Katika demokrasia, raia wote wakomavu wanapaswa kustahi kushiriki katika uchaguzi. hili linamaanisha kwamba mahitaji ya ustahifu yanapaswa kuwa pana kiasi cha kuweza kuruhusu wakazi wote au takribani wote waliokomaa waweze kujisajili kupiga kura. Hakupaswi kuwa mikakati iliyopangwa ya kulitenga kundi lolote – iwe wanawake, watu kutoka makabila madogo au yaliyotengwa, maskini au watu wasio na makazi, au wakazi wa maeneo ya mashambani.
Kanuni za ustahifu huangazia umri, uraia na ukazi. Mahitaji mwafaka yanaweza kutofautiana kutoka demokrasia hadi nyingine.
Kwa mfano, demokrasia zote wakilishi huweka mipaka ya upigaji kura kwa watu waliokomaa pekee. Zinatofautiana katika kueleza umri ambao mtu anapaswa kufikisha ili aitwe mtu mzima japo kwa kawaida tofauti ni ndogo, kutoka umri wa miaka 18 hadi 21. Katika demokrasia nyingi vijana wakomavu (walio na umri wa kati ya miaka 18 na 30) huelekea kushiriki kwa kiwango kidogo katika siasa za uchaguzi kushinda wale wanaowashinda umri. Demokrasia nyingi zilizoimarika kiviwanda zimeshuhudia kupungua kwa idadi ya wapigakura vijana kwa zaidi ya miongo miwili sasa. Wamekabiliana na hali hii kwa kubuni mikakati ya elimu na usajili wa wapigakura vinavyolenga raia vijana.
Kihistoria mahitaji ya uraia yameruhusu upigaji kura kufanywa na watu wazima wanaoweza kuonyesha kwamba ni raia wanaoishi katika nchi hiyo ambamo uchaguzi unafanyika. Nchi nyingine zinaendelea kulegeza misimamo kuhusu hitaji hili, hivyoo kuruhusu raia wa kigeni kupiga kura katika chaguzi za nchi hiyo wakitimiza masharti ya kimsingi kuhusu ukazi. Baadhi ya nchi hufungia zoezi la upigaji kura kwa watu walioishi katika eneo hilo la uchaguzi kwa kipindi cha muda kiasi fulani; nyingine huruhusu wananchi wake wanaoishi ughaibuni kujisajili na kupiga kura kwa muda kiasi fulani.
Katika visa vya baada ya mizozo, inaendelea kuwa jambo la kawaida kuongeza haki ya kujisajili na kupiga kura kwa wananchi wanaoishi ughaibuni. Tabia hii inaweza kuchochea kuhusishwa kwa halmashauri za kusimamia uchaguzi kutoka mataifa hayo ya kigeni: zinaweza kusaidia katika usajili na upigaji kura wa wapigakura kama hao, au zinweza kusimamia mkipango ya kuhakikisha kwamba chaguzi hizo zinakuwa huru na mwafaka.
Kanuni zinazoongoza ustahifu wa wapigakura aghalabu hutungwa na sheria ya bunge au katiba ya nchi hiyo, sio na wasimamizi wa uchaguzi. Badala yake jukumu lao ni kutumia kanuni na sera zitakazokuwa zimewekwa.