Kama ilivyotajwa hapo awali, mahitaji ya upangaji wa mfumo wa uchaguzi hutoafautiana kutegemea aina na shirika litakalochaguliwa pamoja na majukumu na uwezo wake. Wakati shirika linalopangwa ili kufanyia kazi mapendeleo ya juu ya mataifa, wilaya au kieneo, yanayozingatiwa katika uteuzi wa mfumo huwa tofauti kutokana na yale yanayohusishwa wakati wa upangaji wa mashirika ya taifa ya uwakilishaji.

