Uwakilishji wa maeneo au mataifa katika shirikisho huweza kutumia mfumo wa uchaguzi kama bunge la kitaifa (lenye ulinganifu), kama ilivyo huko Afrika Kusini katika mfumo wa orodha funge ya mfump wa PR, au wanaweza wakatumia mifumo tofauti (isiyo na ulinganifu), kama ilivyo huko UK, ambapo Bunge la Scotish na Bunge la Wales huchaguliwa kwa kutumia mfumo wa MMP nao wawakilishaji eneobunge huchaguliwa kupitia mfumo wa FPTP. Mfumo wa kuchagua wawakilishaji wa eneobunge huweza kuweka ukubwa katika ujumuishaji wa makundi ya wachache kwenye mipaka yake au kusawazisha kati ya mapendeleo ya mijini na wilayani. Jinsi wilaya inavyozidi kujitawala ndivyo ambavyo shinikizo la upangaji wake wa uchaguzi lilivyo ndogo ili kuakisi yale mengine ya wilaya au mataifa mengine. Ukweli wa kujitawala kwake hueleza kwamba sifa na mahitaji yake huwa tofauti ikilinganishwa na yale ya maeneo mengine.

