Wananchi lazima watimize hitaji jingine ili waweze kupiga kura: lazima wasajiliwe katika rejista ya uchaguzi. Hitaji kama hilo ni muhimu sana. Rejista ya uchaguzi ni orodha ya katalogi ambamo wananchi wanaopaswa kupiga kura hujumuishwa. Kuwekwa kwa wananchi katika rejista hii huonyesha kuwa wananchi wametimiza mahitaji mengine na ni wakaazi wa eneo halali la uchaguzi.
Sheria zinazohusu uchaguzi zinapaswa kuweka mikakati ya kutosha na sahili inayolenga kukuza ujenzi wa sajili au rejista ya wapigakura. Rejista hii inapaswa kusasaishwa. Inavyosemekana, rejista za uchaguzi huwa na jukumu la kimsingi la kukuza imani miongoni wananchi.
Usajili wa wananchi kiuchaguzi unaweza kufanywa kupitia mifumo mitatu tofauti: kubuniwa kwa orodha ya muda, kubuniwa kwa rejista ya kudumu, matumizi ya rejista za raia.