Demokasia ya moja kwa moja ni dhana inayotumiwa kufafanua mambo maalum ya kura kwenye mfumo wowote wa demokrasia. Dhana hii hutumiwa sana kurejelea aina bainifu za kura au vitendea kazi:
- kura ya maoni, ambayo huhusisha maoni kutoka kwa wapigaji kura yanayohitajika na muundo wa kisheria au yanayohitajika na mawaziri au bunge kuhusu swala la sera za umma kama vile marekebisho ya katiba au sheria iliyopendekezwa;
- uwezo wa raia wa kutoa hoja zao, ambao huruhusu idadi fulani ya wanachama kuanzisha kura ya maoni ya wapigaji kura ya kurakuhusu pendekezo liliotolewa na wananchi hao, kwa mfano la kurekebisha katiba, au la kukubaliana, kubatilisha, au kurekebisha sheria iliyopo; au
- kutolewa ofisini, ambako huruhusu idadi fulani ya wananchi kudai maoni ya wapigaji kura kuhusu ikiwa afisa aliyechaguliwa kuhudumia umma anastahili kutolewa ofisini kabla ya kipindi chake cha kuhudumu kukamilika.
Sifa moja inayopatikana kwenye vyombo hivi ni kuwa vyote huwapatia wananchi haki ya kishiriki moja kwa moja katika mchakato wa kufanya maamuzi ya kisiasa. Demokrasia ya moja kwa moja hivyo basi hutazamwa kama yenye kupinga demokrasia ya uwakilishaji ambapo wapigaji kura huchagua wawakilishaji ili wafanye maamuzi kwa niaba yao. Kwa upande mwingine, demokrasia ya moja kwa moja huweza kutazamwa kama njia muhimu, wakati mwingine, ya wananchi ya kurekebisha au kuwekea vikwazo uwezo wa uwakilishaji wa viongozi walioteuliwa, au na serikali kama njia ya kijihakikishia mamlaka ya kutekeleza yale ambayo huweza kuchukuliwa kama hatua zisizofahamika sana.
Mijasala pana imepiga hatu katika kuunga mkono au kupiga vita demokrasia ya moja kwa moja.
Watetezi hudai kuwa demokrasia ya moja kwa moja huweza kusaidia kupunguza uhaba wa ‘kidemokrasia’ ambapo wapigaji kura wanapoteza uhakika na hamu kwenye miundo ya awali ya demokrasia yenye uwakilishaji. Wanadai kuwa kuwarudishia watu uwezo kutawafanya wawe na hamu na majukumu makubwa katika masuala ya utawala, hivyo basi kuongoza uhalali wa mifumo ya kidemokasia.
Kwa kulinganua, wahakiki hudai kuwa hili linapuuza na kudhoofisha serikali yenye uwakilishaji na kuwa kuwapatia watu uwezo ni jambo ambalo linaweza kuhatarisha haki za walio wachache katika jamii. Inadaiwa pia kuwa wapigaji kura wengi hawana uelewa wa kutosha wa kufanya maamuzi kamili kuhusu masuala ya kura ya maoni, hasa kuhusu maswala changamano ya kikatiba. Elimu kwa wapigaji kura na habari kupitia kampeni hivyo basi ni masuala muhimu katika demokrasia ya moja kwa moja
Miongozo ifuatayo inatazama kwa kina aina tatu tofauti za demokrasia ya moja kwa moja huku ikieleza zaidi kuhusu jinsi inavyopangwa na kutolewa, na pia kueleza umuhimu na udhaifu wa kila moja wapo.

