Skip to content. | Skip to navigation
Lengo kuu la kuunda orodha ya wapigakura ni kutenganisha jukumu la kukagua ufaafu wa wapigakura kutoka kwenye mchakato wa upigaji kura. Usajili wa wapigakura huhusisha kuidhinisha kwamba mtu fulani anafaa kupiga kura, pamoja na kumwarifu mtu huyo kuhusu kituo cha kupigia kura pale ambapo yeye atapigia kura na eneo pana la uchaguzi (ikiwezekana) ambako kura zitahesabiwa. Si muhimu kabisa kutenganisha ukaguzi wa ustahifu wa wapigakura kutoka kwenye shughuli ya upigaji kura, na chaguzi nyingine, zikiwemo chaguzi za kitaifa, zimefanywa pasi na uwepo wa orodha yoyote ya wapigakura. Hata hivyo, ni rahisi zaidi kuendesha shughuli za siku ya upigaji kura ikiwa idhinisho limekamilishwa na kutumiwa kutoa orodha ya wapigakura.
Pamoja na kuidhinisha kwamba watu walioorodheshwa wanastahi kupiga kura, rejista ya wapigakura ina matumizi mengine yanayoeleza vizuri ustahi wa kutumia gharama yote hiyo kuzitengeneza. Miongoni mwa sehemu ambamo ina matumizi ya ziada ni zifuatazo:
© 1998-2025 ACE project