Nchi nyingi hukabiliwa na changamoto katika kutambua wapigakura stahifu wakijitokeza kwenye vituo vya kupigia kura. Mchakato wa uchaguzi unapaswa kuwa na mpangilio wa kuhakikisha kwamba ni watu waliosajiliwa kihalali pekee wanaopiga kura na kwamba watu hao wanaojitokeza kwenye vituo kupiga kura ni wale haswa wanaodai kuwa wao.
Wapigakura watarajiwa wanaokuja kwenye kituo cha kupigia kura siku ya uchaguzi, wanapaswa kujitambulisha kwa maofisa wa uchaguzi kabla ya kupokea kura. Hili huwaruhusu maofisa wa kusimamia uchaguzi kukagua majina ya wapigakura dhidi ya orodha ya wapigakura na kuhakikisha kwamba wanajumuishwa. Kisha kila jina huondolewa au mpigakura kutia sahihi kwenye rejista hiyo. Katika visa vingine, kukiwa na hofu kuhusu uwezekano wa kupiga kura katika zaidi ya kituo kimoja cha kupigia kura, wapigakura wanaweza kuhitajika kuingiza kidole chao kimoja katika wino usifutika haraka ili kuonyesha kwamba wameshapokea kura.
Kama Kanuni ni Kubeba Kitambulisho
Kuna njia mbalimbali ambazo wapigakura wanaweza kutumia kuthibitisha utambulisho wao. Katika nchi ni desturi kwa raia kubeba vitambulisho (k.m. kadi ya kitambulisho cha kitaifa, leseni ya udereva, kadi ya kitambulisho cha kazi, kadi ya huduma za matibabu), usimamizi wa uchaguzi huenda ukakosa kuhitajika kutoa stakabadhi za utambulisho wake. Katika nchi ambamo udanganyifu wa wapigakura hauwezi kutokea, ofisi za usajili huenda zikakosa kuomba kitambulisho chochote; wapigakura hutilia sahihi orodha au rejista ya wapigakura. Na katika hatua ya kutumia faili za kitarakilishi, mara nyingi hakuna sahihi asilia ya kutumiwa katika kulinganisha.
Kadi za utambulizho wa wapigakura zilizotumwa kwa njia ya barua, huwapa wapigakura taarifa zinazojitokeaza kuwahusu katika orodha ya wapigakura na pia zilizomo kwenye nyenzo ya kutekeleza elimu kwa wapigakura. Kadi hii, ambayo hutumwa kwa raia wote walio kwenye orodha ya wapigakura, hujumuisha taarifa za kibinafsi kumhusu mtu kwa jinsi zinavyotokea kwenye hiyo pamoja na siku ya uchaguzi na eneo la kituo cha kupigia kura ambako walijisajili. Kwenye kituo cha kupigia kura, wapigakura hujitambulisha kwa kuzionyesha kadi hizo na kutaja jina na anwani, au kuonysha kitambulisho kilicho na picha kama vile lesesni ya udereva.
Kama Kanuni si Kubeba Kitambulisho
Katika nchi nyingine, kuthibitisha utambulisho katika uchaguzi kunaweza kuwa changamano zaidi na hata kutatiza maofisa wa kusimamia uchaguzi. Hili hufanyika hasa katika nchi inayotumia sajili ya raia, na ambako si desturi kwa raia kubeba vitambulisho vyao. Hali hii huweka mzigo mkubwa wa kifedha na kiusimamizi kwa usimamizi wa uchaguzi ambao unapaswa kutoa uthibitisho wa utambulisho wa wapigakura watarajiwa. Katika visa vingine, wapigakura wenyewe hulazimika kutumia gharama fulani za kutengeneza kadi za wapigakura au vitambulisho vingine.
Mazingatio ya Usalama
Kukiwa na matumizi ya kadi za utambulisho wa wapigakura, hofu kubwa ya usimamizi bora wa uchaguzi huwa kuhusu usalama, na linaloongoza katika visa hivyo vya utovu wa usalama litakuwa ughushi. Kwa kufahamu tishio hili, Agosti mwaka wa 1990, Mexico iliteua kutumia kadi za utambulisho wa wapigakura zilizoimarisha usalama. Ili kuzuia ughushi, vipengee tisa kuhusu usalama vilijumuishwa katika mpangilio wa kadi, hivyo basi kufanya iwe vigumu kunukuu au kubadilisha chochote. Vipengele hivi vya usalama ni pamoja na nafasi ya nambari, hologramu, picha na muunganisho wa kimolekuli.
Hofu nyingine ni usalama katika uhifadhi na usambazaji. Hili lilikuwa suala kubwa katika uchaguzi wa mwezi wa Juni mwaka 1995 katika nchi ya Haiti. Kwa kadi milioni 4.2 za kadi za utambulisho wa wapigakura zilizotolewa, tume ya uchaguzi ilitangaza kwamba milioni moja hazikuwepo. Japo idadi hii iliripotiwa pakubwa, haikuthibitishwa. [1]
Suala jingine kuhusu kadi za utambulisho wa wapigakura ni lile la uwezo wa kutoa kadi hizo kwa jumla ya watu wanaoafiki mahitaji ya kupiga kura. Hili lilikuwa changamoto katika uchaguzi nchini El Salvado katika mwaka wa 1994, na vilevile Nikaragua katika miaka ya 1990. Shughuli za kusajili wapigakura na kutoa kadi za utambulisho wa wapigakura ni changamano sana ikiwa uchaguzi huo unafanyika katika nchi inayopitia hali mizozo ya kutumia zana hatari; hili lilifanyika nchini Nikaragua, Angola, na Bosnia na Hezegovina.
Mwisho, ikiwa gharama za kutoa kadi za utambulisho zinawasilishwa kwa wapigakura, athari yake itakuwa na athari kubwa – kama Senegali ilivyogundua katika uchaguzi wa mwaka 1993. Gharama ndogo zilizowekwa zilikuwa kikwazo kwa wapigakura wengi watarajiwa, kwa kuwazuia kushiriki katika mchakato huo wa uchaguzi.
Sifa Zilizomo kwenye Kadi za Utambulisho wa Wapigakura
Kadi za utambulisho wa wapigakura zinaweza kuwa na sifa mbalimbali, sahili na changamano. Sifa kuhusu usalama mara nyingi huzidisha gharama, na wakati mwingine sana, japo si muhimu kila mara. Katika kisa kimoja, ughushi ulizuia kwa kutoa kadi hiyo kama kiambatisho cha kukatwa chini ya fomu yenyewe ya usajili, ikiwa na nambari ya usajili wa mpigakura sawa na ile iliyochapishwa mapema kwenye fomu. Hili kwa kiwango kikubwa liliondoa hali ya kutoa kadi ghushi au wizi wa kadi zisizo na maandishi kwa kuwa jina na nambari ya kitambulisho sawa vilikuwa lazima kuonekana kwenye kadi na orodha ya wapigakura pia. Iliamuliwa pia kuwa kuwasilisha kadi pekee kwenye vituo vya kupigia kura hakukutosha. Kwa sehemu pana, kadi zilizotolewa wakati wa usajili zilifungwa kutumia mchakato wa kutabakisha hivi kwamba uwezekano wowote kutoa tabaka hilo kunaweza kuharibu kadi. Rekodi linganifu zilitambua ni fomu zipi zilizotolewa kwa vituo mbalimbali vya kupigia kura. Hata hivyo, hatua nyingine ya kiusalama ilikuwa kutokeza ishara za vidole kwenye kadi ya usajili na vilevile kwenye fomu tenge ya usajili.
Hofu ya Kunyimwa haki na Usimamizi
Ingawa kadi ya kitambulisho cha mpigakura imekubaliwa ulimwenguni kote, ni muhimu hasa kuhakikisha kwamba haziishii katika usimamizi kuwanyima haki wapigakura wengine ambao kwao gharama husika zinaweza kuwa tatizi. Ubaguzi wa kiusimamizi hutokea pale ambapo raia ana haki rasmi au kisheria kupiga kura au kujisajili kupiga kura, japo anazuiwa dhidi ya kutekeleza haki hiyo kwa sababu gharama ya kufanya hivyo ni ghali sana. Katika visa vingine, gharama za kupata kadi za utambulisho wa wapigakura zimechukuliwa kama vichochezi vya ubaguzi wa kiusimamizi. Kwa mfano, katika nchi moja serikali haikutoza ada yoyote kwa kutoa kadi ya kitambulisho cha kitaifa japo bado wapigakura walilazimika kulipia picha na stempu rasmi, na walipata hasa kutokana na gharama ya wakati uliotumika katika kupata kadi hizo. Mwishowe, gharama yenyewe ilikuwa ghali hivi kwamba ilizuia wengi. Matokeo yake bila shaka yalikuwa ubaguzi wa kiusimamizi kwa baadhi ya wapigakura stahifu.
MAELEZO
:
[1] Taasisi ya Jamhuri ya Kimataifa (IRI), Haiti: Tathmini ya Kabla ya Uchaguzi wa Juni 25, 1995, Chaguzi za ubunge na MabarazaWashington: IRI, 1995, Kiambatisho cha VI.