Maeneo ya uchaguzi lazima yabainishwe ili yachunguzwe kwa mtazamo wa kisheria. Eneo la kiuchaguzi hivyo basi ni eneo ambamo upigaji kura kubainisha jinsi viti vya bunge vitakavyogawanywa kati ya wagombeaji na vyama vya siasa.
Mipaka ya maeneo ya uchaguzi haina umuhimu sawa katika mifumo yote ya uchaguzi. Kwa baadhi ya mifumo hii, kugawanya viti vya bunge kunaweza kuonekana kuwa muhimu sana na kama uamuzi ulioafikiwa baada ya kujadiliwa kisiasa. Katika nchi nyingi kugeuza kura kuwa kiti cha bunge kunaweza kuleta tofauti kubwa kwa uwiano wa kisiasa katika taifa husika.
Mfumo wa kisheria unapaswa kuzuia aina yoyote ya hila zinazoweza kufanywa katika mpangilio wa mfumo wa uchaguzi. Kila kura ina umuhimu kama nyingine.
Mifumo ya kisheria lazima ipange jinsi maeneo a uchaguzi yatakavyopangwa na kubainishwa. Maeneo pana ya uchaguzi lazima zionekane kuunga uwakilishi wa kisiasa. Taratibu za kisheria zijibu maswali muhimb ambayo ni kama yafuatayo: ni mara ngapi na katika hali gani, mipaka ya maeneo pana ya uchaguzi yatapangwa upya; mchango wa matawi ya asili ya serikali na asasi huru utakuwa upi katika kufanya hivyo; na ni nani atakayetoa uamuzi.
Kuna njia tofauti tofauti za kuweka mipaka katika wilaya za uchaguzi. Kwa kuwa shughuli hii inaweza kuonekana kuwa muhimu kwa mtazamo wa kisiasa, nchi nyingi huondoa halmashauri za kusimamia uchaguzi zisizo huru katika kazi hii. Kwa kawaida, mchakato huo mzima huwekwa mikononi mwa tume maalumu inayosaidiwa na halmashauri za kusimamia uchaguzi kwa mtazamo wa kiufundi. Tume hizi maalumu hujumuishwa kwa njia tofauti: zinaweza kuhusisha vyama vya kisiasa, wananchi wasioegemea upande wowote, wataalamu kama vile wanaohusika na hesabu ya watu.
Mfumo wa uchaguzi kwa kawaida hunuia kugeuza nia ya umma kupiga kura katika serikali ya uwakilishi. Hivyo basi, kuweka mipaka kwa kila wilaya ya uchaguzi kunaweza kuleta matokeo tofauti katika nchi tofauti, ingawa ni lazima kanuni za kimsingi zizingatiwe kila mara. Kulingana na viwango vya kimataifa, kila kura lazima iwe na thamani kama nyingine yoyote ili kuchagua uwakilishi mwema.
Sasa, kuweka mipaka hakutatuliwi kwa njia sawa katika nchi zote. Hata hivyo, kuna kanuni tatu za kimataifa zinazoongoza shughuli hii kila mahali. Kanuni hizi zinaweza kuorodheshwa ifuatavyo: uwakilishi, kuthaminiwa kwa kura zote, kutobagua.
Mipaka ya kubainisha wilaya za uchaguzi lazima iwekwe kwa njia ambayo mwishowe, wapigakura watawaona waliochuguliwa kama washindi wa kweli. Kwa kawaida, matakwa kama haya humaanisha wilaya za uchaguzi lazima zikimu mahitaji ya jamii kadhaa yaani; maeneo ya kiserikali, jamii za kimbari, jumuia mbalimbali kwa misingi ya rangi, maeneo ya kijiografia (kama vile visiwa) yanayodhibitiwa na mipaka ya kiasili.
Kwa mtazamo wa kimuundo, kuweka mipaka ya wilaya za uchaguzi kunaungwa na amri ya katiba za ulimwengu: kila kura ina thamani kama nyingine yoyote ile. Agizo kama hilo la kikatiba hugeuza kila kura kuwa ya kutoa uamuzi ili kuunda mashirika ya uwakilishi. Kanuni kama hizo haziwezi kudhiditiwa na mawazo ya kimaeneo; badala yake, kila wilaya ya kiuchaguzi lazima iwakilishwe na wabunge wengi kadiri matarajio ya idadi yake ya watu yanavyohitaji (uwakilishi wa kiuwiano) au na wawakilishi wengi kama kila wilaya nyingine ya kiuchaguzi inavyowakilishwa (uwakilishi dhahiri).
Mipaka ya wilaya za uchaguzi lazima iwekwe kwa kutumia taratibu wazi na za kisheria. Hapa kanuni zinapaswa kutupa hakika nyingi iwezekanavyo.
Kuwekwa kwa wilaya za uchaguzi kuna athari za kiusimamizi vilevile. Athari hizi lazima zishughulikiwe na halmashauri za kusimamia uchaguzi zinazoendesha usimamizi wa uchaguzi kwa sababu zitalazimika kubadili miundo yake ili kuafiki maeneo ya uchaguzi.
Ni muhimu kuangazia kuwa, pindi wilaya maalumu za uchaguzi zikiwekwa, maeneo hayo hayawekwi nje. Siasa ya kimaeneo hushurutisha uwekwaji wa mipaka ya kudumu ya wilaya hizi za uchaguzi.