Kadi za utambulisho wa wapigakura zinaweza kuwa rahisi au changamano. Katika upande mmoja wa mpangilio huu, halmashauri ya kusimamia uchaguzi hutuma kadi kwa wapigakura wote stahifu na kuwashauri kwamba wamesajiliwa kupigia kura katika maeneo fulani, na kueleza ni lini na wapi watakapopiga kura hizo. Mpigakura huiwasilisha kadi yake kwenye kituo cha upigaji kura siku ya uchaguzi akiwa na au bila kifaa kingine cha utambulisho (kama vile leseni ya udereva iliyo na picha ya mpigakura huyo). Nia ya aina hii ya kadi hasa ni kutoa habari kwa mpigakura; kwa kawaida hutumika katika nchi ambako kuna matarajio kidogo kwamba wapigakura watajaribu kupiga kura zaidi ya mara moja au pengine kufanya udanganyifu kwenye uchaguzi.
Katika nchi nyingine, kadi ya utambulisho wa mpigakura ni kifaa muhimu cha kuzuia udanganyifu katika upigaji kura. Kwa sababu hii, halmashauri za kusimamia uchaguzi zinaweza kufanya juhudi zaidi kuhusisha maswala ya usalama katika kadi hizo ikiwa ni pamoja na:
- kufunika kwa tabaka ili kuzuia yeyote dhidi ya kubadilisha taarifa iliyo kwenye kadi hiyo* picha ya mpigakura huy
- ishara ya kidole cha mpigakura kwenye kadi hiyo vilevile kwenye fomu iliyotumiwa kutoa orodha ya wapigakura
- picha ya mpigakura huyo
- sahihi ya mpigakura huyo
- chapisho la rangi kwenye sehemu ya nyuma badala ya nyeusi ili kutambua udanganyifu kwa njia upigaji rudufu
- nambari ya kitambulisho cha mpigakura inayolingana na nambari iliyo kwenye fomu ya usajili wa wapigakura kama njia ya kudhibiti wingi wa fomu na kadi husika
- Anwani ya makao ya mpigakura. Kadi za utambulisho wa wapigakura wakati mwingine zimekuwa na wajibu mkubwa katika kuongeza kuaminika na hata uhalali wa mchakato wa uchaguzi. Katika nchi nyingine ambako kadi zina mambo mengi ya kiusalama, kadi hizo zimekuwa njia bora ya kutambulisha raia. Nchi nyingine tayari zina mbinu nyingine za kutambulisha raia na hivyo hakuna haja ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi kurudufisha juhudi hizo.
Kadi ya utambulisho wa wapigakura huwa na faida kadhaa:
-
Ni njia ya kutegemewa ya kutambulika.
- Hujitokeza kama njia ya kukubali kwamba mpigakura amesajiliwa rasmi.
- Inaweza kujumuisha sifa nyingine za kiutambulisho (k.m. picha, sahihi,
ishara ya vidole) ili kutoa hakikisho la dhati kwamba mpigakura huyo
ndiye haswa anayejidai kuwa mwenye kadi hiyo.
- Inaweza kutiwa alama pale ambapo mpigakura amepata kuara ili kuzuia visa kupiga kura mara zaidi ya moja.
- Inaweza kupangwa kufaa wapigakura walio na viwango vya chini cvya elimu.
- Inaweza kuwa njia mwafaka ya kujitambulisha pale ambapo wapigakura wengi hawana anwani zile zile.
- Hurahisisha upigaji kura katika maeneo amabko mpigakura hajulikani kibinafsi.
- Inaweza kupeanwa pamoja na nyenzo za kuelimisha wapigakura.
Isitoshe, kunaweza kuwa na sababu nyingine zisizojulikana sana japo za
kuthibitisha uzuri wa kadi za utambulisho wa wapigakura. Kwa mfano,
kulingana na uchunguzi uliofanywa kuhusu kadi za vitambulisho zilizo na
picha, kadi hizo zilisemekana kubeba hisia za kujipenda na haki yao ya
kushiriki katika mchakato wa uchaguzi.
Kadi ya utambulisho wa wapigakura ina ubaya kadhaa:
-
Inaweza kuwa ghali kutengeneza na kusasaisha. Japo hili huwa sio
kawaida lakini gharama hizo hutokana na maswala mengi ya usalama
yanayoongezwa na kadi hiyo huja kuchukuliwa kama kitu cha kimsingi cha
kujitambulisha kinachotumiwa na raia.
- Gharama hizo za juu zinapaswa kuchukuliwa na serikali, mpigakura au
wote wawili. Ikiwa gharama inahamishiwa kwa mpigakura, idadi ndogo sana
ya wapigakura stahifu itakayopata kadi.
- Inaweza kupotea au kuibwa.
- Muundo mzuri wa usimamizi unapaswa kuwepo ili kutengeneza kadi hizo.
- Inapaswa kutngezwa na teknolojia mwafaka. Ikiwa hakuna umeme katika
vituo vya usajili na utoaji kadi, kadi hizo zinaweza kufufikwa na tabaka
nyevu au inaweza kuwa imeachwa wazi.
- Wapigakura wengine hufika katika vituo vya upigaji kura bila kadi zao.
Taratibu zinapaswa kujengwa ili kuweza kukabiliana na hali hii.
- Inapaswa kusasaishwa baada ya muda fulani. Kadi huzeeka baada ya muda
na picha zilizo kwenye kadi hizo kuchakaa. Hivyo basi, kunahitajika
mfumo wa kuzibadilisha kila mara.
- Halmashauri ya kusimamia uchaguzi inapaswa kuwa na mfumo wa kuaminika
wa kuziwasilisha kadi. Kimsingi kadi hiyo inapaswa kutengenezwa
mpigakura anapojisajili japo huenda hili haliwezakani.
ID cards for voting ( Advantages )
Personally I will prefer the cards to be produced and handed over to the rightfully registered voter on site against signing off of an acceptance and adherance sheet. Such cards MUST be based on Biometrics with AFIS registration.