Mfumo wa uchaguzi ni kiambajengo muhimu cha kikatiba yoyote ya kisheria kwa sababu mfumo kama huo hueleza kufungamanishwa kwa waliochaguliwa katika ofisi za umma na uhusiano kati ya vyama vya kisiasa katika nchi na, serikali ama katika nchi nyingi.
Kwa jumla mfumo wa uchaguzi unaweza kuielezewa kama kanuni za kuwachagua ofisa wa umma. Katika maelezo mengine mfumo wa uchaguzi unaweza kuonekana kama udhabiti wa uhusiano kati ya kupiga kura na wawakilishi waliochaguliwa. Mfumo wa uchaguzi hivyo basi ni njia ambayo kura zinabadilishwa na kuwa wawakilishi waliochaguliwa na ujumbe wao wa kisiasa hivyo basi ni wazi kanuni kama hizi huonekana kuwa kanuni muhimu sana.
Mpangilio wa mfumo wa uchaguzi huonekana kwa njia iliyodhibitiwa, inarejelea sio tu uendelezo wa mfumo wa bunge, bali pia uendelezo wa himaya za kikatiba. Kuhusiana na uchaguzi wa wawakilishi wa umma, uchaguzi wa mfumo wa uchaguzi ni muhimu. Ikiwa mfumo wa uchaguzi unafuata kanuni ya zaidi ya nusu ya watu basi wagombeaji wanaopata kura nyingi kabisa hutangazwa kuwa washindi. Kwa upande mwingine, mshindi anapochaguliwa katika raundi ya pili kutoka kwa mshindi wa awamu ya kwanza na wa awamu ya pili ama mshindi anapochaguliwa kupitia njia isiyo dhahiri (kama inavyotukia Marekani) matokeo yanaweza kuwa tofauti.
Kando na hayo, mfumo wa uchaguzi hauhusu tu njia ambayo kura zinageuzwa na kuwa viti bungeni lakini pia zinaweza kuathiri vipengele vingine vya mfumo wa kisiasa kuwakilishwa kwa mitazamo tofauti ya jamii, sifa kuu za kampeni za uchaguzi, uwezo wa himaya za kisiasa kuwapa watu binafsi asasi za kisiasa zinazofanya kazi na mifumo ya kisiasa halali. Mifumo ya uchaguzi inaweza kuwa muhimukuwaleta pamoja viongozi na wananchi (kupitia mbinu kama uwajibikaji, uwakilishi na kuwajibika kisiasa). Kwa yakini mfumo wa uchaguzi huzua matokeio muhimu kwa serikali za kidemokrasia baada ya muda. Vichocheo lazima viwepo ili kuwasaidia wanaogombea kuomba kura kwa njia nyingi. Kulingana na uhalisia wa kijamii na kisiasa (katika jamii kuna tofauti kuu za lugha, imani za kidini, kimbari au kijamii na mfumo maalumu wa uchaguzi unapaswa kuwezesha na kupendekeza ushirikiano na mawazo ya mapatano. Kutoka kwa wagombeaji na vyama vya kisiasa huku wakiwaadhibu wale ambao hawashirikiani na wengine ama kuleta mapatano).
Mifumo ya uchaguzi lazima izingatie sheria za kikatiba na sheria nyingine. Kama tulivyosema mipango ya mifumo ya uchaguzi huzua njia ambazo kura hugeuzwa na kuwa ofisi za umma. Yaani mpango huamua kura zinavyouathiri uwakilishi wa kisiasa. Hii ndiyo sababu kanuni za mfumo wa uchaguzi huanza katika kiwango cha kikatiba na huendelea kwacha kisheria.
Sifa nyingine hubainisha vipengee vya kimsingi kuhusu mfumo wa uchaguzi (kwa upande mmoja zinaathiri njia ambayo kura zinageuzwa na uwakilishi wa kisiasa, unaweza kubainishwa kutoka kwa nyingine kulingana na maamuzi ya kisiasa yanayoeleza kila moja yazo). Kwa kuzingatia haya tunaweza kusema kuwa vipengee vya kimsingi vya mfumo wa uchaguzi ambayo lazima yahusishwe katika sheria za uchaguzi kama ifuatavyo:
- Mgao wa kimaeneo kwa minajili ya uchaguzi ambao unarejelea maeneo ya kijiografia inayotumiwa kugeuza kura kuwa viti bungeni.
- Mfumo wa uchaguzi (ambao unaweza aidha kuatambua wengi ambao wanaweza kuwa –sahili, kamili ama wanaostahili- au uwakilishi wa uwiano).
- Utaratibu wa hisabati ambao lazima utumike ili kugeuza kura kuwa viti vya bunge.
- Vizingiti vya uchaguzi ambavyo lazima vionekane kama asilimia ya chini ya kura ambazo lazima kila mgombea anapaswa kupata ili ahusishwe katika ugawaji wa viti vya bunge.
- Jinsi ambayo uchaguzi unaendeshwa (dhahiri au isiyo dhahiri) inayorejelea uwezo wa wapiga kura na uwezo wa vyama vya kisiasa kutambua ni nani atakayechukua ofisi za umma.
Uchaguzi wa mfumo wa uchaguzi lazima uwekwe katika taratibu za kisheria ambazo hudhibiti miundo ya kijamii na tofauti za kisiasa kwa njia inayotosheleza. Kanuni kama hiyo lazima iunde uwakilishi wa mfumo wa kisiasa ulio na mamlaka ya kutatua mizozoya kijamii kupitia mapatano. Inaweza kusemwa kuwa, hivyo basi, uchaguzi wa mfumo wa uchaguzi hufanywa kwa urahisi zaidi ikiwa malengo yaliyochaguliwa mwanzoni (kiwango kikubwa zaidi cha kuaminika kwa mfano, uwiano wa matokeo, uwakilishi dhabiti wa vikundi vya kisiasa katika kiwango cha kieneo na mengineyo). Kulingana na mawazo, na kurejelea hali iliyoko kijamii, kisiasa, kijiografia na kihistoria ya kila nchi, mifumo ya uchaguzi lazima iteuliwe.
Uchaguzi wa mfumo wa uchaguzi ni uamuzi muhimu kwa mtazamo wa asasi. Uamuzi huu ni muhimu sana kwa matokeo ya kutosheleza ya demokrasia yoyote. Mfumo wa uchaguzi unaweza kusaidia sio tu kuzua matokeo maalumu bali pia kupendekeza ushirikiano na mapatano ya jamii zilizotengana.
Shughuli ya kuchagua mfumo wa uchaguzi unaunga utaratibu wa kisheria wa uchaguzi. Kutumiwa kwa mfumo maalum wa uchguzi katika kila nchi unaweza kuwa na athari ya maana katika matokeo ya kiuchaguzi ya baadhi ya wagombeaji. Kutathminiwa kwa mfumo wa uchaguzi wa nchi kunaweza kuzingatia matokeo yaliyopatikana kutokana na uchaguzi wa awali. Kufanya hivi, kunaweza kufafanua masuala muhimu kama manufaa yake ikiwa yapo.tyanapokelewa na chama cha kisiasa kilicho uongozini unapolinganisha na vyama vingine vya kisiasa. Ufafanuzi pia unaweza kufanywa kwa viambajengo vya mfumo ambao unaweza kuchukuliwa kama kuzuga kanuni za kimataifa ama matokeo ya uchaguzi.
Hakuna mfumo wa kisiasa ambao unaweza kutumiwa katika hali zote. Kanuni yoyote inayoweza kutumiwa kote. Uchaguzi wa mfumo wa kisiasa unapaswa kuazimia malengo wazi na huweza kuchukuliwa kama uamuzi wa mkutano wa dharura. Matokeo yanayotokana na taratibu za mfumo wa uchaguzi ni za kimuktadha na hutegemea upekee wa kisiasa na kimaeneo pamoja na uhalisia tofauti wa kijamii na mizozo maalumu yanayotofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Athari za kijumla za kila mfumo wa kiuchaguzi hutegemea muktadha unaotofautisha kila kesi.
Kusahihishwa kwa mfumo wa uchaguzi kunapaswa kurejelea ikiwa nchi imegika sana ama la kutokana na mitazamo ya kisiasa, kijiografia, kidini ama kimbari. Lazima irejelee iwapo walio wachache wanawakilishwa kwa njia ya haki katika mfumo wa kisiasa. Kurekebishwa kwa mfumo wa uchaguzi kunanuia kuboresha utawala wa nchi kiuchaguzi, lazima irejelee mapendekezo yanayotokana na matukio ya nchi nyingine na jinsi makosa yalitatuliwa.