Mifumo ya uchaguzi kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kama yenye athari mahususi kwenye maswala ya utawala, undaji wa sera na udhabiti wa kisiasa. Mifumo tofauti ya uchaguzi huwa na athari zinazotambulikana kwenye utawala katika mifumo ya bunge. Hasa huwa kuna wasiwasi unaokuwepo kati ya mifumo ya uchaguzi ambayo huonyesha uwezo wa serikali au chama kimoja (kama vile mifumo yenye ufuasi wa wengi) na ile ambayo huwezesha kuwepo kwa miungano ya vyama vya kisiasa (kama vile mifumo iliyosawazishwa). Makundi haya mawili huwa na athari za kisera zilizo wazi: serikali ya chama kimoja hufanya uundaji wa sera uliokamili na huweka wazi majukumu kwa njia rahisi huku miungano ikiwa na uwezekano wa kutoa sera zaidi za uwajibikaji na utoaji wa uamuzi uliokamili. Vile vile, mabadiliko muhimu kuhusu sera za serikali huwa rahisi kufanikisha chini ya serikali ya chama kimoja huku miungano ikiwa na uwezo wa kuhakikisha kuwa masuala yanajadiliwa na kushughulikiwa kabla ya hatua zozote kuchukuliwa.
Karibu nchi zote ambazo huwa na katiba yenye sifa za uchaguzi wa uraisi au huwa ma sifa za uraisi kwa kiasi fulani huchagua raisi kwa njia ya moja kwa moja. Pamoja na hayo baadhi ya jamhuri ambazo huwa na katiba zenye sifa za uanabunge hivyo huchagua kiongozi wa taifa kwa njia ya moja kwa moja. Katika mifumo ya uraisi, kiwango ambacho raisi aliyechaguliwa huweza kudai kipindi cha utawala na uhalali kutoka kwa wengi hutegemea kwa kiasi kikubwa njia ambazo raisi alichaguliwa kwazo. Raisi ambaye huwa na ufuasi wa wengi ulio wazi ana uwezekano wa kuwa na uhalali mwingi na kuwa katika nafasi imara ya kusukumia sera zake kuliko wale waliochaguliwa kupitia kura ya wafuasi walio wachache. Hili huwa na athari muhimu katika mahusiano kati ya raisin a wanabunge. Raisi aliyechaguliwa kupitia kura ya walio wengi iliyo wazi huweza kuwa na uwezo mkubwa ya uhalali panapotokea migongano yoyote bungeni. Kwa kulinganua, uchaguzi wa Salvador Allende huko Chile wa mwaka wa 1970 uliokuwa na asilimia 36 ya viti, na uliopingwa na Rightwing Congress, ulisaidia kuunda hali zilizopelekea kuwepo kwa mapinduzi ya jeshi mwaka wa 1973.
Uhisiano uliopo katia ya bunge na mawaziri hutofautiana kati ya mifumo ya bunge yenye sifa fulani za uraisi na ile yenye sifa za uraisi. Katika mfumo wa uraisi au wenye sifa fulani za uraisi nafasi ya raisi haitegemei uimarishaji wa uhakika wa bunge: raisi kama huyu hawezi kutolewa afisini kwa kuzingatia misingi ya sera pekee. Htaa hivyo, uzoefu wa aina hii huko Latin Amerika, kwa mfano huonyesha kuwa raisi aliyechaguliwa kwa njia ya moja kwa moja bila ufuasi wa kimaeneo wa kuutosha katika bunge atakuwa na wakati mgumu wa kuongoza serikali. Katika demokrasi za uraisi, mifumo ya uchaguzi ya urasisi na uanabunge hivyo huhitaji kushughulikiwa kwa pamoja hata kama majukumu tofauti ya uraisi wa wanabunge huleta masiala tofauti wakati wa kutumia teuzi hizi mbili za mifumo. Uwekaji pamoja wa uchaguzi wa uraisi na wa uanabunge au kinyume chake na nafasi ambazo huweza kuimarisha au kuvunja moyo ugawanyaji wa vyama na uhusiano uliopo kati ya vyama na wanachama waliochaguliwa unastahili kuzingatiwa wakati mmoja.
Mada ndogo za sura hii ni:
- Uchaguzi wa Chemba cha Juu
- Daraja Tofauti za Utawala
- Uchaguzi wa Taasisi za juu ya mataifa
- Uchaguzi wa Bunge za Tifa au za Shirikisho na Mamlaka Huru
- Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Mifumo ya Uchaguzi na Vyama vya Kisiasa
- Teuzi za Demokrasia ya Moja kwa Moja

