ACE
Encyclopaedia   Mada   Mfumo wa Kisheria  
Mfumo wa Kisheria

Kielelezo cha Mfumo wa Kisheria

Lengo letu hapa ni kuchanganua, kwa mtazamo wa kulinganisha, mambo maalumu yanayohusiana na kanuni za kiusimamizi na za kisheria zinazoweza kuonekana kuwa muhimu sana katika kuwepo kwa uchaguzi unaokusudia kuwa wa haki na usawa.

Tunajaribu kujenga vibadala vingi tofauti tofauti vinavyoweza kuzingatiwa katika kujenga au kuunda upya mfumo wa kisheria utakaosaidia katika uchaguzi. Juhudi kama hii hufanikishwa kwa kutoa taarifa ya kina na yenye mpangilio kwa wataalamu hao wanaohusika katika kuendesha uchaguzi kwa mujibu wa vibadala vilivyopo.

Azma yetu ni kumsaidia msomaji yeyote yule kuelewa maana hasa ya mfumo wa kisheria. Ili kufanya hivyo, mifumo tofauti tofauti ya uchaguzi, vibadala mbinu mbalimbali za kimsingi zinazoweza kutumiwa kuendeshea uchaguzi, vyombo tofauti tofauti vya kisheria ambavyo hutumika kuunda kanuni za uchaguzi na sifa za bainishi za kanuni hizi huangaziwa.

Tukitilia haya yote maanani, maswali haya matatu muhimu hushughulikiwa katika njia zifuatazo:

  • Ni vipengee vipi ambavyo sharti vitiliwe maanani ili kufafanua au kurekebisha kanuni ya uchaguzi?
  • Ni vipengee vipi vya kimahakama ambavyo vinapaswa kuhusishwa katika mfumo huo wa kisheria?
  • Ni sifa zipi za kimsingi zinazotambulisha uchaguzi ulioboreshwa?