Kwa kuwa upigaji kura siku zote una mahitaji ya urai na ukazia, wapigakura wengi huishi katika nchi na eneo la upigaji kura wanamoruhusiwa kupiga kura. Hata hivyo, raia wengine wasio na makao ya kudumu ughaibuni wanaweza kudumisha haki yao ya kupiga kura na hivyo basi kujisajili. Isitoshe, wapigakura wengine wastahifu watakuwa katika nchi japo mbali na maaeneo yao ya kupigia kura wakati wa uchaguzi; wao pia hudumisha haki yao ya kupiga kura. Aidha, katika hali za ubaada- mizozo mara nyingi huwa kuna sababu kinaishi za kupanuliwa kwa haki za kupiga kura kwa watu ambao hivi sasa wanaishi nje ya nchi kama watoro, wakimbizi au wakiwa na hadhi nyingine katika nchi zao za makazi.
Kufikia hivi karibuni, wanakeshi waliotumwa ng’ambo ndio waliokuwa raia tu walioruhusiwa kudumisha haki za kupiga kura na kujisajili wakiwa nje ya nchi. Kwa kuwa wapigakura hawa mara nyingi huendelea kuwa na makao katika nchi zao za nyumbani, wanaweza kugawiwa kituo fulani cha upigaji kura. Kuhama kwingi kutokana na shughuli za kikazi kumepanua idadi ya wananchi wanaoenda kufanya kazi ughaibuni, hasa katika Muungano wa Ulaya, na mweleko huu umepanua idadi ya wapigakura wasio wakazi. Watu wanaweza hata kuwa na haki kupiga kura katika nchi yao ya uraia sawa na wanavyoweza kufanya katika nchi wanamoishi. Uwezo ulioimarika wa raia kusafiri na kufanya kazi ughaibuni unafanya shughuli ya kupanga usajili na upigaji kura kuwa nzito.
Ukosekanaji wa Muda Ughaibuni/Ugenini
Kwa wakati wowote ule, idadi ya raia wa nchi watakuwa wakifanya safari fupi fupi ughaibuni. Watu kama hao wanaweza kuruhusiwa kusajiliwa. Nchi nyingine huruhusu usajili kwa watu wanaoenda ughaibuni kwa sababu maalumu kama vile masomo au biashara; kubalisha makao hakuwezi kuwa sababu ya kukubalika. Mikakati inapaswa kupangwa ili kujumuisha wapigakura stahifu walio nje ya nchi wakati wa usajili na upigaji kura; hii inapaswa kujumuisha usajili wa mapema au usajili kwa kutumia barua.
Kando na wanajeshi na wafanyakazi wengine maalumu waliopangiwa shughuli hiyo, kama vile raia waliohamishwa kwa shughuli za kidiplomasi, hakujakuwa na vipengele vyoyote vingi vya kuwaruhu raia wanaoishi ughaibuni kupiga kura. Hata hivyo hili linabadilika. Raia walio nje ya nchi siku hizi huruhusiwa kuomba kusajiliwa na kupiga kura kwa kura maalumu. Wakati mwingine wanaweza kupiga kura kwa kuwakilishwa. Kuwaruhusu kupiga kura kunaweza kuwa ghali lakini mwelekeo huo unalenga kuutokeza upigaji kura nje ya nchi kama kama haki ya raia.
Usajili na Upigajikura wa Anayekosekana Baada ya Mizozo
Hivi majuzi, katika hali nyingi za baada ya mizozo, raia wanaoishi ughaibuni wamepewa haki za kujisajili na kupiga kura katika nchi zao asilia. Kufanya uchaguzi huru na wa haki katika hali hizi ni tatizi, hasa kwa sababu wengi katika raia wanaoishi ughaibuni hawawezi kuonyesha stakabadhi zao rasmi na asilia kutoka kwa nchi zao za asilia. Bila stakabadhi rasmi kama vyeti vya kuzaliwa, pasi au vitambulisho, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kutaka kutegemea stakabadhi zozote zitakazokuwepo – kwa mfano, stakabadhi za kutoka kwa mashirika ya kimataifa zinazothibitisha hali ya ukimbizi wa mtu huyo. Katika visa vingi, jumuia ya kimatifa imeshirikishwa, kusaidia katika usajili wa wapigakura na upigaji kura wenyewe katika mazingira ya kigeni. Wakati mwingine halmashauri za kitaifa za kusimamia uchaguzi zimetumiwa kuendesha chaguzi za raia wa kigeni wanaoishi katika nchi yao.
Katika kisa cha hivi karibuni, usajili wa wapigakura katika uchaguzi fulani ulianzishwa na simu. Wapigakura waliotaka walitoa habari za kina kuhusu utambulisho wao na kisha walitumiwa fomu ya kitarakilishi, ya kutiwa saini na kutumwa huko pamoja na nakala rudufu za stakabadhi zozote walizokuwa nazo. Yeyote ambaye ombi lake lilikataliwa, angekata rufani kwa shirika lolote maarufu la kimataifa.