Katika mwezi Juni mwaka 2004 raia wa nchi 25 za Ulaya walienda katika uchaguzi kuchagua wawakilishi wao katika Bunge la Ulaya. Wengi wao walifanya hivyo kwa mara ya kwanza, huku wengine walikuwa katika nchi nyingine zilizokuwa na tajriba ya miaka mitano ya kuchaguliwa kuingia Bungeni. Katika mwaka, zote zilikuwa zikifanya chaguzi zao chini ya mfumo wa uchaguzi wenye usawa.
Kipande cha kwanza cha sheria kuhusu uchaguzi kwenye Bunge la Ulaya kilipatikana katika mwaka 1976 pale ambapo Kifungu cha Sheria kuhusu Uchaguzi wa Wawakilishi wa Bunge na Kura Bia ya Moja kwa Moja kilikubaliwa. Kama jina linavyoeleza, kifungu hiki cha sheria kiliamua kanuni za chaguzi za moja kwa moja za wawakilishi kutoka kila jimbo. Katika siku za mwanzo mwanzo za EU, wanachama wa Bunge la Ulaya waliteuliwa na bunge katika kila jimbo, bila mchango wa moja kwa moja wa wapigakura. Kupitishwa kwa sheria hiyo mwaka 1976 kulidhihirisha kwamba kuanzia wakati huo wajumbe wangechaguliwa na kura bia ya moja kwa moja katika kila jimbo; na katika chaguzi za kwanza za Bunge la Ulaya zilifanyika katika majimbo tisa wanachama wakati huo – Ubelgiji, Udeni, Ufaransa, Jamhuri ya Muungano ya Ujerumani, Italia, Luxembourg, Uholanzi, Jamhuri ya Ayalandi na Uingereza – hivyo kuishia katika jumla ya wajumbe 410 waliochaguliwa.
Kifungu cha sheria cha mwaka 1976 kilitambua vitu vingi kuhusiana na chaguzi hizi, kama vile urefu wa muhula wa bunge na ufaafu wa wagombea, japo chenyewe hakikubainisha mfumo halisi wa uchaguzi uliopaswa kutumiwa katika chaguzi hizi. Hata hivyo, kifungu hicho kililipa Bunge la Ulaya jukumu la kuunda pendekezo la kuhakikisha usawa katika hatua za uchaguzi. Hadi hatua kama hizo ziafikiwe, kifungu hicho kiliacha hatua za uchaguzi katika vifungu vya kitaifa vya majimbo yake. Kwa kuwa majimbo mengi wanachama wakati huo yalikuwa yakitumia mfumo wa PR kwa njia moja au nyingine kuchagua wabunge wake, ama kibinafsi au kama sehemu moja ya mfumo wa uchaguzi, uteuzi wa mfumo wa uchaguzi wa kutumia kwa bunge la Ulaya ulikuwa sahili. Ubelgiji, Udeni, Jamhuri ya Muungano wa Ujerumani, Italia, Luxembourg na Uholanzi tayari ziliufahamu mfumo wa Orodha ya PR (ila kwa mwakilishi mmoja wa Greenland, kujumuishwa katika uwakilishi wa Udeni, ambaye alichaguliwa na FPTP hadi Greenland ilipotoka katika Jumuiya ya Ulaya katika mwaka 1985). Jamhuri ya Ayalandi iliteua kuwachagua wawakilishi wake kwa kutumia mfumo pendelewa wa STV.
Kulikuwa na vibadala viwili pekee. UK na mfumo wake wa uchaguzi wa FPTP na Ufaransa na mfumo wake wa Awamu Mbili kwa kura chaguzi za kitaifa zote mbili hazikufahamu kuhusu mfumo wa PR. UK iliiga mfumo wa uchaguzi uliotumiwa katika Bunge la Wawakilishi na kuutumia katika chaguzi za Bunge la Ulaya vilevile. Mfumo huu ulipendelea vyama viwili vikubwa Leba na Conservative, vizuri, na kufanya iwe vigumu kwa chama cha tatu kuingia katika ulingo huo. Ukinzani dhidi ya mwakilishi aliyekuwa na mamlaka mawili pia ulichangia katika kuidhinishwa kwa mfumo wa FPTP kwa chaguzi za Bunge la Ulaya katika UK. Ikiwa kuhudumu katika Bunge la Ulaya na Bunge la Uingereza kwa wakati mmoja kusingeruhusiwa, kama walivyotaka baadhi ya wanasiasa wa Uingereza, na aina fulani ya mfumo wa PR pia kuchukuliwa, orodha za vyama zingetokana na wagombea wasiojulikana sio waliochaguliwa kwa shirika jingine lolote la kitaifa au kimtaa, ambalo lingekuwa na hatari ya kuhujumu umuhimu unaotarajiwa kuwa katika uchaguzi.
Mfumo unaogemea, wenye mgombea mmoja, ambapo wagombea watakuwa karibu na wapigakura wao, ulifikiriwa kuwa suluhisho bora. Hakuna mojawapo katika mawazo haya lilifanya kazi Ayalandi Kaskazini. Suala la kuhakikisha uwakilishi wa jumuiya kubwa na ndogo, pamoja na ukeli kwamba vyama vya Uingereza, Scotland na Wales hawapingani kuhusu uchaguzi huko, viliishia katika matumizi ya mfumo wa STV kwa viti vitatu vya Ayalandi Kaskazini. Jaribio lilifanywa kupinga matumizi ya FPTP mahakamani kwa chaguzi za Bunge la Ulaya nchini Uingereza, Scotland na Wales kwa misingi ya mahitaji yaliyopo katika kifungu cha sheria hatua sawazishi za uchaguzi kupendekezwa, lakini hili halikufaulu. Mfumo uliotumiwa Uingereza, Scotland na Wales ulibadilika tu katika mwaka 1999 pale ambapo Sheria ya Uchaguzi wa Bunge la Ulaya ilipopitishwa, kama Uingereza ilivyokisia mabadiliko ambayo yangetekelezwa kwenye kifungu hicho, kama mchakato ulioshia katika uamuzi wa Baraza wa mwaka 2002 (tazama hapo chini) kufanyika. Kuanzia mwaka 1999 na hatimaye, UK ilijiunga na majimbo mengine wanachama katika matumizi ya mfumo wa PR, huku wakiteua Orodha ya PR iliyo na orodha funge na maeneo ya uchaguzi.
Nchini Ufaransa – licha ya matumizi yake ya mfumo wa TRS kwa uchaguzi wa bunge la taifa – mfumo wa Orodha funge ya PR na eneo moja kuu la uchaguzi ulichukuliwa mapema mwaka 1977, kabla ya chaguzi za kwanza za Bunge la Ulaya mwaka 1979. Sababu za kufanya hivi zilikuwa nyingi. Moja katika manufaa makuu ya mfumo wingi – ujenzi wa serikali yenye uungwaji mkono mkubwa – haikuwa wazi na yenye manufaa kwa chaguzi hizi, na uwakilishi wenye usawa wa vyama vyote vya kisiasa ulionekana kama kigezo kingine katika uratibu wa mfumo wa uchaguzi. Wilaya ya kitaifa pamoja na asilimia 5 ya masharti vilifikiriwa kutoa usawa kati ya viwango vya juu vya usawa katika upande mmoja, na haja ya kutenga vyama vilivyo na wafuasi wachache kwa upande mwingine. Uwezo wa kujaza viti vilivyokuwa wazi katikati ya chaguzi na mtu aliyekuwa akifuata kwenye orodha, hivyo basi kuondoa haja ya kufanya chaguzi ndogo, ulikuwa ubora mwingine ulioishia katika kuidhinishwa kwa mfumo wa Orodha ya PR. Baada ya chaguzi tano, haja ya kuimarisha uhusiano kati ya wapigakura na wawakilishi, na haja ya kupata uwakilishi mpana kijiografia (idadi kubwa ya wawakilishi waliochaguliwa bila kuleta usawa walikuwa wakazi wa Paris), viliishia katika wilaya moja ya kitaifa kuachwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2004. Lilibadilishwa na wilaya au maeneo ya wajumbe wanane kwa uchaguzi wa wakilishi 78 wa Ufaransa katika Bunge la Ulaya.
Sehemu nyingine ya sheria muhimu kuhusiana na chaguzi za Bunge la Ulaya ilikamilishwa katika mwaka 2002 kutokana na Uamuzi wa Baraza 8964/02 kurekebisha Kifungu cha Sheria kuhusu Uchaguzi wa Wawakilishi kwenye Bunge kwa njia ya Kura ya Moja kwa moja – marekebisho ya 1976kwenye kifungu hicho cha sheria. Miaka ishirini na sita baada ya uundaji wa kanuni za uchaguzi wa moja kwa moja, uamuzi huu uliweka wazi mfumo mmoja wa uchaguzi kwa chaguzi za Bunge la Ulaya kwa wanachama wote. Kifungu cha 1 kinasema: ‘Katika kila Jimbo Mwanachama, wajumbe wa Bunge la Ulaya watachaguliwa kwa misingi ya uwakilishi sawa, kwa kutumia mfumo wa orodha au kura moja yenye uwezo wa kuhamishwa.’ Kwa chaguzi za mwaka 2004, mataifa yote 25 wanachama hivyo basi yalitumia mfumo wa uchaguzi wa PR.
Ijapokuwa mifumo hii yote ni zao la familia moja, hutofautina katika njia nyingine. Nchi ishirini na tatu (Austria, Ubelgiji, Cyprus, Jamhuri ya Czech, Udeni, Estonia, Ufini, Ufaransa, Ujerumani, Greece, Hangari, Italia, Latvia, Lithuania, Luxembourg, Uholanzi, Polandi, Ureno, Slovakia, Slovenia, Uhispania, Uswidi na UK) hutumia Orodha ya PR, ilhali Malta na Jamhuri ya Ayalandi hutumia STV. Tofauti hii inaweza kutarajiwa, kwa kuwa mfumo wa Orodha ya PR hujenga angalau sehemu ya mfumo wa uchaguzi kwa wabunge wa kitaifa 21 dhidi ya nchi 23 (Ufaransa na UK zikiwa tofauti), huku Jamhuri ya Ayalandi na Malta hutumia mfumo wa STV kwa chaguzi zao za kitaifa. Katika nchi 23 zinazotumia Orodha ya PR, nyingine hutumia orodha funge, ilhali nyingine zimechagua orodha huru – uamuzi ambao mara nyingi huakisi unaofanywa kwa chaguzi za kitaifa, ingawa Greece ni tofauti. Vivyo hivyo, nchi nyingine wanachama, hasa zile ndogi, huchagua wajumbe wake kutoka katika wilaya moja ya kitaifa, ilhali nyingine zimeweka idadi maalumu ya wilaya katika kiwango cha jimbo. Kizingiti cha kupata uwakilishi katika nchi mbalimbali wanachama houtofautian. Uamuzi wa mwaka 2002 unaruhusu nchi kuweka kizingiti chao, japo unaweka mpaka wa kizingiti chochote rasmi kuwa asilimia 5. Nchi nyingine, kwa mfano Cyprus, Hangari na Uswidi, hutumia vizingiti rasmi, pia kwa kuakisi matumizi yake katika kiwango cha kitaifa (ingawa Ubelgiji, ambayo hutumia kizingiti rasmi kwa chaguzi za kitaifa, haifanyi hivyo katika chaguzi za Bunge la Ulaya). Si vizingiti rasmi tu, bali pia kiwango hasa cha ufuasi kinachohitajika ili kupata uwakilishi – vizingiti asilia- hutofautiana kati ya nchi wanachama. Sababu ya tofauti hizo katika vizingiti hupatikana katika kuunganisha idadi fulani ya wawakilishi waliochaguliwa kutoka kila nchi na kiwango cha kuelezwa kwa maeneo ya uchaguzi (hasa, idadi ya wawakilishi wanaopaswa kuwakilishwa kutoka kila wilaya). Italia, iliyo na wilaya moja pana ya kitaifa na wawakilishi 78 wa kuchagua, ina vizingiti vichache chini ya asilimia 1, huku maeneo manne ya uchaguzi na wawakilishi 13 wa Jamhuri ya Ayalandi huashiria kwamba mgombea anayefaulu chini ya mfumo wa STV atahitajika kushinda sehemu kubwa ya kura. Katika mwaka 2004, wagombea wanaoshinda nchini Ayalandi walipata kati ya asilimia 12.9 na 25.9 ya kura za kwanza za mapendeleo katika wilaya yao.
Ijapokuwa mfumo mmoja wa uchaguzi sasa hupendekezwa kwa chaguzi za Bunge la Ulaya, kuna dalili chache sana za uwepo wa nafasi ya kuunganika zaidi. Ingawa makundi ya vyama hubuniwa katika Bunge la Ulaya, hakuna dalili kwamba vyama vya kitaifa vina nia ya kuachilia vyama Umoja Ulaya. Kwa hivyo, kuna uwezekano kwamba maamuzi kuhusu maelezo ya kina kuhusu mfumo wa uchaguzi yatasalia kuwa jukumu la wanasiasa wa kitaifa, wanaochochewa na nia zao za kibinafsi na mazoea yaliyopo ya kitaifa. Mijadala inaonekana kuelekea kwenye idadi ndogo inayojitokeza katika chaguzi za Bunge la Ulaya, ambayo ni suala muhimu kwa nchi wanachama za EU. Licha ya matumizi ya mfumo wa PR katika nchi zote – familia ya mfumo wa uchaguzi huhusishwa na idadi kuwa ya wapigakura wanaojitokeza kushinda mifumo mingine yoyote ile – idadi ya wanaojitokeza inaendelea kuwa ndogo. Katika uchaguzi wa mwaka 2004, nchi 15 zilizokuwa wanachama kabla kupanuliwa katika mwaka 2004 hadi jumla ya asilimia 52.9 na wanachama wapya 10 kuwa na idadi ya chini kabisa kufikia asilimia 40.2. Inaonekana kuwa kadiri wapigakura wanavyoendelea kuziona chaguzi za Bunge la Ulaya kama za ziada, zilizo na uwazi mdogo sana kuhusu mabadiliko yanayopatikana uwakilishi unapobadilika kutokana na chaguzi, nia na kujitokeza kwa wapigakura huendelea kuwa chini. Mifumo ya uchaguzi inayotumika haitazamwi kama kipengele zushi, na kuna mjadala mdogo kuhusu marekebisho yake. Inawezekana hivyo basi kuwa mifumo ya uchaguzi itasalia kuwa vilevile katik siku za baadaye.