Tarehe 10 Disemba, 1983, Ajentina ilirudia demokrasia baada ya takribani miaka tisa ya utawala wa kiimla, na tangu wakati huo imekuwa na uchaguzi huru na wa haki. Alfonsin alipohamishia mkanda wa urais kwa Carlos Saul Menem katika mwaka wa 1989, ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya Ajentina kwamba rais aliyechaguliwa kutoka kwa chama kimoja aliuhamishia urais kwa rais mwingine aliyechaguliwa kuwa rais kwa chama kingine.
Katika mwezi wa Aprili 1994, chaguzi zilifanyika kuunda Bunge la Wawakilishi. Katika mabadiliko mengi yaliyofanyika kwenye Katiba ya 1853 kulikuwa na sheria kuhusu kuchaguliwa tena kwa rais, kupunguza muhula wa rais, kuondoa mfumo wa makundi ya wapigakura, na kuidhinishwa kwa upigaji kura wa awamu ya pili katika mazingira mengine. Muhula wa rais ulipunguzwa kutoka miaka sita hadi mine, na awamu ya pili ya upigaji kura kuhitajika ikiwa hakuna kiongozi anayepata angalau asilimia 45 ya kura katika awamu ya kwanza au mshindi ana asilimia 40 ya kura japo tofauti kati yake na aliyemfuata ni chini ya asilimia 10. Hata hivyo, mabadiliko hayakugusia sifa nyingine muhimu za mfumo wa uchaguzi wa Ajentina – majimbo, Usawa katika Uwakilishi (PR), tazama Orodha ya PR, kura za orodha funge, tazama Orodha Wazi, Funge na Huru, na kizingiti cha asilimia tatu ya rejista ya uchaguzi katika kila eneo.
Chini ya katiba mpya, rais, ambaye ndiye mkuu wa serikali, anachaguliwa moja kwa moja kwa muhula wa miaka minne kwa njia ya upigaji kura wa watu wazima. Kongresi ya Taifa ina bunge mbili. Bunge la Manaibu lina wajumbe 257 waliochaguliwa kwa muhula wa miaka minne kwa njia ya usawa katika uwakilishi, huku nusu ya viti hivyo ikibadilishwa kila baada ya miaka miwili. Wanaweza kuchaguliwa tena. Kabla ya mabadiliko hayo, maseneta walichaguliwa walichaguliwa kwa njia ya siri kwa muhula wa miaka tisa na wajumbe wa mikoa. Kwa hivi wajumbe wa Seneti huchaguliwa maeneo 25 ya wajumbe watano katika maeneo yote (mikoa 24 na mji wa Bueno Aires) kwa muhula wa miaka sita, huku thuluthi yao wakiteuliwa tena kila baada ya miaka miwili. Kila mojawapo ya maeneo hayo 25 ya upigaji kura huchagua maseneta watatu moja kwa moja. Viti viwili hupeanwa kwa chama kilichopigiwa kura na watu wengi na kimoja kwa chama kilichoibuka cha pili. Magavana, Mameya wa Manispaa na mabaraza ya miji huchaguliwa kulingana na katiba zao za mikoa au manispaa.
Manaibu pia huchaguliwa kwa njia ya orodha funge, hivi kumaanisha kwamba raia hawaruhusiwi kubadilisha mpangilio wa wagombea au kufuta majina yaliyo kwenye orodha. Aidha, vyama vingi hutumia orodha funge kuteua na kupanga orodha zao. Hadhi na faili ya maelezo kuhusu watu maarufu katika chama husika hivyo basi wana athari muhimu kwenye tabia wa wabunge.
Kila mojawapo ya maeneo 25 ya upigaji kura ina sheria zake za uchaguzi. Isitoshe, inatambulika kuwa mikoa kumi na mmoja hutekeleza ‘kura mbili mwambatano’ kama ilivyo nchini Uruguei. Sheria hii inaruhusu ushindani wa papo hapo katika chama na kati ya kati ya vyama vya kisiasa. Vyama vya kisiasa huwasilisha wagombea mbalimbali wanaoshindana lakini ambao kura zao hujumlishwa pamoja ili kueleza chama kilichopata kura nyingi. Mshindi ndiye mgombea aliayepigiwa kura nyingi katika chama kilichopigiwa kura nyingi.
Sifa mbili za vyama na za kiasasi zilichangia katika kufaulu kwa demokrasia ya Ajentina kutoka kuchipuka kwa demokrasia mwaka wa 1983 hadi wakati wa mabadiliko ya katiba mwaka wa 1994. Kwanza, mfumo wa vyama viwili ulihakikisha kwamba rais anakuwa na idadi ya kutosha ya wabunge katika bunge la kongresi. Pili, wabunge hawa walidhihirisha kiwango cha juu cha nidhamu, hivyo kuwezesha marais kupitisha sheria kwa urahisi.
Hata hivyo, vipengele vingine vine vilivyochochea mabadiliko ya mwaka 1994 vilikuwa vinatatiza utendakazi wa mfumo wa demokrasia. Kwanza, the federal government controlled the flow of resources from the central government to the provinces. Pili, uwezo wa rais kuathiri utendakazi wa tawi la mahakama la serikali ulitatiza mfumo wa kuhakikisha uchunguzi na kuhakikisha usawa. Tatu, orodha funge za vyama kwa chaguzi za wabunge zilisababisha kutotulia kwingi miongoni mwa raia waliodai kuwa wabunge waliwajibikia sana viongozi wao wa vyama vya kisiasa kuliko matatizo ya wanaowawakilisha bungeni. Mwisho, matumizi mabaya ya mamlaka ya urais kuhusu ufaafu na dharura yalipunguza uwezo wa bunge la kongresi kuchunguza utendakazi wa tawi la utendaji la serikali.
Mabadiliko ya katiba ya mwaka 1983 katika mwezi wa Agosti mwaka wa 1994 yalikuwa matokeo ya makubaliano yasiyo ya kawaida bungeni yaliyoidhinishwa kati ya Menem na aliyekuwa rais Raúl Alfonsín. Kwa upande mwingine, lengo kuu la Menem lilikuwa kuchaguliwa tena, na liliafikiwa. Kwa upande mwingine, malengo ya Alfonsin yalikuwa yaliyotawanyika na magumu kuelewa. Kwa kweli alitaka alitaka kutoa mtindo bora wa bunge kwenye siasa za Ajentina. Hii ndiyo sababu ya kubuniwa kwa nafasi ya “Mkuu wa Umma”: ofisa ambaye angeondolewa na bunge la kongresi. Hata hivyo, ujenzi wa ofisi hii haukupunguza mamlaka mengi aliyokuwa nayo rais.
Katika Mei mwaka wa 1995, Rais Menem alishinda uchaguzi tena kwa asilimia 49.8 ya kura, lakini mabadiliko makubwa yalitukia katika mfumo wa siasa: Mrengo wa tatu, FREPASO, uliibuka wa pili na asilimia 29.3 ya kura, hivyo kihistoria kuwaacha wale Asilia katika nafasi ya tatu na asilimia 17 ya kura.
Katika chaguzi za ubunge za Oktoba mwaka wa 1997, wapinzani wa Asilia na FREPASO walijenga muungano ulioitwa “Alianza” katika mikoa mingi ili kushinda chama cha Peronist. Kwa sababu ya chaguzi hizi, Waperonisti hawakushindwa tu katika mikoa mikubwa bali pia walipoteza katika mkoa wa Buenos Aires, ambako takribani asilimia 40 ya raia wa Ajentina huishi. Kiongozi wa FREPASO, Graciela Fernández Mejide, kiongozi wa kutetea haki za binadamu, alikuwa mpinzani mkubwa kwa mgombea wa chama Peronisti ambaye hakuwa amejulikana katika kinyang’anyiro cha urais mwaka wa 1999.
Chaguzi za ubunge za mwaka 1997 ziliibua maswali muhimu kuhusu mazingira ya baadaye ya siasa za Ajentina. Chama kilichokuwa mamlakani wakati huo, Peronist, kilipoteza takribani asilimia 10 ya uungwaji mkono na idadi yake katika bunge la chini, hivyo basi italazimika kuingia katika makubaliano fulani na upinzani kupitisha miswada bungeni.