Ili kumudu vilivyo vigezo vya usasa, ulinganifu na ukamilifu, mfumo wa usajili hauna budi kuwa sahili na usiotatiza watumiaji wake. Usajili wa wapigakura haupaswi kuwa kipimo cha viwango vya usomi. Haupaswi kivyovyote kusukuma mzigo wa kifedha, kama vile ada za kutolewa kwa wapigakura. Ukifanya hivyo, watashuku uhalali wake na utakosa mashiko kwa vigezo hivyo vitatu.
Zifuatazo ni baadhi ya njia za kuhimiza usajili wa wapigakura:
- Tumia fomu na/ au mtindo mwepesi wa usajili.
- Panga kampeni maalumu zitakazolenga baadhi ya makundi ambayo huenda yangekuwa magumu kusajili.
- Ikiwa mfumo huo unatokana na vituo vya usajili wa wapigakura, angazia kuweka vituo vya usajili vya kuhamishwa ili kufikia watu walio katika maeneo ya mashambani.
- Husisha makundi mengine katika hatua hiyo ya usajili – kwa mfano, makundi ya wanawake, mashirika tengwa na wawakilishi wa vijana.
- Ikiwezekana, angazia kuruhusu usajili wa kielektroniki wa wapigakura.
- Panga usajili ucheleshwe kidogo katika wakati wa kampeni za uchaguzi, wakati ambapo ari yao inaweza kuwa juu.
- Angazia uwezo wa kuruhusu usajili kufanywa kwenye siku ya uchaguzi katika vituo vya kupigia kura.
- Jadiliana kuhusu mipango ya kutumia deta kwa ushirikiano na halmashauri nyingine zinazoshughulikia raia ili kusaidia katika kufuatilia mabadiliko katika taarifa za wapigakura.
- Angazia uwezekano wa kuweka sajili ya muda ya vijana watakaofikisha umri wa kupiga kura katika mwaka mmoja au miwili hivi ijayo. Aidha, angazia uwezekano wa kufanya hii kuwa suala kuu la kampeni ya elimu kwa wapigakura katika shule za upili.
- Jenga na kutekeleza harakati mwafaka za elimu kwa wapigakura.
Ikiwa wananchi hawana wajibu rasmi au kisheria kujisajili, mfumo wa usajili wa wapigakura utakuwa wa kujitolea. Katika hali kama hizi, halmashauri za kusimamia uchaguzi zinaweza kuchagua moja katika mielekeo ya usajili:
- Zinaweza kuweka mazingira sawa kwa wote kwa kuhakikisha kwamba mchakato wa usajili ni rahisi, wazi na angavu, ulio na nafasi sawa kwa raia wote kujisajili. Hata hivyo, hazichukui hatua maalumu za kuhimiza kujisajili kwa watu binafsi au makundi ya watu wanaostahili kupiga lakini huenda wakawa na nafasi ndogo sana ya kujisajili na kupiga kura – kwa mfano, vijana, maskini au watu wasio na makao, na watu kutoka makabila madogo au tengwa. Huu ni mwelekeo usiohusisha watu moja kwa moja katika usajili.
- Zinaweza kurahisisha usajili na upigaji kura kwa makundi ambayo kihistoria hayajawakilishwa vilivyo katika michakato ya uchaguzi, kupitia kwa njia za kampeni zinazolenga makundi hayo. Huu ni mweleko husishi unaotokana na mtazamo kwamba halmashauri hiyo ya kusimamia uchaguzi ina jukumu la kuhakikisha kwamba makundi yote ya wananchi yanaweza kutimiza haki yao ya kupiga kura.
Japo mielekeo yote miwili ina uungwaji mkono miongoni mwa wasimamizi wa uchaguzi, hatua shirikishi za usajili wa wapigakura zinaweza kuibua maswali tatanishi. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi haina budi kutoegemea upande wowote na kuwa huru dhidi ya serikali na vyama vya upinzani. Ikiwa kihistoria makundi yaliyokosa kuwakilishwa vilivyo yanaelekea kuunga mkono chama kimoja dhidi ya vingine, juhudi za kuwahimiza kujisajili na kupiga kura zinaweza kupiga jeki chama hicho wanachounga mkono. Halmashauri za kusimamia uchaguzi zinalazimika kutarajia mambo kama hayo kuibuliwa na zijiandae kutetea vikamilifu mwelekeo shirikishi.
Sifa za Wapigakura Wanaofaa / Stahifu