Msemo kanuni za maadili meme inaweza kurejelea vitu vingi.
Hivyo basi, ni vyema kuondoa hali tatu za msemo huo mwanzoni. Hali hizo tatu
zinaathiri siyo tu mawakala wa uchaguzi bali pia jinsi ya kuendesha uchaguzi na
haiwezi kuonekana kama kanuni za maadili mema zilizohusishwa katika shughuli za
uchaguzi:
- Kwa jumla,
kanuni za usimamizi wa uchaguzi haziwezi kuchukuliwa kama kanuni za
maadili mema. Hivyo basi ni rahisi kutofautisha kanuni za maadili mema kwa
jumla kama zile zinazowatawala viongozi wa Australia na zile kanuni
za kipekee zinazowalenga watu binafsi kama nyingi zilizowekwa na
mashirika ya kimataifa (wachunguzi wa uchaguzi). Tunazungumzia kanuni
ambazo zinaazimia kuweka tabia zisizo na ubaguzi kwa watu au mashirika yanayosimamia
uchaguzi. Kanuni kama hizo zinaweza kutazamwa kama za kiusimamizi, sawa na
zilizowekwa na viongozi wa umma ama mashirika ya wataalamu.
- Kanuni za
jumla zilizobuniwa na vyama vya kisiasa haziwezi kuchukuliwa kama kanuni
za maadili vilevile. Kanuni hizi si za lazima kwa vyama vingine bali tu ni
kwa wanachama wake.
- Kanuni
zilizodokezwa za ubora wa uchaguzi zilizoko katika tawala za kidemokrasia
haziwezi kuchukuliwa kama kanuni za maadili. Kanuni hizi zimewekwa
kulingana na masuala mahsusi ambayo hayatajadiliwa na wagombeaji. Kanuni
hizi za kudokezwa za ubora wa uchaguzi si dhahiri ama wazi.
Ni sifa zipi ambazo zinadhihirisha kanuni za kimaadili za uchaguzi? Kwa
mtazamo wetu zipo kanuni angalau mbili na ni zifuatazo:
- Kanuni ya
kimaadili ni zao la mapatano yanayofikiwa na vyama vya kisiasa.Mapatano
hayo yanaweza kuwepo kwa zaidi ya uchaguzi mmoja.
- Kanuni za
kimaadili hunuia kuzikamilisha kanuni za kisiasa. Hii ndiyo sababu zina
jukumu muhimu katika uchaguzi wa mpito. Azma yao kuu ni ya uwili. Kwa
upande mmoja, zinanuia kufikia ukuzaji wa amani katika uchaguzi. Kwa
upande mwingine, zinanuia kukataza matendo ya vikundi vyenye mamlaka
kutumia mamlaka vibaya.
Kuna tofauti nyingi zinazosababisha tofauti ya hizi mbili. Tofauti kama hizi
zinatokana na sifa bainifu za majukumu yanayotokana nazo yalivyo.
Vyama vya kisiasa vinaweza kuweka kanuni za maadili zinazoweza kuhusisha
mashirika ya kimataifa miongoni mwa waliozipigia sahihi. Kanuni haziwezi
kupendekezwa na viongozi wa uchaguzi.
Kwa sababu kanuni za maadili hupendekezwa na mamlaka ya chaguzi huwa na
changamoto kuu ambayo inaweza kuelezewa ifuatavyo: kanuni za kimaadili ni za
lazima? Kwa mtazamo wa kuzua madai kanuni za kimaadili zinaweza kuwa za hiari.
Licha ya hayo, tunaweza kuzua mawazo kutoka kwa utafiti:
- Nchi
nyingine zimejumuisha mawazo ya kanuni za kimaadili katika sheria za
uchaguzi zilizowekwa na bunge. Hapa majadiliano lazima yaanze kutoka kwa
mtazamo tofauti: Inawezekana bado kuzungumzia kanuni za maadili?
- Uchangamano
mwingine unatokana na hali ambazo kanuni za kimaadili hukubalika kabisa na
wagombeaji na kutoa adhabu zinazostahili kutumiwa kwa yeyote anayekosa
kuzifuata. Katika hali kama hii kanuni za kimaadili zinapata hadhi ya
kawaida.
Kanuni nyingi za maadili zimekubalika japo hazina adhabu yoyote iwapo mtu hatazitii.Hali
kama hii inaweza kuchuuukuliwa kama kufungamanisha sehemu ya kawaida ya
taratibu za uchaguzi.Hata hivyo lazima tukiri kwamba kanuni nzuri za kikatiba
hudhibiti masuala muhimu sana na huwa za lazima.
Kuhusiana na kanuni za kimaadili tunaweza kusema kuwa ni kanuni zinazonuia:
- Kudhibiti
kuwatisha raia na vita;
- Kuweka
kanuni za kuendesha kampeni;
- Kudhibiti
tabia yoyote ya kukiuka kanuni ya vyama vya kisiasa.
Kanuni nyingi za maadili huleta muungano kati ya viongozi wa uchaguzi na
kufanya mikuatano ya mara kwa mara. Hata hivyo, hazivipi vyama vya kisiasa
mamlaka ya kuzifafanua ama kuzitekeleza.