Kielelezo cha Mfumo wa Kisheria
Lengo letu hapa ni kuchanganua, kwa mtazamo wa kulinganisha, mambo maalumu yanayohusiana na kanuni za kiusimamizi na za kisheria zinazoweza kuonekana kuwa muhimu sana katika kuwepo kwa uchaguzi unaokusudia kuwa wa haki na usawa.
Tunajaribu kujenga vibadala vingi tofauti tofauti vinavyoweza kuzingatiwa katika kujenga au kuunda upya mfumo wa kisheria utakaosaidia katika uchaguzi. Juhudi kama hii hufanikishwa kwa kutoa taarifa ya kina na yenye mpangilio kwa wataalamu hao wanaohusika katika kuendesha uchaguzi kwa mujibu wa vibadala vilivyopo.
Azma yetu ni kumsaidia msomaji yeyote yule kuelewa maana hasa ya mfumo wa kisheria. Ili kufanya hivyo, mifumo tofauti tofauti ya uchaguzi, vibadala mbinu mbalimbali za kimsingi zinazoweza kutumiwa kuendeshea uchaguzi, vyombo tofauti tofauti vya kisheria ambavyo hutumika kuunda kanuni za uchaguzi na sifa za bainishi za kanuni hizi huangaziwa.
Tukitilia haya yote maanani, maswali haya matatu muhimu hushughulikiwa katika njia zifuatazo:
- Ni vipengee vipi ambavyo sharti vitiliwe maanani ili kufafanua au kurekebisha kanuni ya uchaguzi?
- Ni vipengee vipi vya kimahakama ambavyo vinapaswa kuhusishwa katika mfumo huo wa kisheria?
- Ni sifa zipi za kimsingi zinazotambulisha uchaguzi ulioboreshwa?
Legal framework
The important components of law are the procedure,regulatory body(s),executing/implementing agency(s)and legitimacy.Law should be clearly defined and reforms should be made so as to cover all aspects.
Judicial decisions are always taken to formulate the process.So
important components are to be included from time to time keeping in view the needs of time.
Determination of seats,delimitations of boundaries, eligibility of voters and contestants etc are the basic features of reforms.