Haki ya kupiga kura lazima ichukuliwe kama haki ya kushiriki katika shughuli za umma kwa njia ya moja kwa moja. Hivyo basi, haki hii inapaswa kutungwa katika kiwango cha juu cha kisheria (katika Katiba kwa mfano) na ya muhimu kabisa. Haki ya kupiga kura lazima ichukuliwe kama ya muhimu katika katiba yoyote ya kidemokrasia. Katiba nyingi ulimwenguni hudhibiti umri wa wanaoweza kupiga kura ama katika chaguzi kuu au katika shughuli nyingine za uchaguzi. Sheria zilizoko na katiba hudhibiti wapigakura kwa kutoa vigezo vingine vya walio na haki ya kupiga kura kufanya hivyo.
Siku hizi, kuna mahitaji mengine ambayo ni lazima yatimizwe ili yeyote yule aruhusiwe kupiga kura. Baadhi ya mahitaji hayo yanaweza kuorodheshwa kama ifuatavyo: umri, uraia, haki ya kupiga kura kiraia na kisiasa. Wakati mwingine kupata usajili wa kieneo katika muda ufaao pia huchukuliwa kama kigezo vilevile. Hii ndiyo hali pia ya anakoishi mpigakura siku ya uchaguzi. Ni wazi kuwa vigezo vingine haviwezi kuwa vya kibaguzi.
- Uraia
Mara nyingi, uraia huonekana kama kuwepo kwa utaifa na huonekana kama uhusiano wa kisheria kati ya mtu binafsi na serikali. Uhusiano huu huwakilisha hitaji linalotakiwa kwa wapigakura na huwa la kihistoria. Ili kuwahusisha au kuwafanya wawe sehemu ya jumuia ya kisiasa, huwaruhusu wananchi kushiriki katika masuala ya umma.
Utaifa na uraia si suala moja: tofauti hii ni muhimu kwa nchi ambamo wakazi na raia wake ni wa mataifa tofauti, kwa sababu wanatoka kwingine na wana tamaduni tofauti na historia tofauti na mielekeo tofauti ya kisiasa pia. Mbali na hiyo, ni muhimu kukumbuka kuwa mara nyingi uraia hurejelea utu uzima. Sifa bainifu ya nchi hutegemea uhuru wake, na ili kupata sifa hizi ni muhimu kujua ni nani anayeweza kuchukuliwa kama raia. Ubainishaji huu hutokana na Katiba, na sheria. Haya mawili lazima yabainishe katika njia ya wazi raia ni nani, kulingana na kanuni zilizowekwa kuhusu mahali pa kuzaliwa, umri, na vipengele vingine. Lazima yabainishe hivyo basi, mahitaji mengine ambayo ni sharti yatimizwe ni kupata utaifa au uraia: kuchukuliwa kama mkaazi halali wa nchi, uhusiano kati ya mtu asiye raia na nchi mpya, ndoa, uzazi na uhusiano mwingine wa kisheria na raia wengine, na kadhalika.
Kwa kuzingatia haya, inaweza kudaiwa kuwa uraia na dhana ya kisheria, si ya kisiasa: Katiba na sheria za kila nchi hubainisha ni lini mtu anaweza kuchukuliwa kama raia. Katika nchi nyingine, uraia hautoshi, ingawa (hasa iwapo uraia umepatikana kwa muda maalumu na njia nyingine mbali na kuzaliwa) ili kutekeleza haki ya kupiga kura. Mara nyingi, katika hali kama hizi, kuishi kwa muda fulani katika nchi husika ambapo uchaguzi utafanyika, ni mojawapo ya matakwa.
Uhusiano wa moja kwa moja unaowaunganisha wananchi na haki ya kupiga kura, hausisitizwi sana kama ilivyokuwa awali, wakati mwingine kutokana na athari ya kihistoria, na sababu za kitamaduni kwa upande mwingine, au kama athari ya sababu nyingine kama vile uhamiaji, au amri zinazotokana na mikataba ya kimataifa.
Mara nyingi, ikiwa kanuni za kisheria haziwekwi kisheria, wageni huruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi wa manispaa kwa kuangalia hali hii sababu kuu inapatikana; wageni wa kisheria huhusika katika maisha ya kila siku kama watu wengine. Mbali na hayo, uchaguzi wa manispaa hauna mvuto mkubwa kisiasa. Mkataba wa Muungano wa Ulaya wa 1990 kwa mfano huidhinisha haki ya kupiga kura na hala ya kupigwa kura kwa viti vya mtaa katika nchi zote katika muungano kwa kurejelea haki hii vipengele hivi hupatikana nchini Udeni, Uswidi na Norwe. Hali ya Uingereza ni ya kufurahisha. Huko raia wa Jamhuri ya Ayalandi na wa Jumuiya ya Madola wana haki ya kupiga kura katika Uchaguzi wa Uingereza.
Vilevile, ni muhimu kutaja udhibiti wa uchaguzi wa wanachama kwa Bunge la Ulaya. Kanuni hizi zilianzisha juhudi nyingi zilizoko katika siku zetu. (cfr. Uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Ulaya). Huko, raia wa Ulaya wanaruhusiwa kupiga kura bila ya kurejelea makazi yao yalipo. Wanaweza pia kupigiwa kura iwapo majina yao yatakuwepo katika karatasi za kura zilizopigwa katika nchi ya Ulaya ambayo ni tofauti na yao asilia.
Mizozo mingi inaweza kuzuka kutokana na kanuni za kitaifa. Hii ndiyo hali ambayo baadhi ya wananchi wa Muungano wa Urusi wanakabiliwa nayo leo (cfr. Wachache Kunyimwa Haki ya Kupiga Kura, na Matatizo ya kuwa Raia wa Urusi). Hali ya kufungia uraia kwa watu wa nchi mahsusi pekee (kwa misingi ya kihistoria na kitamaduni) imewanyima watu wengi haki ya kupiga kura.
2. Ukaazi
Makazi ya mtu yana umuhimu kwa mitazamo miwili. Kwanza, wananchi wa asili tofauti wanaweza kuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa nchi ya kigeni (wanaweza hata kupata uraia wa nchi wanamoishi). Pili, kuishi katika nchi ya kigeni kunaweza kuwa na athari mbaya kwa watu wageni).
Makaazi ni muhimu sana katika uchaguzi wa maeneo na mitaa na inaweza kuwa muhimu sana kwa usajili wa uchaguzi. Wakati mwingine, hasa katika demokrasia zilizoendelea, wananchi wanoishi nchi nyingine wanaweza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa chaguzi za kimaeneo za nchi yao. Katika hali hii, sheria za uchaguzi huwaruhusu kutuma kura zao kwa njia ya barua, kupiga kura katika ofisi za mabalozi au kupiga kura katika maeneo mengine (kama vile haki ya jeshi au mabalozi wanaoishi ughaibuni). Hata hivyo, kuna baadhi nchi ambamo haya hayafanyiki. Kupiga kura katika nchi za ughaibuni ni muhimu kwa nchi ambamo kuna uhamiaji mwingi na ambao ni muhimu.
Matukio mengine yanaweza kufanya mahali ambapo watu wanapigia kura kukosa maana. Huko Kosta Rika kwa mfano, kura huwekwa katika mashine za kiotomatela (ATM). Ni muhimu kueleza kuwa licha ya hayo maeneo ambapo wapiga kura wanamoishi ni muhimu ili kubainisha eneo la uchaguzi (si mahali pa kupigia kura) ambalo kura hiyo itahesabiwa. Msajili wa uchaguzi huruhusiwa kuchora mipaka dhahiri ili kutofautisha maeneo. Ni muhimu kubainisha aina ya uchaguzi wa utakaoathiriwa na wapigakura.
3. Umri
Mahitaji ya umri maalumu wa kupiga kura yamefuatia mabadiliko yanayoelekea kwenye utekelezaji wa haki ya kupiga kura kwa ulimwengu mzima. Kutoka kwa mtazamo wa kihistoria, umri wa kupiga kura haulingani na umri wa kuadhibiwa kwa kosa la jinai. Kwa hakika, wapigakura (takribani miaka 25) walikuwa wazee kuliko wahalifu. Umri tofauti wa kupiga kura uliwekwa kwa wanawake. Katika siku zetu hata hivyo, nchi nyingi zimeamua kuwa vijana wa umri wa miaka kumi na minane ambao ni raia wanaweza kupiga kura.
Kwa kawaida umri wa kupiga kura huwekwa katika Katiba, kwa kuwa huwakilisha kidhibiti dhidi ya haki ya kimsingi. Ijapokuwa nchi nyingi hutofautiana kuhusu umri wa mtu anayepaswa kuhukumiwa kwa kosa la jinai, kuna mwelekeo wa kimataifa wa kutambua utu uzima na haki za kiraia unapotimiza miaka kumi na minane.
4. Kutumia haki za kiraia na kisiasa
Wale binafsi lazima wawe na haki za iraia na kisiasa za kupiga kura. Haki hizi kwa kamilifu huwa zipo hadi pale ambapo ushahidi wa kuonyesha kwamba zimeondolewa utatolewa. Hivyo basi, misingi na taratibu zitakazotumiwa kubatili au kusitishwa matumizi ya haki za kiraia na kisiasa lazima ziwekwe wazi na katika muda wa kufaa.
5. Kudhibiti haki ya kupiga kura
Watu binafsi wana haki ya kikatiba ya kupiga kura na haki ya kikatiba ya kupigiwa kura. Hata hivyo, matumizi ya haki hizo yanaweza kukatizwa kwa hali kadhaa ambazo lazima ziwe zimewekwa kwa misingi ya kidemokrasia, na ambazo zinaweza kuorodheshwa ifuatavyo:
- Kwanza kabisa, kwa sababu tunarejelea kudhibiti kwa haki ya kimsingi kanuni ya kimsingi lazima ifuatwe: kila kidhibiti kilichowekwa kwa haki ya kimsingi lazima kiwekwe katika sheria.
- Mbali na sheria zinazodhibiti sheria za kimsingi lazima zifafanuliwe kwa njia wazi kutathmini tu si mbinu ya kufana mahali ambapo haki za kimsingi zipo matatani.
- Kuwekwa kwa haki za kimsingi lazima ipendelewe badala ya mengi yote. Kwa kuzingatia masuala ya uchaguzi, ufafanuzi unaopendelea kushiriki kikamilifu kwa wananchi ni bora kuliko chaguzi nyingine.
- Lazima zitumiwe kwa njia isiyo na ubaguzi. Yaani iwapo ni hali mbili zinazofanana, udhibiti sawa utatumiwa bila ya kurejelea suala zaidi.
- Vidhibiti vya haki ya kupiga kura lazima vinuie kupatikana kwa taratibu huru na kidemokrasiaa zaidi. vidhibiti vinavyowekwa kwa haki ya kupiga kura na ya kupigiwa kura kujitolea kwa watu binafsi yanakubalika mradi yanaleta fanaka zaidi katika kuwepo kwa haki ya kupiga kura ama haki ya kupigiwa kura kwa mtazamo wa pamoja.
Lazima pawe na halmashauri huru mamlaka ya kusimamia uamuzi kulingana na vidhibiti vilivyowekwa kwa haki za kimsingi kwa kawaida viongozi hawa wanaweza kutambuliwa na halmashauri ya kusimamia uchaguzi ama Tawi la Kisheria la Serikali. Hata hivyo, vidhibiti vilivyowekwa kwa haki za kimsingi lazima zirejelewe kisheria.