Usalama katika Usajili wa Wapigakura
Kwa kawaida, usajili wea wapigakura huhitaji viwango vikubwa vya usalama. Mara nyingi huwa na udhibiti kwenye matumizi ya orodha ya wapigakura na hivyo matumizi mabaya huwa kosa la kuchochea adhabu. Mara nyingi matumizi ya rejista ya uchaguzi pamoja na orodha ya wapigakura iliyotumiwa kujenga rejista hiyo, yametengewa halmashauri ya kusimamia uchaguzi na kupitia kwa halmashauri hiyo, vyama vya kisiasa. Hata hivyo, vyama, wagombea wake na wafanyakazi wake mara nyingi huwa na nafasi ndogo ya kufikia orodha ya wapigakura, hupewa nakala chache, na huruhusiwa kutumia orodha hizo pale wanapokuwa kwenye kampeni za uchaguzi huo na kwa kawaida hawawezi kuzisambaza orodha hizo. Udhibiti mkubwa hata zaidi huwa kwenye matumizi ya orodha ya wapigakura kapa: haitolewi kwa umma wala kupewa vyama vya kisiasa katika shughuli za kampeni.
Kibadala cha Kutumia Huduma za Nje
Licha ya vizuizi hivi vya kiusalama, si kazi zote zinazohusiana na orodha ya wapigakura zinazopaswa kushughulikiwa na halmashauri ya kusimamia uchaguzi. shughuli nyingine zinaweza kukamilishwa, kwa viwango vinavyokubalika, na wafanyakazi wengine wa nje katika mashirika ya kiserikali au sekta ya kibinafsi. Ifuatayo ni baadhi ya mifano:
- Kutumia tarakilishi. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi itanunua tarakilishi ya kutumiwa katika usajili wa wapigakura japo sehemu za ndani zinazohitajika kutengeneza orodha zinaweza kutolewa kwa kandarasi na wajenzi wa mitambo hii. Anayepewa kandarasi anaweza pia kutunza mitambo hiyo. Katika eneo linalotumia orodha ya muda, usajili wa wapigakura ndio huchukua nafasi kubwa ya muhula wa uchaguzi, na hivyo huenda ikawa vigumu kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi kuwa na wahudumu wa kutengeneza mfumo huo tarakilishi kila wakati. Kwa hakika, mfumo wa tarakilishi wenyewe utaweza pengine kupanuka taratibu punde kabla ya kuanza kwa usajili na pengine wanaweza kufunga punde baada ya kukamilika kwa usajili. Kutakuwa na shughuli nyingine za ziada katika kuunganisha tarakilishi ili kuunganisha vituo vya usajili au ofisi za usajili na makao makuu ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi; hii ni shughuli nyingine itakayogharimu kutafuta huduma kutoka nje.
- Utumizi mbaya wa nyenzo. Usajili wa wapigakura mara nyingi hutumia nyenzo nyingi, kwa kutegemea fomu za karatasi, hifadhi ya fomu zilizojazwa, vifaa vya ofisi, nyenzo za kutumiwa kwa elimu ya wapigakura miongoni mwa vingine. Shughuli muhimu ni pamoja kuhifadhi, usafirishaji na usambazaji wa nyenzo, na kutengeneza na kuchapisha nyenzo za usajili na elimu kwa wapigakura. Kutafuta huduma hizi kutoka nje kunaweza kuimarisha shughuli hiyo.
- Vifaa vya mawasiliano. Haja ya vifaa vya mawasiliano huongezeka wakati wa usajili hasa katika maeneo yanayotumia orodha ya muda. Kutafuta huduma za nje kunaweza pia kuwa njia nzuri ya kubuni, kutunza na, kwa wakati mwafaka kuvunja muundomsingi wa mawasiliano.
- Kutoa kadi za utambulisho wa wapigakura. Utumiaji wa huduma za nje unaweza kuwa suluhisho mwafaka la kutengeneza kadi za utambulisho wa wapigakura. Kadi zilizo na taarifa za kiusalama zinaweza kuwa ghali sana kutengeneza. Ikiwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi inahitaji kadi zitengenezwe katika muda fulani, basi kutumia huduma za nje kunaweza kutoa kazi yenye ubora unaokubalika kwa bei nafuu.
Kinga katika Utumizi Huduma za kutoka Nje
Halmashauri ya kusimamia uchaguzi huendelea kudumisha jukumu na kuwajibikia utendakazi wa shughuli muhimu, hata kama huduma hizo zimetolewa nje. Kinga zipo ili kupunguza hatari inayoweza kuzuka kutokana na udhibiti uliopungua kuhusu vipengele vya mchakato wa usajili:
- Mkichukua huduma yoyote kutoka nje, hakikisheni kwamba kunakuwa na viwango mwafaka, vilivyo wazi na vinavyoeleweka vizuri. Jumuisha viwango mwafaka vya utendakazi katika kandarasi hiyo.
- Sisitiza umuhimu wa udhibiti wa ubora. Hakikisheni kwamba halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kudumisha jukumu la wazi la uangalizi. Inaweza kufanya hivi tu ikiwa wafanyakazi mwafaka.
- Kandarasi inayoeleza adhabu za kupewa wale wanaokiuka husaidia kuhakikisha kwamba mtoaji wa huduma hiyo anashiriki katika hatari inayoambatana na utendakazi duni. Kugawana hatari hiyo husaidia kuhakikisha kwamba haja za wadau wote zinalenga kupata malengo yalioafikiwa katika kandarasi hiyo.