Wataalamu
hujadili iwapo katiba na mikataba ya kimataifa ni lazima ichukuliwe ka ma
kanuni za juu katika mfumo wowota wa kisheria. Hata hivyo, maafikiano
yamefikiwa kulingana na mada nyingine zilizoko katika mikataba ya
kimataifa, kama vile kulinda haki za kibinadamu (pamoja na ya kisiasa na
upigaji kura ambazo ni sehemu ya zile haki za kizazi cha pili) lazima
zijumuishwe katika mfumo wa kisheria wa nchi yoyote, ama nchi hiyo itaonekana
kama ambayo si ya kikatiba ama kidemokrasia.
Mikataba ya
kimataifa ambayo ni ya lazima sasa kwa nchi nyingi zinapendekeza kuimarishwa
kwa haki za kisiasa na kiuchaguzi. Miongoni mwa mikataba hiyo inaweza
kuainishwa kama: Mwafaka Bia Kuhusu Haki za Binadamu, Msimamo wa Marekani
Kuhusu na Majukumu ya Mwanamume, Makubaliano ya Kimataifa Kuhusu Haki za
Kisiasa na za Raia, Mwafaka wa Marekani Kuhusu Haki za Binadamu (yanayojulikana
pia kama Makubaliano ya San Jose), na Makubaliano kuhusu Haki za Kisiasa za
Wanawake.
Makala za
kimataifa ni chanzo cha sheria ya uchaguzi. Haiwezekani kudunisha idadi kubwa
ya mikataba ya kimataifa, maamuzi, chati, maazimio na ripoti zinazohusiana na
haki za binadamu kijumla na hasa za kisiasa. Kanuni nyingi muhimu zinatoka kwa
makala za kimataifa. Kwa mfano kila nchi ya kidemokrasia ni lazima ipige kura
ili kuteua wawakilishi wake. Kwa mtazamo huu, makala za kimataifa hudhihirisha
umuhimu wa wachunguzi wa kimataifa katika shughuli ya uchaguzi.
Makala za
kimataifa hutawaliwa na kanuni spesheli za korti za kimataifa. Licha ya hiyo
mikataba hasa ni lazima zichukuliwe na katiba za kitaifa. Katiba za kitaifa
lazima zichukulie mikataba ya kimataifa kama inayozua sheria za kitaifa, kama
kanuni za juu, kama kanuni za lazima. Sheria za kawaida na kanuni lazima
zieleze habari na masuala ya taratibu zilizowekwa na mikataba ya kimataifa.
Kulingana na
kanuni nyingine zinazotokana na makubaliano ya Vienna ya sheria za mikataba
(1969) kuna kanuni tatu zinazoshughulikia mada hii: a) Kila mkataba hudhibiti
nchi zinazoafikiana nao; b) hakuna nchi inayoweza kudhibitiwa na mkataba ambao
haijaukubali; na c) majukumu yanayotolewa yanatokana na idhini ya serikali.
Mikataba ya
kimataifa ni muhimu ulimwenguni kiasi cha kwamba ni vigumu kufikiria kanuni ya
taifa ama kanuni ya kikatiba (hasa katika suala la haki za kisiasa na kupiga
kura) inayoweza kuzipinga. Nchi zinazoongozwa kwa kuzingatia demokrasia za
kikatiba hukubali na kutumia makala za kimataifa katika mfumo wao wa kisheria.