Orodha ya muda ya wapigakura hujengwa kwa matumizi katika tukio maalumu la uchaguzi. Hubuniwa ili kutumiwa mara moja na hivyo basi sio orodha endelevu, ya kusasaishwa au pengine kusahihishwa katikati ya chaguzi. Hutolewa katika kipindi cha kabla ya uchaguzi, mara nyingi katika muda mfupi sana. Kuna njia mbili za kutengeneza orodha ya muda:
- usajili wa wapigakura ulioanzishwa na serikali
- usajili wa wapigakura ulioanzishwa nao wenyewe
Katika mfumo wa pili, huenda kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi hivyo usajili huanzishwa na wananchi wenyewe. Halamshauri ya kusimamia uchaguzi hutenga vitu vya kusajili wapigakura ambavyo huwa na wafanyakazi na hufunguliwa kwa muda mrefu kiasi cha haja ili wapigakura wote wanaostahili kusajiliwa wanapata fursa ya kujiwasilisha wenyewe na kujisajili kupiga kura. Kuanpaswa kuwa na vitu vya kutosha vilivyowekwa mahali pazuri ili kurahisisha usajili wa raia yeyote. Matoleo maalumu yanaweza kuhitajika ili kuweza kuwafikia baadhi ya wapigakura: wakazi wa maeneo ya mashambani ambao huenda wakalazimika kusafiri miendo mirefu kufikia vituo vya usajili; wazee na wanyonge; wapigakura wanaoishi nje ya nchi; na wapigakura wasio na maboma. Huenda likawa wazo zuri kutumia vifaa hivyo kama vile vituo vya usajili na baadaye kama vituo vya kupiga kura.
Katika mfumo wa pili watu huenda kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi hiyo usajili huo huanzishwa na raia. Ikiwa tarehe za uchaguzi hazikuwekwa na sheria, kutakosekana uwazi kuhusu lini ambapo uchaguzi unaofuata uatakapofanyika na lini orodha ya wapigakura inapaswa kutengezwa. Matokeo yanaweza kuwa kwamba orodha hiyo iundwe wakati wa kipindi rasmi cha uchaguzi na kipindi hicho hicho kinaweza kurefushwa ili kujumuisha watu wengi. Katika hali hii mpangilio wa mapema ni muhimu hasa katika kuhakikisha kwamba hesabu ya watu inakamilishwa kwa haraka.
Orodha za muda na Vigezo vya utendakazi
Vigezo vitatu hutumiwa katika kupima utendakazi wa orodha ya wapigakura: usasa, ulinganifu na ukamilifu.
Usasa unahusu kiwango cha usasa wa taarifa iliyo kwenye orodha ya wapigakura kwenye siku ya uchaguzi. Yaani, je, wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura wamejumusihwa katika orodha hiyo? Je, waliofariki wameondolewa kutoka kwenye orodha hiyo? Je, orodha hiyo ina anwani ya hivi punde ya makazi yake, hasa kwa wale waliohamia kwingine kanla ya uchaguzi? Kadiri orodha hiyo inavyotengenezwa karibu na wakati wa uchaguzi, ndivyo viwango vya usasa na utendakazi vitakavyoimarika. Shughuli hii inapofanywa mapema, itakuwa na udhaifu katika misingi ya usasa. Kwa hivyo, ili kufaulu katika sehemu ya usasa, orodha ya wapigakura inapaswa kutengenezwa karibu na uchaguzi na inapaswa kusasaishwa au kusahihishwa karibu na siku ya uchaguzi.
Ulinganifu unahusu kiwango cha usawa na usahihi wa taarifa iliyotolewa kuwahusu wapigakura waliosajiliwa. Katika mfumo wa kutumia orodha ya muda ya wapigakura, taarifa hukusanywa ama kupitia njia ya hesabu ya kutoka nyumba hadi nyingine au au kwenye vituo vya usajili wa wa wapigakura. Hivi inamaanisha kwamba inapaswa kunakiliwa na ofisa na kuhamishwa moja kwa moja hadi kwenye kiziodeta cha usajili wa wapigakura kinachotumiwa katika kutoa na kuchapisha orodha ya wapigakura au pengine ihamishiwe moja kwa moja kwenye orodha ya wapigakura. Ikiwa orodha ya muda inatengenezwa kwa muda mfupi sana, kuna uwezekano wa kupata makosa hapa na pale au yaliyofanywa ya maandishi wakati taarifa hiyo inapojazwa kwenye kiziodeta na hatimaye kwenye orodha yenyewe. Tatizo hilo linaweza kutatuliwa kwa kutumia idadi kubwa ya wasajili ili waweze kutambua kasoro hizo.
Ukamilifu unahusu kiwango cha taarifa iliyoko kwenye orodha ya wapigakura kuwahusu wapigakura wote stahifu wakati wa uchaguzi. Kwa mifumo ya hesabu, orodha hiyo inaweza kukamilika kabisa ikiwa:
- wasajili wanazuru tena na tena makao ambako hakuna yeyote aliyekuwa nyumbani wakati huo
- wanaacha taarifa inayowaelekeza wapigakura kuhusu jinsi ya kuanzisha shughuli hiyo wenyewe
- wanafunzwa vilivyo na kuwajibikia kazi yao.
Kwa mifumo inayotumia vituo vya usajili wa wapigakura, kiwango cha ukamilifu kitakuwa juu ikiwa:
- vituo hivyo vinatosha
- saa za kuendesha shughuli hiyo zinatosha ikiwemo jioni na wikendi
- Nafasi za usajili zinapeanwa kwa watu wapigakura walio na ugumu (k.v. nje ya nchi na vituo vya)
Suala la Gharama
Orodha ya muda huhusisha usajili wa wapigakura wote katika muda mfupi. Suala la kutumia wakati na pesa katika kipindi hicho kifupi ni muhimu. Katika orodha endelevu, gharama hutumiwa kwingi na kwa muda mrefu. Katika lugha ya wasimamizi wa uchaguzi, uundwaji wa orodha ya muda una gharama kubwa.