Bunge la Uswizi lina vitengo viwili, Baraza la Kitaifa na Baraza la Majimbo. Katika Baraza la Kitaifa, majimbo huwakilishwa kutegemea idadi ya watu. Katika Baraza la Majimbo, kila jimbo lina wawakilishi wawili, japo pia kuna nusu-majimbo kadhaa yaliyo na mwakilishi mmoja kila mojawapo. Kwa Baraza la Kitaifa, kuna kanuni sawa za uchaguzi kwa Nchi nzima; kwa Baraza la Majimbo, ni jukumu la kila jimbo kutambua kanuni za uchaguzi almuradi ziwe za kidemokrasia.
Uswizi mpya ilipobuniwa katika mwaka wa 1848, kanuni za uchaguzi za Baraza la Kitaifa zilipendekeza mshindi kuchukua kila kitu katika maeneo ya mpigakura mmoja kama vile FPTP, tazama Kwanza Baada ya Uchaguzi (FPTP). Baada ya Vitaa Vikuu vya Kwanza, kanuni zilizbadilishwa kutegemea usawa katika orodha ya vyama, tazama Orodha ya PR. Hivi sasa, Baraza la Kitaifa lina wajumbe 200 ambao huchaguliwa katika maeneo 26 ya uchaguzi, yanayolingana na majimbo 26 na nusu majimbo ya Uswizi. Jimbo kubwa, Zurich, huchagua wawakilishi 35, na majimbo madogo kabisa, huchagua mmoja pekee. Vyama huwasilisha orodha za wagombea katika kila jimbo zilizo na majina ya wagombea wake kwa kiti cha jimbo hilo. Matokeo huhesabiwa kando kando kwa kila jimbo.
Kwa kuwa na maeneo 26 ya uchaguzi badala ya eneo moja la kitaifa huwa na athari hasi kwa vyama vidogo. Ikiwa Uswizi ingezichukulia kama eneo moja la uchaguzi, ni nusu tu ya asilimia ya kura itakayohitajika kushinda kiti kimoja katika viti 200 vya Baraza la Kitaifa. Kura zinapofanyika katika majimbo 26 tofauti hata hivyo, asilimia kubwa ya kura huhitajika ili mgombea aweze kushinda. Katika eneo loa Zurich, ni lazima chama kishinde takribani asilimia 3 ya kura ili kushinda kimoja katika viti 35 vya jimbo. Katika majimbo madogo yaliyo na kiti kimoja, chama kilicho na kura nyingi ndicho hushinda kiti. Hivyo basi, ikiwa idadi ya viti katika kila eneo inapunguzwa hadi kuwa kimoja, mfumo wa usawa huibuka kuwa mfumo wa mshindi kubeba kila kitu (FPTP).
Kinyume na Nchi za nchini Ujerumani, Uswizi ina idadi ndogo ya kura ambazo chama kinalazimika kupata ili kupata uwakilishi wowote. Hivyo basi, kanuni ya usawa hutumiwa katika mfumo huru.
Wagombea walio kwenye orodha ya chama huwasilishwa na wapigakura bali si vyama. Vyama huwasilisha orodha ya majina bila nyadhifa zao, hasa katika mfuatano wa kialfabeti. Idadi ya majina haiwezi kuwa zaidi ya idadi ya viti vinavyoapaswa kujazwa kutoka kwa kila jimbo. Katika kuorodhesha wagombea wenyewe, wapigakura wana viteuzi vitatu:
- Kuacha jina la mgombea, kama linavyojitokeza kwenye orodha,
- Kumweka mgombea kwenye orodha kwa mara ya pili, au
- Kuacha mgombea kutoka kwenye orodha.
Sharti la pekee ni kwamba jumla ya idadi ya majina haishindi idadi ya viti vinavyopaswa kuchaguliwa kutoka kwenye jimbo. Mpigakura pia anaweza kuamua kutofanya mabadiliko yoyote kwenye orodha hiyo. Katika hali hii, hakuna mapendeleo yatakayofanywa kwa mgombea yeyote, ila kura za idadi ya viti vinavyohusishwa na chama hicho.
Wapigakura pia wanaweza kutatiza zaidi orodha yao kwa kuandika majina ya wagombea wengine kutoka kwenye vyama vingine. Hivyo, mpigakura wa Kisoshalisti anaweza kuweka mgombea wa Demokrasia Huru kwenye orodha hiyo, ama mara moja au mara mbili. Kutokana na uwezo huu wa kuandika ndani, uwekaji wa matokeo kwenye tarakilishi huwa mgumu. Katika mfano uliotolewa hapo juu, Mwanademokrasia Huru huandika hesabu ya wagombea wa chama cha Demokrasia Huru na kutatiza nguvu za yule wa kutoka kwenye chama cha Kisoshalisti; mpigakura atakuwa amezigawa kura zao katika vyama husika viwili. Wapigakura wanaweza kuzidisha kwa kuandika wagombea kutoka kwenye vyama vingi kadiri wanavyotaka, ila pia, idadi ya majina hairuhusiwi kuzidi idadi ya viti katika jimbo hilo.
Uwekaji wa matokeo katika tarakilishi huendelea katika njia ifuatayo: kwa kila jimbo, idadi ya viti ambavyo kilka chama hupokea hutambuliwa kwa misingi ya idadi ya kura za wagombea wa chama hiki. Pili, wagombea hupewa viti hivi kulingana na jinsi walivyofuatana. Nafasi hizi walizochukua hutegemea idadi ya kupatikana kwa jina lake kwenye orodha zote, ikiwa ni pamoja na wale walioandikwa kwenye orodha nyingine za vyama.
Uhuru wa kuteua ambao mfumo wa Uswizi unaruhusu hulegeza udhabiti wa chama dhidi ya wagombea, na hivyo nidhamu huwa chini. Ingawa chama Uswizi bado kinadhibiti uhusishwaji na kutohusishwa kwa mgombea kwenye orodha, hakiwezi kuamua nafasi za mgombea kuchaguliwa kutokana na nafasi yake kwenye orodha. Wagombea wakishaorodheshwa, huwa wako peke yao na hivyo litatakuwa jukum lao kujaribu kurai idadi kubwa ya wapigakura kuandika majina majina yao mara mbili kwenye orodha, na wengi kuwatia alama. Ingawa mfumo huu huonekana kuwapa wapigakura nafasi kubwa, huzidisha pia nafasi ya makundi yenye nia za kibinafsi. Makundi haya huwaelewa wanachama kuhusu wagombea wanaotetea nia zao na wanapaswa kupigiwa kura mbili, na vilevile kuhusu wagombea wanaopaswa kufutiliwa mbali kwa sababu ya kutotetea maslahi yao. Kundi la walimu kwa mfano, litawaeleza wanachama wake ni wagombea wapi wanaojali mahitaji na maslahi ya walimu.Barua hutumwa na makundi makubwa kuanzia kwa wafanyabiashara hadi kwa makundi ya kutetea wafanyakazi na waajiri. Wagombea hutegemea vyama vya kisiasa tu katika kuorodheshwa kwenye karatasi ya uchaguzi; ili kuchaguliwa wanapaswa kupata uungwaji mkono wa idadi kubwa ya makundi mbalimbali yenye nia mbalimbali.
Waswizi bado hupigia kura orodha za vyama, lakini mfumoi wao wa uchaguzi huwaruhusu kutokeza mapendeleo yao ama kwa kuunga au dhidi ya wagombea fulani. Uchaguzi hufanyika katika maeneo madogo ambako wapigakura wanahisi kutulia kuliko katika kituo kimoja cha kitaifa. Vipengele hivi kwa jumla huhujumu uhusiano kati ya wapigakura na wagombea. Kutokana na mfumo huu wa uchaguzi Uswizi sasa hivi ina vyama 14 katika Baraza la Kitaifa.
Kando na kushiriki katika chaguzi, wapigakura wa Uswizi wana usemi mkubwa kupitia kwa kura ya maamuzi, tazama Kura ya Maamuzi. Kwa hakika, katika kura zote za maamuzi za kitaifa zilizowahi kufanyika katika demokrasia za Magharibi tangu kuwepo kwa Vita Vikuu vya II, zaidi ya thuluthi mbili zilifanyika Uswizi. Wapigakura wana haki ya kuitisha kura ya maamuzi kuhusu muswada wowote unaoamuliwa na bunge. Hitaji la pekee ni kwamba zipatikane saini 50,000, ambazo ni rahisi kupata katika nchi ya watu milioni 7. Wapigakura hao wana usemi wa mwisho kuhusu marekebisho ya katiba. Marekebisho yote ya katiba yaliyoamuliwa na bunge ni lazima yawasilishwe kwa wapigakura. Zaidi ya wapigakura 100,000 pia wanaweza kuwasilisha rekebisho lao la katiba, ambalo kwanza litajadiliwa bungeni lakini mwisho liamuliwe kwa kura ya maamuzi. Chombo hiki maarufu cha hatua ya kikatiba hutumiwa sana na inaweza kutekelezwa kwa suala lolote ambalo watu wanataka kufanyia uamuzi. Kura ya maamuzi ilipoanzishwa katika karne ya 19, ilitarajiwa kuwa athari zake zingekuwa bunifu. Waasisi wa kura mpya ya maamuzi nchini Uswizi walikisia kwamba wapigakura wanaweza kufanya mabadiliko, lakini kinyume ndicho kilichofanyika na hivyo matokeo ya kura ya maamuzi huchelewa. Mfano mzuri ni kuingizwa kwa kura ya wanawake katika mwaka wa 1971. Bunge lilikuwa limejitayarisha mapema kushinda wapigakura wa kiume kuwapa wanawake haki ya kupiga kura. Mfano huu ni mwafaka kwa kuwa unaonyesha jinsi inavyochukua muda mrefu kuwakinaisha wapigakura wa Uswizi kukubali wazo jipya.