Usimamizi wa uchaguzi ni muhimu na lazima ili kuunda taratibu za kisheria. Iwapo usimamizi unafaa basi uchaguzi pia utafana. Ili kuwa na usimamizi unaofaa na kuleta matokeo yanayofaa matakwa kadhaa lazima yatimizwe kama yafuatayo: Kwanza, sheria za uchaguzi zishungulikie kila kiwango, kitengo, tendo na taratibu ili kuzuia makosa (yoyote ama hatia; pili viongozi wa uchaguzi wapangwe kulingana na nchi au eneo kisiasa na upekee wa kijamii viongozi kama hawa wapewe mamlaka ya kiasasi ya kutekeleza waibu wao chini ya kanuni za kijumla zinazotawala taratibu za kiuchaguzi; uhakika, uhalali, uhuru, uadilifu na kutobagua.
Utendakazi wa kufana na unaoleta matokeo yanayofaa ya usimamizi wa uchaguzi ni kipengee muhimu cha uchaguzi wowote.
Kwa kuzingatia haya, mahitaji ambayo halmashauri za kusimamia uchaguzi zinapaswa kutimiza na yameelezewa chini ya mada Mpangilio wa Uchaguzi na yanaelezwa ifuatavyo:
- Matokeo ya kitaalamu na huru kulingana na vyama vya kisiasa vilivyo mamlakani lazima wagombeaji wote wahudumiwe bila ya ubaguzi.
- Kila mgombeaji atambue kutoegemea upande wowote kama sifa moja ya kubainisha.
- Utendakazi wao uwe wa kuleta matokeo yanayofaa na wapewe msaada wowote wa kiraslimali ili waweze kutimiza majukumu yao.
- Utendakazi wao uhusiane kwa karibu na mifumo ya kisheria unaotawala kuwepo kwao. Wasimamizi wa uchaguzi watathminiwe na watahini wa kutoa na huru ambao wanaweza kuwa wa kisheria.
Mara nyingi uaminifu huhusishwa na mamlaka. Hivyo basi imani ikiwa kidogo kwa mashirika ya umma imani kwa viongozi wa uchaguzi utaongezeka. Hali kama hii siyo ilivyo kwa mashirika ya kidemokrasia yaliyoimarishwa. Kwa hakika wasimamizi wa uchaguzi wanaweza kuwekwa katika makundi yafuatayo:
- Kuna nchi ambazo usimamizi wa uchaguzi umewekwa katika viongozi wa kawaida (kitaifa au kimtaa) wakati mwingine, mifumo ya marekebisho. Hayabadilishwi kama viongozi wa kawaida wanonekana kuwa waaminifu, waadilifu, wasio na ubaguzi.
- Kuna nchi ambazo bodi za uchaguzi huundwa ili kurekebisha usimamizi wa uchaguzi uliofanywa na Tawi Kuu la Uongozi la Serikali. Bodi kama hizi hazipewi mamlaka ya kusimamia taratibu za kiuchaguzi.
- Kuna nchi ambazo kitengo maalamu za uchaguzi katika tawi za kitamaduni za serikali zilizopewa mamlaka ya kupanga uchaguzi.
- Kuna nchi ambazo kiwango cha imani kipo chini mpaka viongozi huru wa kusimamia uchaguzi huwekwa katika katiba. Viongozi hawa hawaondoi usimamizi wa serikali wa uchaguzi bali pia wanakataza mwingilio wowote wa mashirika ya serikali, kwa yakini wanaonekana kama tawi la nne la serikali. Kubuniwa kwa viongozi huru wa uchaguzi huonekana kamahatua muhimu katika kuundwa kwa usimamizi wa kiuchaguzi usio na ubaguzi unaoaminika na wapiaji kura vyama vya kisiasa.
Utendakazi mwema na kuaminika kwa halmashauri huru ya kusimamia uchaguzi hutegemea sio tu kuwepo kwa fedha za kutosha bali pia kuwepo kwa wafanyakazi huru wasio na ubaguzi wa kuifanyia kazi.
Usimamizi wa chaguzi za kidemokrasia huhitaji halmashauri huru na zisioegemea upande wowote, ambazo ni huru dhidi ya misukumo au mapendeleo yoyote ya kisiasa. Hili ni suala muhimu, hasa kwa nchi ambazo utawala wa kidemokrasia bado haujaimarishwa. Kuna wasimamizi wa uchaguzi ambao huchukua na kufanya uamuzi muhimu unaoweza kuathiri matokeo ya uchaguzi. Hivyo basi, hali mahususi za kisiasa lazima zitiliwe maanani ili kujua ni nani atasimamia uchaguzi na ni asasi zipi zitapewa mamlaka ya kufanya hivyo.
Maamuzi kama haya ya kisheria lazima yabainishe ukubwa nba kufungamanishwa kwa halmashauri za kusimamia uchaguzi. Uamuzi wa kisheria utabainisha ni nani atateuliwa na uteuzi na kufutwa kutoka kwa uteuzi huo utakavyofanywa. Mada kama hizi huamua utendakazi na viongozi vya uchaguzi. Kuhusishwa kwa halmashauri za kusimamia uchaguzi kunapaswa kuzingatia masuala yafuatayo:
Muundo
Muundo wa usimamizi lazima uhusishe maajenti wa uchaguzi uwe wa kati ama wa kitaifa. Kunaweza kuwa na wakala wa nchi katika kiwango cha jimbo ama eneo. Kulingana na upanuzi wa mamlaka ya kusimamia uchaguzi na upanuzi wa mifumo ya mawasiliano hata kunaweza kuwa wakala wa uchaguzi wa wilaya. Kuna wakala wa kati wa uchaguzi walipo mradi mfumo wa uchaguzi, hali ya kijiografia na idadi ya watu katika nchi uraruhusu. Hata hivyo, ni muhimu kuzuia kubuniwa kwa mashirika duni ya uchaguzi. Mashirika duni na yasiyohitajika huwa na athari wazi: huongeza hela zinazotumiwa katika uchaguzi.
Muundo wa uchaguzi huundwa kwa kuzingatia vipengele vya uchaguzi. Vipengele vya uchaguzi ndio msingi wa muundo wa uchaguzi. Jukumu muhimu la utaratibu wa uchaguzi ni kubainisha kwa njia wazi ni nani atafungamanisha vipengele vya uchaguzi na vinavyohusiana na ofisi kuu na viongozi wa uchaguzi. Mfumo wa Kisheria pia lazima ubainishe aina ya uhusiano ambapo vipengee vya uchaguzi vitakuwa nao na halmashauri za kiserikali katika siku ya uchaguzi.
Mamlaka na kuwajibika
Mamlaka ya viongozi wa uchaguzi na uwajibikaji wao lazima uandikwe kwa sheria kwa njia wazi. Sheria kama hii inafaa kuhusisha mada zifuatazo:
Muundo na uhusika, majukumu ya kisheria yatakayotimizwa, maofisa wangapi watahitajika ili kuziwezesha halmashauri za kusimamia uchaguzi kufanya kazi, taratibu za uchaguzi, uhusiano; kurejelewa kwa taratibu zinazodhibiti kuendelezwa kwa mamlaka ya kisheria.
Matakwa ya uhusika
Mradi tu iwezekane, inapendekezwa kuteua wataalamu wanaojua mfumo wa kisheria unaodhibiti usimamizi wa uchaguzi. Kwa kawaida inatakikana angalau baadhi ya watu wanaofungamanishwa na uongozi wa uchaguzi wawe wataalamu wa kisheria. Matatizo yanayoathiri viongozi wa mamlaka ya chini yanaweza kutokana na kigezo kinachokubalika. Viongozi wa uchaguzi kufungamanishwa na wawakilishi wa vyama vya kisiasa pia kunaweza kuzua changamoto. Uhuru na uadilifu wa viongozi wa uchaguzi kufungamanishwa na viongozi ama majaji walioteuliwa na chama kinachotawala pia kunaweza kupotezwa. Suluhu bora inaweza kupatikana katika hali ambazo vyama vya kisiasa vina mamlaka ya kuyaeleza mawazo yao mbele ya viongozi wa uchaguzi, bila ya mamlaka ya kutimiza jukumu lolote katika kutatua masuala yoyote ya uchaguzi.
Uteuzi wa wakala wa kuaminika wa kisiasa kama vile mashirika yasiyo ya kiserikali na wanachama wa Tawi la Kisheria la Kiserikali ili kuchukua ofisi za uchaguzi ni chaguo zuri.
Masharti
Viongozi wa uchaguzi lazima wakae kwa muda mrefu katika nchi nyingine wanapewa ruhusa ya kufanya kazi katika kipindi cha wakati. Licha ya hayo, kazi yao ya muda ni muhimu pale ambapo wanasimamia orodha ya wapiga kura. Katika hali kama hii matendo ya muda ya viongozi wa uchaguzi lazima yawe ya kisheria. Orodha ya wapigakura lazima iwepo kwa kila uchaguzi. Mara nyingi halmashauri za kiwango cha chini za kusimamia uchaguzi, kama vile wanaosimamia maeneo madogo ya uchaguzi au wanaosimamia maeneo ya kupiga kura si wa kudumu, wanapewa fursa ya kazi mwanzoni mwa kipindi cha uchaguzi na kufungiwa kazi pindi matokeo ya uchaguzi yanapoidhinishwa.
Mashirika ya uchaguzi yanapaswa kurekebishwa visehemu vyake au kwa kiwango fulani. Si wazo la busara kuzipa halmashauri za kusimamia uchaguzi muhula mpya kila mara. Kwa hakika, tajiriba inaweza kutusaidia kuongeza matokeo ya asasi. Taratibu zote na vipengee vinavyounga uteuzi na kuondolewa lazima ziwekwe katika sheria ili ziwakinge wanachama wa mashirika ya uchaguzi kutokana na nguvu za kisiasa. Ujira wa maofisa wa kusimamia uchaguzi si lazima utoke kwa serikali. Nchi nyingine huwapa maofisa wa kusimamia uchaguzi kinga ili watekeleze wajibu wao.
Ufadhili
Halmashauri za kusimamia uchaguzi lazima zibuniwe na kujumuishwa kabla ya uchaguzi kufanyika chini ya sheria. Licha ya hayo, lazima zipewe ufadhili wa kutosha ili zitelekeze wajibu wake. Mifumo ya kisheria lazima zihusishe kanuni wazi na zisizo na maendeleo juu ya matendo ya muda ya viongozi wa uchaguzi yatafadhiliwa ili kukataza bajeti kuwa chombo cha kisiasa kinachotumiwa na bunge, vyama vya kisiasa au Serikali dhidi ya halmashauri za kusimamia uchaguzi.
Mamlaka na Majukumu
Mamlaka na majukumu ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi lazima yawekwe katika sheria kwa njia wazi. Sheria wazi ya uchaguzi itachangia pia katika kuleta usimamizi unaosababisha matokeo yanayofaa kwa halmashauri za kusimamia uchaguzi.
Halmashauri za kusimamia uchaguzi lazima ziwe huru, wazi na zisizo na ubaguzi. Pindi halmashauri ya kusimamia uchaguzi ikishabuniwa, lazima itekeleze majukumu yake na kutumia mamlaka yake bila mapendeleo. Kila mfumo wa kisheria hulenga kuziongoza halmashauri za kusimamia uchaguzi kuhusu jinsi zinavyopaswa kuendesha uchaguzi huru na wa haki. Katika kufanya hivi, halmashauri za kusimamia uchaguzi zinapaswa kutekeleza majukumu yake katika njia ya kutosheleza na isiyo na mapendeleo.
Miongoni mwa sifa bainifu muhimu za halmashauri ya kusimamia uchaguzi, baadhi zinaweza kuorodheshwa ifuatavyo: a) Uhuru na kutokuwa na ubaguzi; b) Utoshelezi na utendakazi mwema; c) Utaalamu, Uzingatifu wa Sheria na Kutopendelea; na d) Uwazi
Kwa kuzingatia haya, ni muhimu kutambua kwamba mfumo wa uchaguzi unapojipata katika kiwango cha kuimarishwa, ni muhimu kujibu maswali kadhaa yanayotokana na kuwepo kwa mashirika huru na ambayo yanahusiana na fedha zilizopo.
Bila shaka, ili kuchagua shirika huru kutoka kwenye mamlaka asilia ndiyo mbinu bora kwa nchi zinazokuwa na mapinduzi ya kisiasa. Hata hivyo, uteuzi kama huu unaweza kuzua maswali mengine hatimaye. Kadiri mapinduzi yanavyofaulu kuwa ya kidemokrasia, ndivyo halmashauri ya kusimamia uchaguzi itakavyoendelea kukosa umuhimu wake. Hii ni kweli hasa katika nchi ambayo mfumo kamili wa sheria zipo na zinafuatwa na kuimarishwa. Hali hii ya kuchunguza au kupima huwakilisha uwepo maongozi ya kisheria na kuimarika kwa imani ya umma kwa mashirika ya kuhudumia umma. Mbali na hayo, kuwa na halmashauri huru ya kusimamia uchaguzi katika hali kama hizo kunaweza kuwa ghali sana.
Kwa hakika, halmashauri za kusimamia uchaguzi huwa asasi ghali sana. Zinaweza kuonekana kuwakilisha matumizi mengi bila ya mazao katika mfumo wa jumla wa kuhudumia umma zinazotolewa kwa wanaolipa kodi. Katika nchi zingine, demokrasia huchukuliwa kama kitu muhimu sana na pesa za umma zinazotumika kulipia asasi za kiuchaguzi huonekana kutumika njema. Kwa kawaida, uchaguzi wa kufana huonekana si kwa mtazamo wa kifedha. Hili huwa ukweli hasa pale ambapo gharama za uchaguzi zimefadhiliwa kupitia muungano wa kimataifa. Hata hivyo, pindi shughuli za uchaguzi zinapokuwa bora na za kufana, tawala za kidemokrasia zinavyoimarika na ufadhili wa kimataifa kupungua, mazingatio ya kifedha huwekwa katika kituo kimoja kikuu. Katika hali kama hizi, uwekaji wa demokrasia katika nchi unapaswa kujiuliza iwapo gharama za uchaguzi zimezidishwa au la.