Katika nchi yoyote, uwezo wa mipangilio na uwepo wa binadamu wenye maarifa huweza kushurutisha teuzi zilizopo kuhusu uteuzi wa mfumo wa uchaguzi na pia kiasi cha fedha kinachopatikana. Hata pale ambapo ufadhili na wahisani vinapopatikana, masuala ya uendelezaji (sustainability) wa muda mrefu wa uteuzi wa mfumo wa uchaguzi ni muhimu. Hili hata hivyo haimaanishi kuwa mfumo wa moja kwa moja zaidi na wa gharama ya chini ndio ulio bora kila wakati. Unaweza kuwa uwekevu usio wa kweli, kwani mfumo wa uchaguzi usiotekeleza chochote huweza kuwa na athari hasi kwenye mfumo wa kisiasa wa nchi nzima na pia kwenye uimara wa kidemokrasia. Uteuzi wowote wa mfumo wa uchaguzi huwa na upana mkubwa wa matokeo ya kiuongozi, yakiwemo yale yatakayoshughulikiwa katika yafuatayo.
Mada ndogo za sura hii:
- Mifumo ya uchaguzi na uwekaji wa mipaka ya maeneo ya uchaguzi.
- Mifumo ya uchaguzi na usajili wa wapigaji kura.
- Mifumo ya uchaguzi na muundo na utoaji wa karatasi za kura.
- Mifumo ya uchaguzi na elimu kwa wapigaji kura.
- Mifumo ya uchaguzi na idadi ya siku za uchaguzi.
- Mifumo ya uchaguzi na kuhesabu kura
- Gharama na athari za kiutawala – Hitimisho.

