Sheria za uchaguzi ni chombo cha kisheria kinachotumiwa kuzua mada nyingi za
uchaguzi zinazoihusu nchi hasa katika nchi hizo zinazofuata sheria za
kitamaduni za kiraia. Sheria za uchaguzi huwekwa na wanasheria wa kawaida
(matawi ya kisheria ya serikali, mabaraza, bunge) ili kuibua kanuni za jumla
zilizowekwa kwenye katiba.
Kwa kawaida, kwa kuwa lazima mifumo ya uchaguzi iwe halali, thabiti na
ya kudumu, sheria za uchaguzi lazima ziwekwe na angalau thuluthi mbili ya
wanachama wa baraza.
Hakuna muundo wa kufuata ili kuweka sheria za uchaguzi ama njia ya kufuata
kuhusu yaliyomo na muundo wake katika nchi nyingine kwa mfano sheria na
uchaguzi huwekwa katika kipande kimoja cha sheria (kanuni au sheria) ilhali
nyingine kanuni na sheria nyingi huwa na kanuni za uchaguzi kwa njia mahsusi
(katika hali kama hizi kuna kanuni maalum zinazotawala mamlaka ya uchaguzi,
vyama vya kisiasa, mfumo wa vifaa na mambo kama hayo).
Chini ya katiba, sheria za uchaguzi zinaweza kutawala mada za uchaguzi
ifuatavyo:
- Kuhusishwa
kwa ofisi za wawakilishi;
- Haki ya
watu binafsi ya kupiga kura, kupigiwa kura ,kuhusiana kwa njia huru na
wengine na kujiunga na vyama vya kisiasa;
- Sifa za
mfumo wa kupiga kura;
- Matakwa
ambayo ni lazima yanashughulikiwa na wagombeaji waliochaguliwa;
- Kanuni za
kisheria za vyama vya kisiasa (kama matakwa yanayopaswa kutimiza
kusajiliwa haki na majukumu ya wanachama, ufadhili, muungano na
mengineyo);
- Sifa kuu
za mamlaka ya uchaguzi (kama muundo, mipango na mamlaka);
- Taratibu
za uchaguzi (kampeni, siku ya uchaguzi, kuhesabiwa na matokeo ya
uchaguzi);
- Uchaguzi
na vyombo vya habari;
- Adhabu;
na mfumo wa rufaa;
Nchi zilizo na mahakama maalumu za kikatiba zinaweza kuidhinisha sheria za
uchaguzi zinazoweza kupingwa kikatiba. Mahakama kuu ya nchi itapewa mamlaka ya
kuamua kuhusu mizozo kama hii.
Kwa kawaida, mabadiliko makubwa kwa sheria za uchaguzi hayawezi kufanywa
ikiwa uchaguzi uko karibu kuanza. Kidhibiti hiki hunuia kulinda uthabiti wa
kisiasa na hakika ya kisheria.
Sheria za uchaguzi haziwezi kuwekwa kurejelea kanuni za uchaguzi
zinazohusiana na masuala ya utawala halisi au ya kindani na mamlaka ya
uchaguzi. Kanuni kama hizi lazima ziwekwe katika vyombo vingine kama sheria.