Kwa kuwa kazi nyingi ya usimamizi wa uchaguzi huhusisha kukusanya, kuhifadhi, kuhalalisha na kusasaisha deta kuhusu utambulisho wa wapigakura, maofisa wa kusimamia uchaguzi katika nchi mbalimbali wamaenza kuweka michakato hii katika tarakilishi. Faida zake ni wazi na mara nyingi za kushawishi kufanya hivyo. Tarakilishi huwapa maofisa wa kusimamia uchaguzi uwezo wa kuhifadhi deta kubwa kwa usalama, kutengeneza na kugawa deta hiyo katika njia mbalimbali, na hasa kubadilisha mambo mengine kama vile mipaka ya maeneo ya uchaguzi kwa kurejelea faili za tarakilishi kuhusu idadi ya wapigakura.
Katika visa vingine hata hivyo, mazingira ya kijamii, kiuchumi au kisiasa yanaweza kutatiza utumizi wa tarakilishi au hata usiowezekana kabisa. Licha ya haya, bado kunapaswa kuwa na njia za kutekeleza mikakati ya usajili inayofaulu katika vigezo vya usasa, ulinganifu na ukamifu. Ijapokuwa utumizi wa tarakilishi katika unaendelea kuongezeka katika demokrasia zilizoimarika kiuchumi, tarakilishi zilianza kutumika katika kizazi kilichopita na hasa mwongo uliopita. Kabla ya miaka ya 1980 na 1990 kwa mfano, tarakilishi hazikuwa vyombo mwafaka, bora au nafuu vya usajili.
Pale inapowezekana, wasimamizi wa uchaguzi sasa hivi wamepata kwamba tarakilishi zinaweza kufanya shughuli za usajili kuwa bora na nafuu. Kwa kweli, wanakabiliwa na shinikizo linaloongezeka la ‘kusasaisha’ usajili ambayo inaweza kuwasajiisha kutumia mifumo ya kitarakilishi. Ari ya kutumia tarakilishi mara nyingi huchochewa na matarajio yanayoongezeka kuhusu kuharakisha shughuli ya usajili, vilevile haja ya kukagua orodha za wapigakura katika njia mbalimbali (k.m. kwa kutumia vitengo vya kijiografia kama vile maeneo ya kupigia kura).
Ni muhimu hata hivyo, kutambua gharama inayohusishwa katika ujenzi na utunzaji wa faili za usajili wa kutumia tarakilishi. Si suala tu la kujenga na kuweka tarakilishi mitambo ya ndani na nje ya tarakilishi: kutakuwa na haja ya mara kwa mara ya kuufanyia uchunguzi wa kitaalamu na kuusasaisha mfumo huo, na kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi na mafunzo ya hali ya juu kuzitumia tarakilishi hizo. Kinachohitajika ni tathmini ya makini ya faida na upungufu wake, pamoja na tathmini ya kweli kuhusu uwezo wa kuudumisha mfumo huo katika siku za baadaye.
Faida na Upungufu wa kutumia wa Tarakilishi
Matumizi ya tarakilishi kwa sehemu mbalimbali za mchakato wa usajili wa wapigakura yanaweza kupunguza gharama au kuimarisha kabisa kuaminika kwa deta hiyo. Matumizi ya tarakilishi ni muhimu hasa kwa shughuli zifuatazo:
- shughuli ya mwanzo ya kunakili taarifa kuhusu wapigakura
- kulinganisha kadi za utambulisho wa wapigakura, zikiwemo nambari za usajili na kiziodeta cha usajili
- kutunza orodha endelevu, ikiwemo kuwasambazia wapigakura nakala ya taarifa za kisasa kuwahusu zilizo kwenye faili yao ya kisasa
- kuchapisha nakala za orodha za kwanza za wapigakura
- kudumisha rekodi za hesabu ya nyenzo zilizo katika vituo vya kieneo vya usajili au katika makaomakuu
- uingizaji wa deta ili kusahihisha orodha ya mwanzo ya wapigakura
- kuchapisha nakala za orodha za mwisho za wapigakura
- uwekaji na utunzaji wa rekodi za kijumla
- kutambua watu waliojisajili mara mbili
- kutoa takwimu kuhusu usajili wa wapigakura kwa kurejelea maeneo ya kijiografia, na vilevile jinsi, umri, na kadhalika
- kutoa uthabiti na viwango kwa deta iliyoonyeshwa kwenye orodha ya wapigakura
- kutoa nakala za orodha ya wapigakura katika maumbo mbalimbali ya kielektroniki kwa vyama vya kisiasa kwa gharama ndogo na bila kuharibu karatasi
- kuhakikisha ukaguzi wa mara kwa mara wa mabadiliko yanayofanywa kwa kila rekodi ya mpigakura – kwa mfano, badiliko hilo lilifanywa na nani, kwa misingi ya taarifa kutoka wapi, na ni deta ipi iliyobadilishwa, hivyo basi ni sehemu zipi za rekodi zilizoathiriwa na mabadiliko hayo, na kadhalika.
Matumizi ya tarakilishi pia yana upungufu ufuatao: - Ufaragha na Usiri. Matumizi ya tarakilishi huenda hayakiuki suala la ufaragha au usiri. Lakini ikichukuliwa kuwa matumizi haya yanarahisisha uhifadhi, ugawanaji na usambazaji wa deta iliyo kwenye tarakilishi, kuna uwezekano kwamba deta inaweza kugawanwa visivyo au hata kwa njia zisizo za halali. * Hatari ya kuibwa. Mfumo wa kutumia tarakilishi huhusisha kwa karibu mitambo ya nje ya tarakilishi (bidhaa ya thamani kwa wezi) na mtambo wa ndani na taarifa kuhusu usajili wa wapigakura (kwa kawaida haina thamani kwa wezi). Orodha iliyotengenezwa kwa mikono hutofautisha mtambo wa nje wa tarakilishi na taarifa. Kwa mfano, mashine ya tapureta inayotumiwa kutengeneza orodha ni tofauti kabisa na orodha ya wapigakura yenyewe, iliyo kwenye karatasi. Hata hivyo, kukiwa na orodha zilitengenezwa kwa matumizi ya tarakilishi, taarifa hiyo mara nyingi huhifadhiwa kwenye tarakilishi hizo na hivyo imefungamanishwa na mtambo wa nje wa tarakilishi. Mtambo huo wa nje ukiibwa, mtambo wa ndani na taarifa kuhusu usajili pia vitakuwa vimepotea.
- Ugawanaji wa habari usio mwafaka. Matumizi ya tarakilishi hurahisishia mashirika ya serikali uwezo wa kugawana taarifa ambazo pengine zinapaswa kulindwa (kwa mfano, rekodi za afya na utoaji ushuru wa wananchi).
- Gharama. Kuna gharama kubwa kwa kununua mitambo ya nje, ya ndani na kuvitunza. Utunzaji na uimarishwaji wa mara kwa mara vitakahitajika kwa mitambo hiyo, na vilevile muundomsingi wa kielektroniki wa kuendesha mfumo huo ipasavyo.
Kuanza
Hakuna radimu za tarakilishi za kutumiwa kwa shughuli za usajili mpana wa wapigakura, japo mpango wa halmashauri za kusimamia uchaguzi wa kuweka orodha ya wapigakura katika tarakilishi haipaswi kuanzia chini. Mara nyingi, usaidizi wa kiwango fulani upo kutoka kwa halmashauri za kusimamia uchaguzi katika nchi nyingine ambazo zimefaulu kuweka matumizi ya tarakilishi. Suala kuu ni kupata mfumo bora unaoweza kutumiwa na viwango Fulani vya ubora na ufaafu.
Hofu na/au kutoelewana vimeenea kuhusu uwezekano na matumizi ya tarakilishi. Suala la kutumia tarakilishi lilipojadiliwa katika muktadha mmoja, kwa mfano, hofu moja kuu ilikuwa kwamba tarakilishi zingeweza kutoa ufuasi wa mtu kisiasa au makabila wanamotoka. Katika muktadha mwingine, hofu ilikuwa kwamba matokeo ya uchaguzi yangebadilishwa na halmashauri za kusimamia uchaguzi au serikali. Katika muktadha wa tatu, watetezi wa matumizi ya tarakilishi walishikilia kwamba matumizi ya tarakilishi hizo yangerekebisha makosa katika uingizaji deta, au kusahihisha rekondi zilizoingizwa kimakosa au vibaya. Mradi wa kwanza ukienezwa vizuri unaweza kufanya hatua kubwa kabisa katika kuondoa mitazamo hiyo mibaya kuuhusu.