Huku mifumo ya uchuguzi ikiwa taasisi muhimu zaidi inayoathiiri jinsi ambavyo mifumo ya serikali ya nchi fulani inavyofanya kazi, hapo awali haijabainishwa kirasmi katika katiba, chanzo cha juu cha sheria; katika miaka ya hivi karibuni hivyo basi haya yameanza kubadilika .
Sasa hivi, nchi nyingi zimeweka mambo muhimu kuhusu mifumo ya uchaguzi kwenye katiba zao au kwenye ratiba iliyotengwa kwenye katiba, Umuhimu wa hili kwa wanaounga mkono mabadiliko ya uchaguzi ni kuwa sheria zilizofanywa madhubuti kwenye katiba huwa ngumu zaidi kubadilisha kuliko sheri za kawaida, huku zikihitaji idadi kubwa maalum ya wawakilishaji bungeni, kura ya maoni ya kitaifa hutumia vibaya au mikakati mingine iliyothibitishwa, ambayo huhifadhi mifumo na mabadiliko ya haraka .
Kwa mfano katiba ya Afrika Kusini hueleza kuwa mfumo wa uchaguzi wa uanabunge huwa na matokeo ya kawaida katika usawazishaji na hivyo mabadiliko badala ni machache katika mifumo ya aina ya PR isipokuwa tu pale ambapo marekebisho ya kikatiba yamefanywa.
Hata hivyo, maelezo kuhusu mfumo wa uchaguzi yanapatikana sana katika sheria ya kawaida na hivyo huweza kubadilishwa na walio wengi katika bunge. Haya yanaweza kuwa na upendeleo kwa kufanya mfumo uwe wa kuvutia zaidi wakati wa mabadiliko ya maoni ya umma na mahitaji ya kisiasa, lakini bado inajumlisha hatari ya waliowengi katika bunge ya upande mmoja ikibadilisha mifumo ili kujipatia upendeleo wa kisiasa .
Nafasi za mabadiliko hutegemea mikakati ya kisheria ya kuleta mabadiliko pamoja na miktadha ya kisiasa ambapo wito wa mabadiliko hufanyiwa. Siyo miondoko yote ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi inayofaulu. Karibu mifumo yote ya hivi karibuni ya mabadiliko muhimu imejitokeza katika mojawapo ya hali hizi mbili.
Ya kwanza ni katika njia ya mabadiliko ya kidemokrasia au baadaye kidogo, wakati muundo kamili wa kisiasa unang,ang,aniwa na wote .
Ya pili ni pale ambapo kuna migogoro ya kiutawala katika demokrasia iliyowekwa. Mifano miwili huchukuliwa kuwa isiyo halali kwenye serikali mbili zenye ufuasi wa wengi zinazofuatana na zilizochaguliwa kwa kura chache kuliko zile za wapinzani wengi huko New Zealand, na mtazamo ni kuwa viwango vya juu vya ufisadi katika maeneo ya Italy na Japan vilikuwa vimeenea hadi kwenye mfumo wa kisiasa badala ya matokeo ya hatua ya watu binafsi .
Hata pale ambapo kuna shaka kubwa inayoenezwa ya kutoridhishwa na mfumo wa kisiasa, mabadiliko yanahitaji kuafikiwa na wanaoshikilia uongozi wakati huo. Wanasiasa waliosoma huweza tu kuchukua hatua pale ambapo watajifaidi kutokana na mabadiliko au ikiwa wanaogopa athari za uchaguzi zitakazowakumba ikiwa hawatakubali mabadiliko. Hata pale wanaposadikishwa, bila kushangazwa au kwa kutoepukika, watajaribu kuchagua mfumo ambao utawafaidi wao zaidi ikiwa hawana uhakika, hili linaweza kufanikishwa au ikiwa mitazamo tofauti inahitaji suluhusho tofauti, maafikiano yatakayojadiliwa huwezekana – pengine kwa kuihusisha mifumo iliyochanganyika .
Vigezo kumi vilivyotolewa huwa wakati mwingine vinagongana au huwa vimejitenga vyenyewe. Wapangaji wa mfumo wa uchaguzi basi lazima wapitie mchakato maalum wa kupanga ni vigezo vipi ambavyo ni muhimu kwa muktadha fulani wa kisiasa kabla ya kuendelea katika kutathmini ni mfumo upi utakaofanya kazi bora zaidi.
Njia bora zaidi ya kufuata ni kwanza kuorodhesha mambo ambayo yanahitaji kuepukwa katika hali zote, kama vile machafuko ya kisiasa ambayo huweza kusababisha kuvunjika kwa demokrasia. Kwa mfano nchi ambayo imegawika kikabila huweza kuhitaji, zaidi ya yote, kuepukana na na kuyaondoa makundi ya makabila madogo kutokana na uwakilishaji ili kuimarisha uhalali wa mchakato wa uchaguzi na kuepuka mitazamo ya kwamba mfumo wa uchaguzi haukuwa wa haki.
Katika ulinganuzi huu, baadhi ya masuala kama haya yakiwa muhimu kwa mfumo wa uchaguzi, demokrasia changa kwingineko huweza kuwa na mahitaji tofauti – pengine katika kuhakikisha kwamba serikali inaweza kuweka sheria kwa ufanisi bila woga wa kufungiwa, au kwamba wapigaji kura wataweza kuondoa viongozi wabaya wakitaka .
Kuweka umuhimu miongoni mwa vigezo kama hivi shindani huweza tu kuwa uwanja wa washiriki wa ndani wanaoshirikishwa katika mchakato wa mpango wa kitaasisi. Hata hivyo, makubaliano na mabadiliko huweza kuwa na athari kinyume na ilivyopangwa na watetezi au huweza kuwa na athari nyingine ambazo hazikutarajiwa. Katika nchi ya Mexico, mabadiliko katika mwaka wa 1994 yaliyopangwa na chama kinachotawala ili kuweka makubaliano na upinzani yalipelekea kuwepo kwa matokeo yasiyolingana katika miaka ya hivi karibuni. Mifano ya Afrika Kusini na Chile inaeleza ukweli kwamba uhalisia wa kisiasa na matamanio ya vyama vinavyotawala ya kushikilia uongozi wao na kushawishi huweza kuwa zaidi ya kikwazo kwenye mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kama vilivyo vikwazo vya kisheria. Nchini Afrika Kusini kumekuwa na vilio vingi kuhusu elementi ya uwajibikaji nchini utakaojengwa kwenye mfumo wa PR wa orodha funge katika wilaya kubwa za uchaguzi ambapo wawakilishi waliochaguliwa huchukuliwa kuwa kama wamejitenga na wapigaji kura wao. Haya yamehimizwa kutokana na matokeo ya wengi ya tume ya uraisi ambayo ilitoa ripoti mwezi wa Januari mwaka wa 2003, lakini serikali ilikwepa mabadiliko ambayo yangepunguzia udhibiti wao wa kuchagua wagombeaji na jinsi ambavyo wanachama wangechagua wagombeaji, na kukataa kuruhusu mabadiliko. Zaidi ya miaka kumi baada ya kutolewa mamlakani, mfumo husalia kwa ufanisi kama bado haujabadilishwa.
Huko New Zealand, matumizi ya kura ya maoni wakati wa mchakato wa mabadiliko ulisababishwa mwanzoni na sababu za kisiasa - jaribio la kiongozi wa chama kimoja kikubwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu. Katika kura ya maoni ya kwanza, wapigaji kura waliulizwa ikiwa walitaka mabadiliko yoyote na waonyeshe mfumo mpya walioutaka kutokana na mifumo minne. Katika kura ya maoni ya pili, mfumo mpya uliochaguliwa ulishindwa na kupendelea mfumo uliokuwa unatumika awali. Kutokana na haya, mfumo mpya uliosawazishwa wa wanachama wengi ulichukuliwa huku ukiungwa mkono kihalali na umma.
Mifumo ya uchaguzi hatimaye itahitaji kurekebishwa kulingana na wakati ikiwa itahitajika kutumiwa kulingana na mielekeo na mahitaji mapya ya kisiasa , idadi ya watu na kiubunge. Hata hivyo, pale tu ambapo mfumo umechaguliwa, wale ambao wanafaidika kutokana nao huweza kukataa mabadiliko. Bila mageuzi au migogoro ya kisiasa kama kichocheo, inaonekana kwamba mabadiliko ya kando kando huwezekana kuliko mabadiliko ya kimsingi katika mabadiliko ya baada ya migogoro, hili husababisha wasiwasi kati ya vikwazo halisi ambavyo huweza kuathiri utekelezaji wa uchaguzi unaoongozwa, kwa mfano, na siasa za haraka za makubaliano ya amani ,na matamanio ya kupata mfumo ulio sawa mwanzoni. Katika kujaribu kuleta maendeleo, kwenye mifumo iliyopo, wabadilishaji huweza kuzingatia ukubwa wa mabadiliko ya wilaya, viwango vya mwanzo au fomula ya idadi ya kikomo. Mengi ya mabadiliko ya kutajika yaliyopendekezwa miaka michache ya hapo awali huhusisha kuongeza elementi ya orodha ya PR kwenye mfumo wa FPTP iliyopo ili kuunda mfumo uliochanganywa, na uliosawasishwa zaidi (kwa mfano mabadiliko yaliyofanywa kuwa sheria huko Lesotho na Thailand).

