Haki ya wananchi wote waliokomaa kushiriki katika shughuli za serikali yao ni moja katika mambo ya kimsingi katika demokrasia. Pengine njia moja kuu ya kushiriki huku ni kupiga kura katika uchaguzi ulio huru na wazi. Kwa wananchi kutekeleza haki yao ya kidemokrasia ya ya kupiga kura, lazima pawe na rejista kamilifu na inayojumuisha wapigakura wote, iitwayo pia orodha ya wapigakura, na hii lazima itunzwe vizuri ili kuhakikisha kwamba kila mwananchi anayefaa kupiga kura anasajiliwa mara moja tu kupiga kura. Orodha ya wapigakura hurahisisha kazi ya kutenganisha majukumu mawili muhimu ya halmashauri ya upigaji kura: kuthibitisha ufaafu wa wapigakura na kudhibiti uhalali wa mchakato mzima wa upigaji kura. Orodha hiyo inaweza kutumiwa pia katika kuwaelimisha wapigakura, na inaweza kupewa vyama vya kisiasa na wagombea nyadhifa mbalimbali ili kuwasaidia katika kampeni zao. Japo upigaji kura unaweza kuendelea bila orodha hii, orodha ya wapigakura ina ubora unaoeleza matumizi wake.
Kwa kuthibitisha kwamba wapigakura wameafiki mahitaji yote, orodha ya wapigakura husaidia kuuhalalisha mchakato mzima wa upigaji kura. Kwa upande mwingine, watu wanaweza kushuku uhalali wa mchakato huo iwapo kutakuwa na matatizo katika usajili wa wapigakura, na hasa kuaminika kwa orodha ya wapigakura. Usajili wa wapigakura hivyo basi ni moja katika majukumu muhimu ya wasimamizi wa uchaguzi.
Gharama Kubwa ya Usajili wa Wapigakura
Japo usajili wa wapigakura ni muhimu sana katika usimamizi wa kura, ni ghali sana. Jukumu la kuwasajili wapigakura na kutengeneza orodha zao hugharimu zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya gharama yote ya usimamizi wa kura. Kuna vitu mbalimbali ambavyo huchangia gharama hii. Hivi vinajumuisha, aina ya mfumo wa kusajili wapigakura, uwezo wa wasimamazi wa kura, na sifa za kijamii, kiuchumi pamoja na idadi ya watu.
Usawa na Ushirikishwaji Kisiasa 
Rejista za kura hukuza kanuni za kidemokrasia kwa kuangazia usawa wa wananchi wote na kuhakikisha kushirikishwa kwa wapigakura wanaofaa katika mchakato huo wa upigaji kura. Tofauti huzuka kuhusu hatua ambazo mamlaka za usimamizi wa kura zinapaswa kuchukua ili kuwasajili wapigakura kutoka katika makundi ambayo kihistoria yameonekana kusajili idadi ndogo sana ya watu na kwamba pia ni wachache wao tu ambao hujitokeza kupiga kura – kwa mfano, wanawake, raia kutoka katika makundi yanayodunishwa, maskini, na vijana. Nchi nyingine hujaribu kuhimiza usajili maalumu unaolenga kuzidisha kushiriki kwa makundi haya. Nyingine nazo haziwahusishi moja kwa moja: viongozi husawazisha uwezekano wa watu wote kusajiliwa na kupiga kura, lakini hawang’ang’anii kuongezeka kwa usajili wa kundi maalumu.
Kando na tofauti hizi, kuna mwafaka kuwa ili mfumo wowote uonekane kuwa wa kidemokrasia na unaoshirikisha umma, lazima utoe nafasi sawa kushiriki katika mchakato kamili wa kusajili wapigakura.
Kutengwa Kisheria na Kiusimamizi
Wapigakura wanaweza kutengwa kutoka kwenye orodha za wapigakura ama kisheria au kutokana na njia za kiusimamizi. Katika demokrasia shirikishi zilizozuka katika nchi za Magharibi katika Karne za 18 na 19, ustahifu wa watu kujisajili na kupiga kura ulichukuliwa kwa misingi kama vile kumiliki mali, utajiri, viwango vya usomi, rangi, jinsia na ukomavu wa kiakili. Yeyote asiyeafiki viwango hivi hakuruhusiwa. Kutengwa huku kisheria kuliondolewa taratibu na leo vingi katika vigezo havithaminiwi kuwa sahihi. Hata hivyo, nchi nyingi bado zinawatenga watu kisheria kwa misingi ya umri (aghalabu wapigakura wanapaswa kuwa angalau miaka 18, ingawa matarajio ya miaka wakati mwingine huwa juu zaidi), uraia, makao, kuwa na makosa ya jinai na kukosa akili timamu. Vigezo hivi aghalabu huandikwa katika katiba ya nchi au katika sheria kuhusu kura kutoka kwa wanasiasa badala ya kuchukuliwa kutoka kwa viongozi wasimamizi.
Kutengwa na usimamizi kunajumuisha kuacha nje ya orodha za wapigakura watu ambao wanastahili kabisa kupiga kura. Wanaweza kutengwa ama kwa hiari au kutokana na hali fulani za lazima; kwa mfano, watu wanaostahili kupiga kura wanaweza kwa hiari zao wenyewe kukosa kujisajili kwa kukosa nia au kuwa na mtazamo wa chini kuhusu siasa au uchaguzi. Mpigakura anaweza kusajiliwa kimakosa, au akose kusajiliwa kabisa, kwa sababu ya kubadilisha eneo au jina lake. Aidha, kutengwa kunaweza kusababishwa na udhaifu katika mfumo wa usajili wa wapigakura kama vile kukosekana taarifa za kutosha kuhusu siku ya mwisho ya shughuli ya usajili wa wapigakura. Mfumo mzuri wa usajili hung’ang’ana kuzuia au kupunguza kutengwa kwa wapigakura wanaostahili kupiga kura. Lengo kuu linapaswa kuwa kuwasajili watu wote wanaostahili kupiga kura. Katika hali halisi, hili haliwezi kuafikiwa kwa ukamilifu, lakini linapaswa kuchochea uwekwaji wa vigezo bora vya kiutendaji vitakavyotumiwa kupima viwango vya kufaulu kwa usajili hasa katika usajili wa watu wote.
Uchangamano wa Usajili wa Wapigakura
Katika uamuzi kuhusu usajili wa wapigakura, wasimamizi wa upigaji kura wanapaswa kuzingatia hali za nchi zao, jimbo au eneo lao. Miongoni mwa maswali wanayokabiliana nayo ni:
- Je, orodha ya wapigakura itengenezwe kwa kila uchaguzi au ni bora kutunza orodha iliyopo?
- Wapigakura wanaostahili watajitambulishaje katika vituo vya kupigia kura? Watumie kadi za kura au njia nyingine?
- Ikiwa kadi ya mpigakura itatumiwa, ni taarifa gani inayopaswa kuwa kwenye kadi hiyo?
- Je, usajili uwe wa lazima au kwa hiari ya mtu?
- Kama usajili ni wa hiari, je, raia wenyewe wajitolee au serikali ihimize?
- Je, hali za hapo (k.m. viwango vya elimu, uwepo wa miji, kutembea tembea kwa watu, utajiri wa kadiri, historia na demokrasia) vitaathiri uteuzi wa mfumo wa usajili?
- Uwepo wa tarakilishi utatekeleza jukumu gani katika mchakato wa kuwasajili wapigakura? Ni sehemu zipi za shughuli nzima ambazo itakuwa bora zikishughulikiwa kwa kutumia tarakilishi?
Majibu ya maswali haya na mengine kama haya yatasaidia kutambua aina ya mfumo wa usajili wa wapigakura ambao utawiana na muktadha fulani wa kisiasa.
Mielekeo Mitatu ya Usajili wa Wapigakura
Demokrasia kwa jumla, na hasa usajili wa wapigakura, vinaweza kuchukuwa maumbo mbalimbali. Katika kuamua kuhusu jinsi ya kuzipa umuhimu kanuni za demokrasia ya uchaguzi, ni muhimu kuteua mfumo ambao:
- unaafiki kabisa hali halisi ya hali za eneno hilo
- ni wa kweli na gharama yake inaweza kushughulikiwa kwa kutilia maanani mazingira ya kifedha na kiusimamizi ambamo mfumo huo utajengwa na
Kwa upande wa usajili wa wapigakura, kuna viteuzi vitatu:
- orodha ya muda
- orodha au rejista endelevu
- rejista ya raia/umma
Halmashauri ya kusimamia uchaguzi lazima ichague moja katika hzi, au kuzitumia zote, kama msingi wa kuzingatiwa katika kutengeneza mfumo wa usajili wa wapigakura.
Orodha ya Muda
Rejista ya muda ya wapigakura, au orodha ya muda, hutengenezwa ili kuafiki suala maalumu la uchaguzi, na wasimamizi wa uchaguzi hawana haja ya kuitunza au kuiimarisha kwa matumizi ya baadaye. Aghalabu orodha hii huundwa punde kabla ya uchaguzi ingawa haipaswi kuwa hivyo. Mfumo huu nao ni ghali na unachukua muda mwingi sana kwa kuwa unahitaji kutangamana moja kwa moja na wapigakura wastahifu kabla ya uchaguzi. Unaweza kuwa bora zaidi hasa mahali ambako miundomsingi inakosekana kutunza orodha endelevu, hali ya kuhama hama kwa watu iko juu au ambako kuna upinzani dhidi ya serikali kuendelea kuhifadh orodha ya watu. Orodha ya muda inaweza pia kupendelewa na kiasi fulani cha mashirika ya serikali kama vile halmashauri au tume za kusimamia uchaguzi.
Orodha Endelevu
Orodha endelevu ya wapigakura hutunzwa na kurekebishwa mara kwa mara na usimamizi wa uchaguzi. Mfumo huu hutegemea muundomsingi mwafaka wa kutunza orodha. Utunzaji wake hujumuisha kuongeza majina na taarifa nyingine muhimu kuhusu watu ambao wanaafiki mahitaji ya kupiga kura, na kufuta majina ya wale ambao hawaafiki matarajio hayo (k.v. kupitia kwa vifo au kubadilisha makao). Kwa kuwa orodha endelevu hurekebishwa mara kwa mara hakuna haja ya kampeni za usajili wa mwisho punde kabla ya uchaguzi, ingawa muda hutengwa wa kupitia orodha hiyo wakati wa kampeni. Orodha endelevu inaweza kutunzwa ama kieneo au kitaifa.
Ili kurahisisha urekebishaji wa orodha, halmashauri nyingi zinazoshughulika na uchaguzi hujenga ushirikiano wa kutumia deta pamoja na mashirika mengine ya serikali. Kwa mfano, raia wanapobadilisha makao yao, wanaweza kuwaarifu watoza ushuru, posta, halmashauri za kusimamia nyumba au mfumo wa matibabu. Katika nchi nyingi zilizo na orodha endelevu, ushirikiano huwezesha mamlaka inayoshughulikia uchaguzi kupokea marekebisho ya mara kwa mara ya mabadiliko kwenye faili za mashirika haya. Hili huwezesha urekebishaji wa rejista ya uchaguzi bila kukutana ana kwa ana kati ya mpigakura na halmashauri ya kusimamia uchaguzi. Katika visa vingine, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inapogundua kuhusu mabadiliko ya anwani, halmashauri hiyo inaweza kumtumia mpigakura kadi nyingine mpya ya kupigia kura na ombi la kuijaza na kuthibitisha taarifa zinazoonekana juu yake.
Rejista ya Raia/Umma
Kiteuzi cha tatu cha usajili wa wapigakura ni rejista ya umma/raia. Hii inweza kujumuisha taarifa mbalimbali kuwahusu raia wote, kama vile jina, anwani, uraia, umri na nambari ya kitambulisho. Katika nchi kadhaa, hasa Ulaya na Amerika ya Kusini, orodha ya wapigakura hutolewa kutoka kwenye taarifa iliyoko katika sajili ya raia. Katika nchi zilizo na sajili ya raia, swali kuu huwa ikiwa shirika linalohusika na shughuli hiyo (mara nyingi wizara ya mambo ya ndani) linapaswa kuwajibikia orodha hiyo ya wapigakura. Nchi nyingine huipa asasi hiyo jukumu la sajili zote mbili; nyingine huchagua mashirika mawili, huku kila mojawapo likiwa na jukumu la kushughulikia moja katika orodha hizo.
Ikiwa rejista ya raia ipo, kupatikana kwa orodha ya wapigakura huwa rahisi na nafuu. Hivi ni kwa sababu gharama kubwa huchukuliwa na sajili ya umma. Ijapokuwa ni ghali kuitunza sajili ya raia, taarifa zinazonaswa na kuhifadhiwa zinaweza kutumiwa kwa kazi nyingi hivyo basi kuipunguzia serikali gharama ya kutunza deta.
Kipingamizi kikubwa katika mfumo huu ndicho nguzo yake kuu. Japo gharama yake kubwa au ughali wake unakubalika, kutumia deta kwa kikoa miongoni mwa mashirika ya serikali kunaweza kuzua mikinzano mikubwa. Malalamishi yanaweza kutokea kuhusu kukosekana au uwezekano wa kukosekana kwa siri. Wasiwasi hii ikienea, rejista ya raia inaweza kukataliwa bila ya kujali umuhimu wake.
Picha:
Image:
Kuzinduliwa upya kwa Vikao vya utambulisho wa umma katika Côte d'Ivoire na picha ya Umoja wa Mataifa s licensed under a Creative Commons Attribution-Noncommercial-No Derivative Works 2.0 Generic License.