Ufaafu wa kujisajili kwa mpigakura unapaswa kuwa sambamba na sifa za kimsingi za kustahi kupiga kura. Hizi huelezwa katika katiba ya nchi hiyo, au katika sheria ya haki. Nchi nyingi zinazoazmia kuwa demokrasia hujaribu kutunza haki ya kupiga kura kwa raia wote waliofikisha utu uzima, aghalabu miaka 18. Kunaweza kuwa na mahitaji mengine ya usajili na upigaji kura, hasa katika mfumo unaoegemea kwa maeneo tenge ya upigaji kura. Nchi nyingi hufungia upigaji kura kwa raia ambao haki zao zimeondolewa kwa muda kwa sababu ya kutumiwa kwa kosa fulani la jinai au kuwa na matatizo ya kiakili.
Vizuizi Vichache kwa Usajili na Upigaji kura
Katika miaka ya nyuma kulikuwa na vigezo vingine vingi vya kutambua ustahi wa mtu kushiriki katika maamuzi ya kidemokrasia kama vile umilikaji wa mali, kabila, jinsia na urazini, yeyote aliyeonekana kukosa vigezo hivi alitengwa. Baada ya muda, vigezo hivi vimepoteza uhalali wake na kutupiliwa mbali. Usawazisho wa aina hii unaweza kuonekana kama ulio na vigezo fulani vya kisasa. Kwa mfano, nchi nyingine huruhusu raia wa kigeni kupiga kura katika chaguzi za wenyeji wao almuradi wameafiki mahitaji maalumu ya ukazi. Nchi nyingi zimeendelea kuruhusu raia wake wanaoishi ughaibuni kupiga kura; mifano ya hivi karibuni ni Afrika Kusini, Bosnia na Hezegovina, na Iraki.
Mahitaji ya Uraia kama Kizuizi cha Usajili
Serikali zinazoibuka mpya au nchi zilizo na mipaka ambayo imebadilishwa hivi karibuni au kuzoziniwa kila mara zinapaswa kupambana na suala la wakati ambapo mkazi atafikisha uwezo wa kuwa raia na haki zake zote za kidemokrasia. Hili sio tu suala la kushughulikiwa na halmashauri ya kusimamia uchaguzi. Badala yake, ni suala la kisiasa ambalo litatokeza masuala ya kimsingi ya kiusimamizi kama vile uhusiano kati ya taifa na serikali na hali ya uraia katika serikali hiyo mpya. Hata hivyo, kuna athari ya moja kwa moja kwenye uchaguzi ikiwa mahitaji yasiyolegezeka ya uraia yanazuia idadi kubwa ya wakazi wa nchi hiyo dhidi ya kujisajili kupiga kura. Katika wakati amabpo chaguzi nyingi duniani huchunguzwa na waangalizi – wakiwemo waangalizi wa kimataifa na kitaifa, na wawakilishi wa vyama vya kisiasa – hivyo basi kuweka vizuizi dhidi ya usajili kunaweza kuishia katika tuhuma za kukiuka kanuni za kidemokrasia kuhusu chaguzi huru na zenye uwazi.
Kutambua Wapigakura Waliotimiza mahitaji

Wasimamizi wa uchaguzi wanaweza kuchagua kutoka katika mbinu mbalimbali za kuthibitisha kwamba wapigakura watarajiwa wameafiki mahitaji ya uraia na wanaweza kujitambulisha. Katika nchi zinazotumia orodha za muda, mbinu inayotumika mara nyingi huwa usajili wa kutoka nyumba moja hadi nyingine au ujenzi wa vituo vya usajili wa wapigakura, au vyote viwili pamoja. Utaratibu huo unaweza kuwa changamano zaidi ikiwa wapigakura watarajiwa wanajiwasilisha wenyewe kwa maofisa wa kusimamia uchaguzi. Katika nchi ambamo wakazi wake hubeba vitambulisho kama vile cheti cha kuzaliwa, pasi, kadi ya kitambulisho cha raia au leseni ya udereva, kutolewa kwa kitambulisho hicho huwa kumetosha. Ikiwa wakazi hao hawabebi vitambulisho vya kibinafsi – hasa katika nchi changa – kauli ya kiapo inaweza kuhitajika kutambua kitambulisho cha mtu, au raia mwingine anaweza kutoa habari kwa niaba ya mtu huyo.
Katika nchi zinazotumia orodha endelevu, utaratibu huo hutofautiana kutegemea kama mtu huyo anajisajili kwa mara ya kwanza au anabadilisha taarifa ambayo tayari iko kwenye orodha hiyo. Usajili wa mara ya kwanza hutofautiana kidogo na mbinu inayotumika katika orodha ya muda. Kwa mfano, ili kuthibitisha utambulisho na ustahifu, mtu ambaye amefikisha umri wa kupiga kura katika siku za hivyo karibuni anaweza kuonyesha cheti chake cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho kilicho na picha, ilhali raia wageni watahitajika kuonyesha stakabadhi za uhamiaji. Kama ni suala la kubadilisha taarifa ya mtu ambaye tayari yuko kwenye orodha hiyo, inaweza kuwa muhimu kuonyesha vitambulisho vinavyofaa – pengine cheti cha ndoa ili kubadilisha jina au leseni ya udereva kwa kubadilisha anwani.
Katika nchi zinazotumia sajili ya raia, kitambulisho cha mpigakura mtarajiwa mara nyingi hutambuliwa kwa kutumia nambari ya kitambulisho ya mtu huyo ili kukagua rekodi yake kama raia. Taarifa hiyo inaweza kuhamishwa kutoka kwenye sajili ya raia hadi kwenye sajili ya uchaguzi muda baada ya muda ili mabadiliko yote yaliyo kwenye sajili ya raia yaweze kudhihirika katika sajili ya uchaguzi.
Kupiga kura mbali na Kituo cha Kawaida cha Kupigia Kura
Mifumo mingi ya upigaji kura huwataka wapigakura kujisajili katika vituo maalumu vya kupigia kura na kufungia upigaji kura kwa watu waliojisajili pekee katika eneo hilo. Mara nyingi huwa muhimu kupekeesha, hata hivyo, kwa wapigakura ambao hawana budi kuwa mbali na makao yao ya kawaida wakati wa uchaguzi. Suluhisho moja ni kuruhusu upigaji kura wa mapema kwa yeyote atakayekuwa mbali wakati wa kawaida wa kupiga kura. Suluhisho jingine ni kutoa idhini ya uhamisho wa usajili kwa mtu ambaye hatakuwepo kwa sababu zinazokubalika au kuridhisha kuwa ni halali. Sababu hizo zinaweza kufafanuliwa kwa njia rahisi sana ili kutoa fursa ya kutumiwa kwa mbinu hii kwa maofisa wa kusimamia uchaguzi pekee au wanajeshi ambao hawatakuwepo kwa sababu ya shughuli zao rasmi; au zinaweza kuelezwa kwa upana ili kumfikia mtu yeyote anayehisi kwamba hataweza kupiga kura siku yenyewe ya uchaguzi.
Kutengwa dhidi ya Kupiga kura
Halmashauri ya kusimamia uchaguzi hujaribu kusajili yeyote anaestahili kupiga kura. Hata hivyo, katika nchi ambamo upigaji kura ni lazima, watu wanaweza kupendelea kutohusishwa katika shughuli ya kupiga kura. Katika nchi ya Brazili, kwa mfano, upigaji kura ni lazima kwa wananchi wote walio kati ya miaka 18 na 70 – ila tu kama hawana uwezo wa kusoma, ambapo katika hali hiyo sasa wako huru kuteua. Upigaji kura ni wa hiari kwa watu walio na umri wa miaka 16 au 17, au yeyote aliyepitisha umri wa miaka 70. Mpigakura yeyote aliyesajiliwa katika Brazili anayetamani kutoshirikishwa katika shughuli ya kupiga kura anapaswa kutuma ombi la ruhusa hiyo kutoka kwa jaji wa uchaguzi katika eneo lake la upigaji kura.
Image:
Afghan Elections 2009 (Kandahar City) / Élections Afghanes 2009 (Kandahar) by Canada in Afghanistan / Canada en Afghanistan is licensed under a Creative Commons Attribution-Noncommercial-No Derivative Works 2.0 Generic License.