Sajili ya Raia – Upungufu / Ubaya —
Skip to content.
|
Skip to navigation
Search Site
Advanced Search…
English
Español
العربية
Français
Swahili
Home
Encyclopaedia
Personal tools
Log in
Practitioners' Network
You are here:
Home
→
Encyclopaedia
→
Mada
→
Usajili wa Wapigakura
→
Mambo ya Kijumla
→
Sajili ya Raia
→
Sajili ya Raia – Upungufu / Ubaya
face
Practitioner Login
sw
Encyclopaedia
Info
Voter Registration
Topic Index
Sajili ya Raia – Upungufu / Ubaya
Sajili ya Raia – Upungufu / Ubaya
Ni ngumu kuunda na kutunza. Huifanya orodha ya wapigakura kuwa rahisi kutengeneza lakini sajili yenyewe hutaka raslimali nyingi kuitengeza. Hata hivyo, kwa sababu ambazo huenda hazihusiani na uchaguzi, serikali inaweza kuwa imeamua kutunza orodha ya usajili. Ikiwa hivyo, ni bora kutumia taarifa iliyo kwenye sajili kwa kazi ya kutayarisha orodha ya wapigakura.
Hutegemea pakubwa nambari ya kitambulisho cha kitaifa cha raia, hivyo kutoa nafasi kwa viziodeta vingi kuunganishwa. Nchi ambazo hazitumii nambari za vitambulisho vya kitaifa vya wananchi hupata ugumu wa kutengeneza sajili ya raia iliyo na kiwango cha juu cha usasa, ulinganifu na ukamilifu.
Katika nchi nyingi, sajili ya raia ilijengwa kutokana na rejista za kanisa na nakala za mwanzoni zilikuwa kwenye karatasi. Sajili za raia hivi leo zinaelekea kuwa za kitarakilishi hivyo basi kuwezesha halmashauri za kushughulikia raia kuvamia nafasi hiyo ya utunzaji deta inayotolewa na orodha hizo. Sajili ya raia inayoweza kutumiwa ipaswavyo na vilivyo katika kutengeneza orodha ya wapigakura, huhitaji muundomsingi thabiti wa tarakilishi ili kutunza kiziodeta kwa matumizi na halmashauri inayoshughulikia raia na vilevile halmashauri ya kusimamia uchaguzi.
Katika kiziodeta cha sajili ya raia, makini inapaswa kuzingatiwa katika kutunza deta inayohitajika katika kusimamia uchaguzi na utengenezaji wa orodha ya wapigakura. Jina lolote linaloongezwa kwenye kiziodeta hicho linapaswa kuingizwa moja kwa moja kwenye eneo mwafaka la usimamizi. Mfumo huo hivyo basi hutaka nyenzo na wafanyakazi ili kumudu ujenzi wa muundomsingi wa tarakilishi.
Katika nchi nyingine, sajili ya raia huunganisha mawazo ya Orwellian Big Brother, hivyo basi kuzidisha chuki kubwa dhidi ya ujenzi wa orodha kama hiyo.
Vivyo hivyo, watu wengine huhofia matumizi mabaya ya viziodeta vikuu kama vile sajili ya raia. Hofu yao ni kwamba deta hiyo inaweza kutumiwa kwa kazi zisizokubalika za kibiashara au kwamba kuna vizuizi vichache kuhusu kubadilishana deta kati ya mashirika ya serikali.
Sajili ya raia hufanya halmashauri ya kusimamia uchaguzi kutegemea serikali kwa utoaji na utunzaji wa orodha ya wapigakura. Pale ambapo vyama pinzani, makundi ya kutetea haki za raia au wapigakura wenyewe wana shaka au hawana imani na serikali, shauku zao zinaweza kuendelezwa hadi kwenye halmashauri ya kusimamia uchaguzi na orodha za wapigakura. Mara nyingin huwa muhimu kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi kuwa na, na kuweza kudhihirisha uhuru wao dhidi ya serikali. Kwa kiwango fulani, mifumo ya kusajili raia huhujumu uhuru huu kwa kuifanya halmashauri ya kusimamia uchaguzi kutegemea mashirika ya serikali ili kutimiza baadhi ya majukumu yake ya kimsingi. Kukiwa na imani ya kutosha katika serikali, huenda hili likawa si chochote. Hata hivyo, kukiwa na imani ndogo katika serikali matumizi ya mfumo wa sajili ya raia ambao unachukuliwa kuwa wa kiwango cha chini na pengine unaopendelea mrengo wa upande wa serikali yanaweza kuhujumu ufaafu wa halmashauri ya kusimamia uchaguzi.
Ikiwa wizara inayoshughulika na kutunza sajili ya raia haitaki au inashindwa kuisasaisha, kuilinganisha na kuikamilisha viwango vinavyokubalika, halmashauri ya kusimamia uchaguzi italazimika kuanza na deta mbovu kama msingi wa kutengeneza orodha ya wapigakura.
Usajili wa Wapigakura
Contributors to Voter Registration
Bibliography
Contact
Privacy Policy
Terms of Use
Accessibility
Site Map
Copyright and Disclaimer
©
1998-2025 ACE project