Kanuni kuu
zinazotawala mifumo ya utawala ya uchaguzi lazima iwekwe katika kiwango cha
kikatiba. Chini ya mpango huu, kanuni zinazochukuliwa kuwa duni lazima zibuniwe
ili kuzua habari na matumizi ya kanuni za kikatiba. Siku hizi hakuna kanuni
dhahiri za kufuata ili kujua mada zipi zimehusishwa katika katiba. Uamuzi kama
huu unategemea hali tofauti zilizoko katika kila nchi. Hivyo basi mada
zilizowekwa mara nyingi na katiba ni kanuni za kimsingi za muundo wa serikali,
juu ya wakala wawakilishi wanapaswa kufungamanishwa, juu ya haki za kimsingi
pamoja na mbinu za kisiasa zinazoweza kutumiwa kuwalinda, juu ya kanuni kuu
zinazotawala mfumo wa uchaguzi,juu ya sifa kuu zinazodhihirisha upigaji kura,
juu ya kuwepo kwa vyama vya kisiasa na utawala wao wa kindani (inahusisha mada
kama ufadhili) juu ya kuwepo kwa mamlaka yanayotawala uchaguzi na mahakama za
uchaguzi na juu ya aina za kanuni za kitaratibu zinazopaswa kufuatwa.
Kulingana na
kiwango cha uchangamano wa kanuni zinazotumiwa kufanya marekebisho na hata
ingawa mara nyingi katiba zinapaswa kukaa kwa muda mrefu ili kusababisha
hakika, mifumo ambayo haibadiliki inatofautishwa na inayoweza kubadilishwa.
Kanuni
nyingine za kimsingi zinaweza kuwekwa katika katiba ili kuhakikisha kuendeshwa
kwa uchaguzi huru, wa kweli na wa baada ya kipindi maalumu katika kila nchi
zinaweza kuorodheshwa kama ifuatavyo: haki ya kupiga kura ni haki ya watu wote
na ni lazima itumiwa kwa njia huru, ya siri na ya moja kwa moja; uchaguzi
lazima usimamiwe na shirika huru; uchaguzi lazima uendeshwe kisheria, kwa njia
huru, isiyo na ubaguzi wala mapendeleo yoyote; wagombeaji na vyama vya siasa
lazima zipewe nafasi sawa ya kuvifikia vyombo vya habari; kila amri ya uchaguzi
lazima irekebishwe kisheria ili kuthibitisha kwamba ni ya kikatiba na halali.
Katiba
lazima ionekane kama kanuni kuu ya serikali yoyote, hapa tunadai kuwa ni ya
lazima na ni lazima iwe na mamlaka na iheshimiwe vilevile. Kanuni za kuongoza
uchaguzi zilizowekwa na katiba si za kinadharia bali ni kanuni ambazo ni lazima
zizingatiwe na utawala wa kikatiba na kidemokrasia.
Vilevile kwa
kuwa katiba ndiyo sheria kuu katika mfumo wa kisheria inahalalisha kanuni zilizo
katika mfumo wa kisheria. Kanuni za kikatiba haziwezi kukiukwa ama kupuuzwa na
kanuni zisizo za kikatiba.Ukiukaji wowote wa katiba unaotokana na kanuni zisizo
za kikatiba ni batili.
Kuna aina
mbalimbali za halmshauri za kusimamia uchaguzi. Hata hivyo, asasi huru za
kikatiba mara nyingi huwa zimeimarishwa. Asasi hizi mara nyingi huwa mamlaka ya
juu ya uchaguzi na huwa huru kabisa kutokana na tawi lolote la kitamaduni la
kiserikali.
Siku zetu,
kubuniwa kwa tume za kikatiba kumepewa hadhi ya juu. Tume kama hizi zimepewa
mamlaka ya kueleza na kusimamia sheria za kikatiba tukirejelea haya, kwa kuwa
mada za uchaguzi zimetambulika kikatiba sio tu kwa kuzua tume za kikatiba
ambazo zimejikita katika kutatua mizozo ya uchaguzi lakini kupanuliwa kwa
mamlaka ya tume za kitamaduni za kikatiba kufanya hivi, inaonekana kuwa ya
kukubalika.
Mifumo ya
muungano hufanya kazi chini ya mradi wa uwili kwa upande mmoja katiba za
muungano huibua mada za kisiasa ambazo zimepelekwa kwa kiwango cha muungano.
Kwa upande mwingine, japo ni lazima serikali zitumie uhuru wake kisheria kuweka
sheria za uchaguzi, zinalazimika vilevile kufuata kanuni zote za kiuchaguzi
zilizowekwa na katiba za muungano.
Kujumuishwa
kwa mada za kiuchaguzi katika katiba haimaanishi kuwa makala mpya za kikatiba
lazima ibuniwe. Nyongeza kama hiyo inaweza kufanyika kwa kufanya mikakati na
marekebisho maalumu ya kimtindo.