Mfumo wa kisheria huwa muhimu kila mara. Kanuni za kisheria ni za lazima na
hudhibitisha jinsi mfumo wa uchaguzi unavyofanya kazi. Mbinu za kisheria
huwezesha shughuli za uchaguzi kwa usalama na hakika.
Katika utawala wa kidemokrasia na kikatiba, masuala ya uchaguzi hudhibitiwa
kisheria na sheria tofauti zinazotokana na kanuni za kimsingi ama na katiba.
Vyombo hivyo ni pamoja na:
- Katiba: ni
kanuni za kimsingi na za lazima ambazo hutokana na mfumo wa kisheria wa
nchi. Katiba hutoa kanuni za kimsingi ambazo huongoza jinsi nchi na
serikali imepangwa, kwa haki za kimsingi ambazo zitafuatwa, kwa kanuni
zinazoongoza mfumo wa uchaguzi, kwa masharti ambayo ni sharti mtu
ayatimize ili awe raia, kwa kuwepo kwa vyama vya kisiasa, viongozi wa
uchaguzi wenye mamlaka na korti za uchaguzi na masuala ya taratibu.Kanuni
za kikatiba ndio kanuni za juu katika mfumo wa kisheria; haziwezi
kubadilishwa kwa urahisi na hukaa kwa muda mrefu kuliko nyingine.
- Mikataba
ya kimataifa: Mikataba ya kimataifa hukuza haki za kimsingi,hasa zile
zinazohusiana na kujihusisha katika uchaguzi na upigaji kura.
- Sheria za
uchaguzi: sheria za uchaguzi huwekwa na baraza. Baraza nyingi ulimwenguni
huwakilisha matakwa ya watu. Kanuni nyingi za uchaguzi zinapatikana katika
sheria za uchaguzi. Huwa zinaweza kurekebishwa kuliko sheria za kikatiba
na ni muhimu kushughulikia mada za uchaguzi vyema.
- Vigezo vya
kimahakama: Ni maamuzi amahukumu zinazotolewa na majaji na korti ili
kutatua mizozo ya kiuchaguzi. Siku hizi zimefikia hadhi ya juu kwa sababu
ya nafasi ya majaji na korti katika maisha ya nchi.
- Amri za
kutoa uamuzi za mamlaka ya uchaguzi: Hutolewa na viongozi wa kiutawala ili
kupa nguvu kanuni za kisheria na kikatiba.
- Kanuni za
kuongoza tabia: hizi ni kanuni zilizokubaliwa na maajenti wa kisiasa.
Kanuni za tabia huazimia kuwezesha tabia za heshima, kufuata amri na
ustaarabu wakati wa uchaguzi. Marefa ndio hupewa jukumu la kuzipa nguvu.