Rejista au orodha endelevu ni orodha ya wapigakura stahifu wote kwa wakati huu, iliyo sahihishwa ili kujumuisha mabadiliko kwenye usajili wa wapigakura katikati ya matukio ya uchaguzi. Orodha endelevu hutunzwa na wasimamizi wa uchaguzi – tofauti na ilivyo sajili ya raia, au rejista ya raia kutunzwa na mashirika mengine ya serikali. Orodha endelevu huepuka shuguli za ziada ambazo hupatikana katika orodha ya muda, badala ya kujifungia katika kipindi cha punde kabla ya uchaguzi, kazi ya kuunda orodha ya wapigakura hufanywa katika muhula mzima wa uchaguzi. Orodha endelevu pia hutumia fursa ya tarakilishi kuhifadhi, kutunza na kusambaza deta; hurekodi taarifa kutokana na chaguzi zilizopita kwenye tarakilishi na kuzitumia katika shughuli ya usajili wa wapigakura wakati huu na katika siku zijazo. Ili kusasaisha taarifa iliyomo, orodha endelevu aidha hupata deta yake kutokana na ile iliyokusanywa na mashirika mengine yanayoshughulikia umma kama vile mashirika ya kusajili magari na madereva, idara za kutoza ushuru na halmashauri za kusimamia nyumba.
Mbinu za Kuisasaisha
Masahihisho ya mara kwa mara kwenye orodha hiyo huongeza majina ya watu waliofikisha umri wa kupiga kura, wanakuwa raia au pengine kuwazesha kuwa na uwezo wa kupiga kura (k.m. kutokana na kuwachiliwa kutoka gerezani), au wale waliohama kutoka eneo moja la upigaji kura hadi jingine. Masahihisho hayo huondoa majina ya watu waliokuwa kwenye orodha awali na hatimaye wakafa au wakapoteza uwezo wa kuafiki mahitaji ya kupiga kura. Halmashauri nyingine za kusimamia uchaguzi husahihisha orodha hiyo kila mwaka. Ubaya wa mwelekeo huu ni kwamba orodha hiyo huwa tayari ishapoteza usasa wake miezi kadhaa kabla ya kuakamilishwa kwake na huendeleza kupoteza usasa huo hata zaidi katika mwaka unaofuata. Kutokana na viwango vikubwa vya kuhama katika jamii nyingi, takribani asilimia 20 ya wapigakura wanaweza kubdilisha anwani zao katika mwaka mmoja. Matokeo yatakuwa uwepo wa orodha ya wapigakura iliyojaa kasoro kuhusu usasa.
Mwelekeo mwingine ni kusasaisha taarifa kuhusu wapigakura kwa karibu karibu. Katika visa vingine, halmashauri ya kusimamia uchaguzi husasaisha orodha kila siku kutegemea inavyopokea taarifa kupitia njia nyingine kama vile usajili wa kielektroniki au arifa ya moja kwa moja kutoka kwa mpigakura huyo. Usasaishaji huo pia unaweza kufanyika kila mwezi kutegemea jinsi halmashauri ya kusimamia uchaguzi inavyopokea taarifa hiyo kutoka kwa mashirika ambayo halmashauri hiyo hushirikiana nayo katika utumizi deta.
Miafaka kuhusu Utumizi deta kwa Ushirikiano
Orodha endelevu hujenga haja ya mpangilio wa utumizi deta kwa ushirikiano kati ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi na mashirika mengine ya kiserikali ambayo raia hupiga ripoti kuhusu mabadiliko katika taarifa zinazowahusu ambazo zinaweza kuathiri ustahifu wa kupiga kura. Kwa mfano, mara nyingi orodha za wapigakura hujumuisha taarifa kuhusu makao ya kila mpigakura. Katika nchi ambako uchaguzi chaguzi hufanyika hupangwa kwa misingi ya maeneo mbalimbali ya bunge au sehemu za uchaguzi, mpigakura anastahi tu kupiga kura katika eneo alilo na makao ya kudumu. Hii ndiyo sababu ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi hutaka taarifa kuhusu mabadiliko makao ya ili iweze kutunza orodha hiyo endelevu. Mtu aliyehama huenda akawa ameipasha taarifa hiyo kwa shirika linaloshughulikia raia – shirika la kushughulikia leseni za udereva ili kusasaisha leseni, idara ya ushuru katika kujaza fomu ya matoleo ya ushuru au posta katika hatua ya kuelekeza kuhusu atakapokuwa akizipokea barua zake. Halmashauri za kusimamia uchaguzi zinazotunza orodha endelevu hutafuta uwezo wa kupata taarifa zilizotolewa na wapigakura kwa mashirika mengine yanayoshughulika na raia. Kisha, wao hutumia taarifa hiyo kusasaisha taarifa katika usajili wa wapigakura.
Hii huhusisha changamoto kadhaa, zikiwemo zifuatazo:
- Katika nchi isiyotoa nambari maalumu ya kitambulisho kwa raia wake, inaweza kuwa vigumu kumtambua mtu vilivyo kutokana na taarifa iliyotolewa kwa shirika jingine. Kwa mfano, watu zaidi ya mmoja walio na majina sawa (mara nyingi mzazi na mwanawe) wanaweza kuwa wanaishi katika makao mamoja. Mmoja wao akibadilisha makao, huenda ikawa vigumu kutambua aliyehama.
- Ikiwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi inategemea taarifa kutoka kwa mashirika mengine, inastahili kupokea taarifa iliyo tayari kwa matumizi. Halmashauri mablimbali hata hivyo zinaweza kuwa na aina mbalimbali za viziodeta vya tarakilishi, hivyo huenda zikakosa kujiandaa kubadilisha mifumo yazo. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi haina budi kupata njia ya kufanya kazi navyo vyote. Ili kufanya hivyo, halmashauri itahitajika kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi wenye uwezo wa kusaidia na wenye umilisi katika maswala ya tarakilishi.
Faida za Ndani na Nje za Orodha Endelevu
Kwa kuwa kazi ya kutengeneza orodha ya wapigakura hufanywa katika muhula mzima wa uchaguzi, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kuwazia kufundisha na kuimarisha ujuzi miongoni mwa wafanyakazi wake. Idadi ya wafanyakazi wa kitaaluma na wanaoshikilia nyadhifa katika mfumo unaoendelea itakuwa kubwa zaidi ya jinsi ambavyo ingekuwa iwapo wangetumia orodha ya muda. Hali hii hutoa nafasi ya kujenga elimu bora kwa wapigakura katika mchakato wa usajili wa wapigakura.
Kwa mfano, nchi nyingine zinazotumia orodha endelevu hukisia haja ya kusajili watu wapya wanaostahili kupiga kura kwa kutengeneza rejista ya muda ya wapigakura. Ikiwa umri wa kupiga kura ni miaka 18, vijana wanaweza kuwekwa katika rejista hiyo ya muda ya wapigakura wakiwa na umri wa miaka 16 au 17, na kuhamishiwa kwenye orodha ya jumla wanapofikisha miaka 18. usajili hiyvo basi utafanyika mapema wakiwa vijana na halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kushirikiana na mifumo ya shule za upili kujenga mpango wa elimu kwa wapigakura huku wakishughulikia usajili wa wapigakura.