango na mielekeo ya demokrasia ya moja kwa moja itashughulikiwa katika sehemu hii.
Ili kupata habari zaidi kuhusu yaliyomo katika sehemu hii, tazama sehemu zinazotoa muhtasari, kanuni elekezi na yaliyomo kuhusu mifumo ya uchaguzi.

