Baada ya uamuzi kufanywa kuhusu malengo muhimu yatakayotimizwa, na vikwazo muhimu vya kuepuka – katika mfumo wa uchaguzi , kuna kundi la vyombo vya mpango wa muundo wa uchaguzi ambavyo huweza kutumiwa ili kusaidia kufanikisha malengo haya. Vyombo hivi ni pamoja na:
- Kundi na aina ya mfumo wa uchaguzi
- Ukubwa wa wilaya
- Jukumu la uhusiano wa vyama vya kisiasa na wagombeaji
- Muundo wa karatasi ya kura
- Taratibu za kubainisha mipaka ya maeneo ya uchaguzi
- Mikakati ya usajili wa orodha ya wapigaji kura
- Uwekaji muda na mapatanisho ya uchaguzi
- Quota na utoaji wa hali nyingine maalum
Vyombo hivi vitafanya kazi tofauti katika miungano tofauti. Matumizi yake hutegemea kiwango cha ufahamu au huweza kupatikana katika jamii, kwa mfano idadi, aina na mahali kundi la watu linapatikana. Athari yake pia itategemea vyombo vingine vya muundo wa kitaasisi, kama vile uteuzi kati ya mfumo wa bunge na wa uraisi, mahitaji ya usajili na utawala wa vyama vya uchaguzi, uhusiano kati ya vyama vya kisiasa na vichocheo na uwezo wa kukumbuka. Ni muhimu kusisitiza tena kwamba hakuna hata suluhisho moja sahihi ambalo linaweza kulazimishwa kwenye ombwe tupu.

