Sifa ya kimsingi ya sheria za uchaguzi ni jinsi zinavyodhibiti shughuli za vyama vya kisiasa na wagombeaji. Udhibiti wa vyama vya kisiasa na wagombeaji ni muhimu kwa mfumo wowote wa uchaguzi.
Vyama vya kisiasa vinaweza kujihusisha ama kivyao ama kwa kuhusiana na vingine. Wakati mwingine wagombeaji huru huwania mbalimbali kivyao. Nchi nyingine huruhusu kuwepo kwa mashirika mengine ya kisiasa pamoja na miungano ya watu binafsi ili kujihusisha katika uchaguzi ama kwa pekee yao ama kwa ushirika na vyama vya kijadi (kama inavyotukia Meksiko). Hata hivyo, hali ilivyo kwa sasa inadokeza kwamba demokrasia inayotokana na kuwepo kwa vyama vya kisiasa, jukumu linalotekelezwa na mashirika hayo na uhusiano wao na mashirika mengine ni muhimu.
Kudhibitiwa kwa shughuli za vyama vya kisiasa na wagombea katika mchakato wa uchaguzi hasa kuhusiana na uteuzi wa wagombea na kampeni za kiuchaguzi, ni kipengele muhimu sana kwa mfumo wowote wa uchaguzi. Kwanza, sheria za uchaguzi zinapaswa kutambua anayeshughulika na hali ambamo wanapaswa kufanya kazi. Mara nyingi, mada kama hizo hudhibitiwa na Katiba (haki ya kimsingi ya kupigiwa kura imejumuishwa). Hata hivyo, katika nchi nyingine kanuni za kimsingi zinatolewa na sheria. La muhimu hata hivyo, ni kuangazia kuwa kila suala la mashirika na vyama vya kisiasa vinadhibitiwa. Kanuni kama hii lazima ifanye kazi ya kutosha ili kujumuisha mfumo wa utawala unaofadhili, haki na majukumu ya wanachama, uhisiano kati ya mashirika hayo na wagombea, na ushiriki katika uchaguzi, miongoni mwa mambo mengine.