Utandawazi katika maisha ya kisiasa, kibinafsi, na kitaaluma, usambazaji wa demokrasia duniani kote na ongezeko katika uhamiaji yote yamechangia katika ongezeko la haki za Upigaji Kura kwa wakimbizi, wanadiplomasia, wanajeshi wanaohudumu nchi za Ngambo ambao wako Ngambo ya nchi yao kwa muda au daima. Uwezo wa watu hawa kutumia haki yao ya Upigaji Kura wakati uchaguzi unapofanyika katika nchi za kwao limekuwa jambo la muda mrefu katika upangaji na usimamizi wa uchaguzi.
Kwa kuwa idadi ya nchi zinazotekeleza uchaguzi wa kidemokrasia zimeongezeka, hata hivyo, umekuwa muhimu sana. Si kwamba tu watu wengi zaidi wanasafiri na kufanya kazi duniani kote. Uchaguzi unapofanywa katika nchi ambapo uongozi wa kidikteta umebadilika, na hata zaidi baada ya ghasia za kivita, haki za wakimbizi na watu wanaoishi Ngambo ya nchi kushiriki katika kujenga siku za usoni za nchi hiyo zimekuwa muhimu sana. Wakati huo huo, masuala ya kanuni zinachipuka, ni nani aliye na haki ya kuwakilishwa na vipi?
Huku katiba za nchi nyingi zikiwa zimetoa uhuru kwa wanainchi wote Upigaji Kura, katika hali halisia wapiga kura walio Ngambo ya nchi yao hunyimwa haki ya Upigaji Kura kwa sababu ya ukosefu wa utaratibu wa kuwawezesha kutumia haki hiyo.
Ingawa hili ni tukio la hivi karibuni, upigaji kura wa Ngambo sasa ni ajenda mojawapo ya kisiasa katika mataifa mengi. Haki ya wote, bila kipimo wala vikwazo – upigaji wa kura wa Ngambo umetambuliwa na nchi nyingi kama sehemu ya haki ya wanaichi katika dunia ambapo kuishi ng’ambo ni sehemu ya hali ya maisha ya mamilioni ya watu na ambapo kutekeleza haki na kutii sheria kunabadilkai kila siku.