Mpango wa kisheria, marekebisho na utekelezaji wa mfumo wa kisiasa, uwe ni wa kimataifa au kimaeneo (Muungano wa Ulaya au Bunge la Marekani ya Kati) kitaifa, (ya kila nchi), serikali, huru, kiidara, kimanispaa, Kikantoni ama ya jimbo haiwezi kupuuza miktadha ya kitamaduni, kiuchumi, kisheria, kijamii na kisiasa ambapo shughuli za uchaguzi na asasi ambazo zipo na wala si desturi inayopendwa.Yaani kutumika na kufafanuliwa kikatiba, kisheria lazima ziafikiane na muktadha. Muktadha wa mfumo wa uchaguzi haujaundwa kutokana na vipengee visivyo na uhusiano bali umeundwa na ufanya kazi na athari za mfumo wenyewe na vipengee vinavyohusiana.
Hakuna umbo la uchaguzi lisilo na kifani ama lisilo na dosari lakini mifumo tofauti ya uchaguzi hutumiwa kufanikisha malengo yaliyowekwa na raia na washika dau wa kisiasa wakati namahali palipotambulishwa. Mfumo utakuwa wa kutosheleza pale ambapo unaweza kukimu maendeleo ya kidemokrasia ya jamii ambamo utatumika au pale ambapo inawezesha jamii kufikia demokrasia au kuimarisha demokrasia yenyewe.
Ingawa utaratibu huo unaweza kuchochea matokeo fulani, kama vile uundaji wa wengi kirahisi au inaweza kuonyesha kwa uhalisi kuwepo kwa makundi tofauti ya kisiasa, ukweli ni kwamba vipengele ambavyo ni muhimu vinavyotokana na vipengele vya kiufundi vya uchaguzi ni vile ambavyo vinaridhisha kuwepo kwa wengi. Vipengele hivi vinaweza kuwa ukubwa wa baraza la kutunga sheria, tofauti zilizoko kati ya vyama vya kisiasa na kuundwa kwa ushirikiano, makazi tofauti ya kijiografia ya walio na sifa za kupiga kura, mapatano au maafikiano ya uchaguzi na kadhalika.
Mradi shirikishi na wawakilishi wa kiemokrasia, ambao unawezekana kisiasa na unaaminika lazima ushughulikie na hata kutimiza matarajio na mitazamo ya kisiasa ya kila mmoja wa washikadau (wananchi, vyama vya kisiasa, mashirika ya wananchi, makundi ya watetezi na kadhalika) licha ya sadfa muungano na kukaribia au hata kuja pamoja kwa mambo hayo katika mada kadhaa za ajenda ya kisiasa. Mifumo ya kisiasa ni zao la makubaliano ya kisiasa. Hizi ndizo njia ambazo mkusanyiko wa matakwa ya vyama vya kisiasa hudhihirishwa. Matakwa hayo hayatapuuzwa na wanaoendesha mahakama ila tu pale ambapo yanapinga kuwepo kwa uchaguzi huru na wa kweli kama itakavyoelezwa zaidi.
Chaguo la kielelezo thabiti cha uchaguzi (dhahiri au isio dhahiri) kukuzwa kwake (mfumo wa wengi, uwakilishi kwa kurejelea idadi, au mchanganyiko au vijisehemu) na sifa zake au kuchanganya vipengee (sahili, kamili au wengi waliohitimu, uwakilishi kiuwiano dhahiri ama usio dhahiri na kishazi cha kiserikali) lazima iwe uamuzi unaotegemea idhini au wengi. Licha ya hayo ukubalifu wa wengi ama kwa upana tu hakutawafungia nje uwezekano wa kuwakilishwa wa wachache ama sauti ya kitengo cha serikali kama inavyo tokea katika bunge ama baraza za kisheria vilevile katika sehemu za utawala na usimamizi (mabaraza ya miji).
Ili kuzuia mifumo ya uchaguzi kuwa ya kinatharia, isiyotosheleza ama isiyofanya kazi, makubaliano ya kisiasa, muktadha wa kijamii na vipengee vya mazingira ni muhimu. Hata hivyo, vipengele hivyo haviwezi kuangamiza au kufutilia mbali kanuni zinazounga shughuli ya uchaguzi iliyo huru na yenye usawa. Haki ya binadamu ya kushiriki moja kwa moja au kisiri, kusherehekewa kwa kura ya kweli na ya mara kwa mara, ya watu wote, ya siri nahaki sawa ya kupiga kura, hkuheshimika kwa haki za binadamu, kutopendelea kwa wasimamizi wa uchaguzi kuhusu idara za serikali na washikadau wa kisiasa na sheria za kudhibiti kuweko kwa sheria za uchaguzi.