Sajili ya Raia – Faida / Uzuri —
Skip to content.
|
Skip to navigation
Search Site
Advanced Search…
English
Español
العربية
Français
Swahili
Home
Encyclopaedia
Personal tools
Log in
Practitioners' Network
You are here:
Home
→
Encyclopaedia
→
Mada
→
Usajili wa Wapigakura
→
Mambo ya Kijumla
→
Sajili ya Raia
→
Sajili ya Raia – Faida / Uzuri
face
Practitioner Login
sw
Encyclopaedia
Info
Voter Registration
Topic Index
Sajili ya Raia – Faida / Uzuri
Sajili ya raia ina uzuri kadhaa:
Gharama inayotumika kukusanya deta kwa usajili wa wapigakura ni ya chini kwa sababu taarifa kuu ishakusnywa na kutayarishwa kwenye sajili ya raia. Kwa kiwango kikubwa, shirika jingine la serikali hugharamia malipo hayo kwa niaba ya usimamizi wa uchaguzi. Gharama huwa juu lakini nafasi inayotekelezwa na halmashauri ya kusimamia uchaguzi ni ndogo.
Sawa na ilivyo katika orodha endelevu, taarifa iliyo katika sajili ya husahihishwa mara kwa mara hivyo basi kuiwezesha kutoa orodha ya wapigakura yenye usasa kwa muda mfupi.
Aidha, sawa na orodha endelevu gharama za kutunza sajili ya raia huenezwa katika miaka.
Serikali zinazotumia sajili ya raia hung’ang’ana kuhakikisha kwamba inatoa taarifa ya kutegemewa nay a kutegemewa. Orodha za wapigakura kutoka kwenye mashirika ya usajili huonekana kuwa bora katika mazingira ya vigezo vitatu vya utendaji – usasa, ulinganifu na ukamilifu.
Kwa kuwa mashirika yanayoshughulikia usajili wa raia hutumiwa pia kutekeleza majukumu mbalimbali ya kiusimamizi, mara nyingi raia hupewa muda mfupi wa kutoa taarifa kuhusu mabadiliko yoyote kwenye taarifa zao. Kwa sababu hii, huku mfumo wowote wa usajili ukichelewa kujumuisha mabadiliko hayo, muda huwa mfupi sana kwa sajili za raia, hivyo basi mifumo hii hufanya kazi vizuri katika kigezo cha usasa wa taarifa.
Kwa kuwa sajili ya raia husasaishwa kila mara, hutoa wakati wa kutosha wa kuthibitisha ulinganifu wa taarifa iliyomo.
Wananchi wote huhitajika kuorodheshwa katika sajili ya raia na hivyo kutoorodheshwa kwenye orodha ya wapigakura kumeelezwa kama hujuma ya kijamii. Raia asiye katika sajili huenda akakosa kufikia huduma mbalimbali za kijamii kama vile ajira au faida mbalimbali wanazopata watu wasio katika ajira, usaidizi wa kimatibabu na elimu. Kwa sababu hii, mifumo ya sajili hufanya kazi vizuri katika kigezo cha ukamilifu.
Sajili ya raia inaweza kutumiwa kama msingi wa kutambua wateja wa huduma fulani ya serikali. Kukiwa na usiri wa kutosha (kama ilivyo huko Uswidi), hata mashirika katika sekta ya kibinafsi yanaweza kuifikia deta hiyo na kuepuka gharma ya kutunza orodha za wateja wao wenyewe. Sajili hiyo kwa jumla huwezesha ubora katika uondozi.
Usajili wa Wapigakura
Contributors to Voter Registration
Bibliography
Contact
Privacy Policy
Terms of Use
Accessibility
Site Map
Copyright and Disclaimer
©
1998-2025 ACE project